Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani imezuia watu wasiokuwa wanafunzi na wafanyakazi wa chuo hicho kutumia Viwanja vyake kufanyia mazoezi,
Kumekuwa na idadi kubwa ya watu wanaoishi ndani ya chuo hicho mfano watoto, ndugu au wake wa wafanyakazi wa chuo na wengine wanaoishi maeneo ya ya jirani na chuo hicho kwenda kufanya mazoezi ya viuongo asubuhi au jioni kwa mtu moja moja ama vikundi,
Lakini katika hali ya kushangaza Uongozi wa chuo hicho kupitia askari wake (Auxiliary Police) wamekuwa wakiwazuia watu kuingia na kufanya mazoezi katika eneo la chuo, kwa kile wanachosema wameagizwa na uongozi wa chuo kupitia kwa mratibu wa michezo kuzuia watu kutumia viwanja hivyo mpaka upate kibali, Lakini watu wanapoomba vibali vya kufanya mazoezi katika viwanja hivyo huwa hawapewi.
Sasa tunajiuliza kama lengo ni kuweka utaratibu wa kutambua watu wanaotumia viwanja au lengo ni kuzuia kabisa watu wasio wafanyakazi au wanachuo kufika katika viwanja hivyo,
Sehemu za mazoezi ya viungo kwa mji wa Dar ni changamoto ndiyo maana watu hutumia viwanja vya michezo vya shule za msingi na sekondari hasa nyakati za asubuhi na jioni maana viwanja vya wazi vilishavamiwa na ile bomoabomoa ya nyumba zilizonjengwa maeneo ya wazi nao ulikufa kibudu!!
Chuo kikuu cha Dsm ina kitengo cha physical education sasa inashangaza chuo ambacho kingetumika kuhamasisha watu kufanya mazoezi inazuia watu kufanya mazoezi katika eneo lao.na wamekwenda mbali zaidi (auxiliary police) hata km unapita tu eneo la chuo ukiwa na nguo za mazoezi wanakuzuia km huna kitambusho cha uanafunzi au mfanyakazi.
Je shule za msingi na sekondari za Dar nazo zikisema ziwazuie wasio wanafunzi kutumia viwanja vyao itakuaje nao sio wote wenye uwezo wa kwenda gym na sio kila zoezi hufanyika gym,
Tunaomba wanaohusika waliangazie hili zuio, maana nimeona viongozi mbali mbali wa serikali wakihimiza watu kufanya mazoezi, sasa tunashangazwa na uamuzi huu wa UDSM maana umuhimu wa mazoezi wanaujua lkn pia changamoto za sehemu za kufanya mazoezi inajulikana.