Amavubi nilikuwa najiandaa kulala ila kwa hoja zako zisizo za ukweli zimenifanya nikatishe usingizi ili nikujibu hapa.
1.Kwanza awali ya yote niseme wewe Amavubi haupo Mbeya,haujawahi kushuhudia mechi za Mbeya city na wala haujawahi kuona hamasa wanayokuwa nayo mashabiki wake siku ambayo timu hiyo incheza(hii siyo point nzito nzito it is just an introduction)
2.Unasema Mbeya City ilikuwa inaungwa mkona na wananchi,wafanyabiashara na halmashauri:Kwanza nikwambie tu,halmshauri ya jiji la Mbeya ndio mmiliki wa timu hii hivyo lazima waisapoti,wananchi tunaisapoti natutaendelea kuisapoti kwani hii ndio timu yetu sisi wananchi wa mkoa wa Mbeya.Hao unaosema wafanyabiashara nao wanaisapoti kama wananchi wa Mbeya.Timu haijapoteza uungwaji mkono kutoka kwa pande zote hizo tatu labda kama una proof uiweke hapa jukwaani.
3.Unasema upepo ulibadilika ghafla baada ya wanasiasa kupenyeza agenda zao,kwanza hausemi upepo upi uliobadilika,pili wanasiasa hao waliobadili upepo huo ni akina nani?wataje ili tuje na majibu ya hoja zako mufilisi.
Upepo ulibadilika ghafla baada ya wanasiasa kupenyeza ajenda zao ambazo zilionekana kuungwa mkono na wanazi wa Mbeya City na hivyo kudhoofisha waliokua na nia njema kabisa ya kuisaidia timu hiyo bila kuegemea mrengo wa siasa>Kwenye nyekundu hapo nimeqoute maneno yako,kwanza umejichanganya mwenyewe,unasema upepo ulibadilika baada ya wanasiasa kupenyeza agenda zao tena unasema ziliungwa mkono na wanazi wa MCC FC,sasa kama ziliungwa mkono hiyo si inakuwa neema kwao?jipange upya mkuu.
4.Wafanyabiashara walihanikizwa kutoisaidia tena timu:ni nani aliyewashinikiza wafanyabiashara hao wassiungemkonao timu?je timu ya Mbeya city inaendeshwa na wafanyabiashara au Halmashauri?Wafanyabiashara wanajitolea wao binafsi na kwa mapenzi yao binafsi na si kama unavyotaka kuuaminisha umma hapa.Mmoja wa wafanyabisha wakubwa tu hapo Mbeya (simtaji kwa jina)ambaye binafsi namfahamu ambaye ni mmoja wa walezi wa timu na mpaka naandika hpa bado yupo kwenye nafasi hiyo na hajaacha kuilea timu hiyo tena hii ni pamoja na wenzake.Hakika hii ni hoja mufilisi kabisa Amavubi.
5.Hahaaa hapa nacheka tu mimi mwenyewe,Amavubi hizi habari umezitoa wapi ndugu yang?eti ahadi ya kununuliwa basi na kujengewa uwanja zimeyeyuka;nani alitoa ahadi ya kuwannunulia MCC fc basi?Mbeya city kupitia Mmiliki wake ambaye ni halmashauri ya jiji ndio walikuwa na mpango wa kununua basi,(hii mipango ilikuja baada ya kupokea milioni mia moja za Azam msimu wa mwaka jana.Katika malengo yake MCC FC haijwahi kusema inataka kujenga uwanja sasa wewe porojo hizi umezitoa wapi?acha kusambaza uongo ndugu.
6.Mashabiki waandamizi ndio mashabiki wa ain gani hao?unajua utaratibu unaotumika kusafirsha mashabiki kwenda kuishangilia timu inapocheza nje ya Mbeya?Mechi ya Stand united mashabiki walikwenda wakutosha tuu
View attachment 200634Hao ni baadhi ya mashabiki walioenda kuishangilia timu shinyanga sasa leta hoja yingine na sio hii mufilisi.
6.Financially mbeya city wapo vizuri na kila siku wanaingia mikataba minono na makampuni mbalimbali,juzi kati wameingia mkataba na cocacola,wakaingia mkataba na benki ya posta,wanadhaminiwa na Binslum tena kwa pesa ndefu kupitia RB battery sasa hiyo ya kusema financialy hawako fit unaitoa wapi?leta hoja nyingine siyo hii mufilisi.
7.Eti wachezaji wengi wamekopwa usajili,labda nikuulize msimu huu Mbeya city imesajili wachezaji wapya wangapi?halau ukishapata jibu ndio utajua kwamba kwenye hili wewe umekurupuka.
Mwisho niseme tu,wengi wanataka kujitia unabii kuitabiria mabaya mbeya city na kujifanya wanaijua sana hii timu,sasa mkae mkijua kuwa Mbeya city haitapotea na wala haitashuka daraja kama wengi mnavyoiombea.Sisi wana mbeya na mashabiki wa timu yetu ya Mbeya city tutaendelea kuiunga mkono na kamwe hatutasikiliza maeneo yenu.Tunashikilia mkia lakini mkae mkijua tu tutarudi kwenye fomu yetu.
IDUMU MBEYA CITY,WADUMU MASHABIKI WAKE,WADUMU WANA MBEYA,WADUMU WADHAMINI.
TIMU YETU TUNAIPENDA NA DAIMA TUTAKUWA NAYO.
MUNGU IBARIKI MBEYA CITY FC,MUNGU TUBARIKI WANA-MBEYA......AMEN
View attachment 200635