Nimegraduate jumamosi iliyopita pale DIT
Wiki tatu kabla ya graduation nilipata kazi kwenye kampuni flani hivi binafsi baada ya kufanya vizuri sana interview yao
Ishu ilikuepo kwenye cheti lakini niliwaambia ukweli nimemaliza chuo july bado sijapewa hata transcript
Wakanikubalia kwa sharti nikimaliza tu graduation niwapelekee
Sasa kwenye graduation DS kwa niaba ya mkuu wa chuo aliahidi kutupa transcripts zetu jumanne baada ya sikukuu ya maulid
Cha ajabu ile wiki nzima imepita bila kupata transcript na mi nilikuwa nimeomba ruhusa kazini ya wiki moja ambayo iliisha tangu ijumaa,leo nimeshindwa hata kwenda job nimeamkia pale chuo ambapo ilibidi nipate transcript yangu leo lakini nimeambiwa siwezi kupata imekosewa na sikuambiwa hata imekosewa nini
Kuna baadhi wamepata lakini si wengine tumeambiwa zetu zimekosewa na haijulikani bado tutapewa lini
Jioni hii imeingia simu ya HR nimeshindwa hata kuipokea yani naona kama ataniona mzushi tu
My take;
Mkuu wa chuo Prof NDOMBA ama waziri Prof NDALICHAKO kama mnanisoma humu huyo Registrar na Examination Officer wanazingua sana wanafanya kazi kwa mazoea wiki nzima kila siku nakuja hapo nimeishia kupewa majibu ya kukera, watumbueni hao watu wawili (Registrar na EO) wanaotufanya tushindwe kuchukua matunda yetu baada ya kumaliza ukizingatia shule yenyewe ilivyo ngumu hapo