UDOM: Kivutio kikubwa cha Tehama nchini Tanzania

UDOM: Kivutio kikubwa cha Tehama nchini Tanzania

University of Dodoma (UDOM)

Public Institution
Joined
Feb 24, 2024
Posts
48
Reaction score
52
d0102d23-0335-4446-ad4c-522c636c0a35.jpeg


Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imefanya ziara ya mafunzo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kujifunza mafanikio katika masomo ya TEHAMA.

Mkuu wa msafara, Dkt. Rehema Horera katika hotuba yake alisisitiza umuhimu wa ufadhili wa Samia kwa wanafunzi wa Sayansi ya Data na Akili Bandia, huku akieleza nia ya Serikali kuongeza idadi ya wanafunzi wanaopata ufadhili huo.

fdad30ff-414a-4bc5-81a5-b81c358ed7c6.jpeg


Aidha, alipongeza jitihada kubwa zinazofanywa na UDOM kuzalisha wataalamu wabobebu katika TEHAMA na kuwataka kuongeza juhudi zaidi kujitangaza kimataifa kuvutia wanafunzi toka nchi jirani.

Kwa upande wake, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Taaluma Prof. Razack Lokina alisisitiza kuwa siri ya mafanikio ya UDOM ni utamaduni wa kujituma kwa wahadhiri na wanafunzi.

e353551c-4cc7-4a75-9154-770a37f11ee7.jpeg


Ujumbe huo ulitoa wito kwa UDOM kujitangaza kimataifa zaidi ili kuvutia wanafunzi wa kigeni. UDOM imefanikiwa katika mashindano ya TEHAMA, ikiwemo Cyber Champions na Girls in ICT.

c9fb5e54-3a40-4112-a0ed-20d7f2cef019.jpeg
 
Back
Top Bottom