J ni mwanaume shupavu na rijali.Huku nilipo ni mwezi Sasa tangu watuweke kwenye LOCKDOWN ya lazima shughuli zinaanza saa 1 asubuhi hadi saa 9 mchana baada ya hapo ni marufuku kutoka nje.
Natumia muda mingi online, jans nimemwona dada mmoja Instagram amenikumbusha mbali sana kipindi hiko Lowassa ndio waziri mkuu, tukiwa "teenagers".
Nilikuwa form 4 Baada ya kupiga mock EZEB, likizo ile ya June nilienda kwa msela Wangu J kupiga stori mtaa wa 3 kutoka home, katika stori akanimbia oya halafu kuna demu m1 hivi hapo jirani anakuulizia anataka umpigie mapindi ya form 3 , twende tukamsalimie, nikasema poa twende coz nilikuwa najiamini nimeshamaliza topics zote form 1 hadi 4, notices za (Math. za HYDEN, Bios. & Chem. za MBUGA, Physics. za OSAMA)
Ah ile kufika pale kwa T, mtoto wa kishua geti kubwa mlinzi juu,mtoto T alikuwa anasoma form 3 (Saint....... Boarding school ) , tukakaribishwa na beki 3 na juice juu, bac nikakaa kibarazani na T katika kuongea somo lipi na topic gani nimfundishe, akasema yeye yupo mchepuo wa Arts, kwahiyo Math na Bios itakuwa poa.
Bac akaenda ndani kuchukua vitabu ili tuanze pindi, sasa namcheki msela J simwoni nikajiuliza jamaa kapotea wapi ila sikujali sana, T karudi na vitabu vya Math. Na Bios, bac nikaanza kumpigia maswali ya "Exponential na Function" kama dakika 20, T akanimbia "ai jamani hesabu ngumu kichwa kinaniuma" (Huku kama ananiegemea hivi mkono wake kwa Bega langu, mwili ukapigwa shoti [emoji51][emoji51]) , bac nikamwambia poa tutaendelea kesho, akasema tupitie na Biology kidogo, nikasema poa tuanze na "Nervous System", akasema hiyo nimfundishe kesho, yeye anataka tuanze ya "Reproduction", nikasema kimoyomoyo, "ohoooo mbona kazi ipo hapa mamaa mbona kesi hii", na udomo zege wangu ukijumlisha sijawahi kunyandua, Nikashikwa na aibu kiaina, nikajikuta nimeropoka "nimesahau kusafisha banda la nguruwe home mama akirudi mapema utakuwa msala" [emoji23], T akacheka kisha akasema "Unaogopa nini, tupitie hata introduction tu"
Nikasema poa, ile naanza kusoma sentensi ya 1, 2,3 (huku nawaza dodo hili nimeokota chini ya mnazi, makopakopa kibao[emoji3590][emoji175][emoji177][emoji179] kichwani navuta picha ya mimi na T tunafunga ndoa [emoji7][emoji7][emoji8][emoji8]) mara nasikia piii piiii, dingi yake amerudi , T akaniambia dingi hana noma maana tunasoma, dingi yake akaja hadi pale kibarazani nikamsalimia fresh tu akasema "someni sana vijana" akaingia ndani.
Nikamwambia T, msitue J tuondoke akasema poa, khe hata sekunde 5 hazijapita tunasikia makelele ndani "niachie nasema niachie" ah ile kuingia sebuleni namkuta baba T kashikana shati na J,
J ana shati na boxer tu, kumbe muda wote ule nipo barazani, J alikuwa ananyanduana na beki 3 ndani [emoji23].
Bac mlinzi akaja pale tukawaachanisha, yule mzee kakasirika sana "yaani mimi nimejenga nyumba nyie mmekuja kufanya ufuska wenu kwangu, Maiko (mlinzi) mfungulie Bibirela", T akasema ondokeni anamfungulia mbwa, bac mimi na J miguu kisogoni mbio kufika karibu na geti tu nasikia "wof wof wof" nikasema Ohooh J tunakufa leo, tukatoka nduki, mimi breki ya kwanza home, uzuri nilikuwa sina kitambi kipindi hiko bado sijawa "Okonkwo" , speed nilikuwa ninayo.
Kesho yake nikasepa nikaenda kujichimbia "camp la form 4 la washikaji zangu Sinza" sikuonekana mtaani hadi likizo ikaisha, T akarudi boarding, yule beki 3 sijui kama alirudishwa kwao, hata J nikampotezea kama miezi kadhaa hivi. Baada ya Necta nakutana na J ndio akaniambia yule mzee alienda kumchongea J kwao Kisha akawa ananitafuta na mimi. Ah baba T bana sijui alitaka kunichongea na kwetu (na mshua wangu alikuwa mkali loh) dah utam kapata J, shida anilete mimi kwetu, angejua nilikuwa domo zege hata asingekuwa na wasiwasi [emoji23][emoji23][emoji23].
Nikawa najiuliza, kwa beki 3 tu kafanya vile, je angenikuta nimejiongeza nimembananisha T kwenye kochi si angenitoboa macho na bisbisi [emoji23].
I believe "udomo zege" ulibadili "my fate" that day.
Sent using Jamii Forums mobile app
Anafaa kuigwa na vijana wote wanaochipukia