Udikteta katika Mahusiano unaimarisha ama unabomoa mahusiano?.

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,325
2,491
Wasalaam wanabodi,
Awali ya yote kama tujuavyo kuna msemo unasema kila kitu kina pande mbili yaani (+ve) na (-ve), hivyo hata Udikteta kuna Udikteta +ve na Udikteta -ve.

Tujadiliane Udikteta +ve katika mahusiano ambao lengo lake ni kuimarisha mahusiano. Je ni kweli unaimarisha ama unabomoa?

Chukulia mfano umeoa (ke) ambaye utambana na kumfuatilia kila hatua anayotoka, lakini pia chukulia umeoa (ke) lakini unamwacha free bila kumfuatilia chochote, anarudi muda anaotaka, kwako kila kitu sawa ilimradi unampa uhuru wote na unamtrust kwa kila afanyalo na kila anapokwenda.

Japo wanasema "Bwana asipolinda nyumba, alindae akesha bure", lakini too much freedom inaweza kuleta madhara makubwa kwani kuna wasichana ambao walilelewa kidikteta na wazazi wao ndo wakatulia kwa wazazi, sasa unapomwoa ukimpa uhuru ndipo uhuru huo unaweza ukatumika vibaya na ukaleta madhara baadae kwakuwa hajauzoea.

Lakini pia kuna wasichana walizoea kuishi kwa uhuru wakiwa kwa wazazi wao, ila akiingia kwenye ndoa anakumbana na dikteta ambaye hata kama unaenda kununua vocha lazima upangiwe muda wa kwenda na kurudi.

Tudadavue : udikteta unaimarisha mahusiano ama unayaharibu? Karibuni.
 
unazungumzia jiNsia gani ishike madaraka moja wapo kati ya hayo? au wote?????
 
Inategemeana. Kuna wanawake wengine wanajielewa, wanajua majukumuu, wajibu, mipaka yao kwenye ndoa. Hawa hawahitaji dikteta ila kama bible inavyosema, ishi nao kwa akili. Kuna wengine wanahitaji mwongozo kidogo, wanakwenda. Ila kuna wale ambao bila ubabe na kuwabana ndoa inakaa kwenye mawe. Cha msingi, mpende mkeo na ishi nae kwa akili.
Note : kwa wanawake wengine kuishi nao kwa akili kunaweza kuwa ndo huko ku apply dictatorship
 
1467566348835.jpg
 
ila wanawake huwa hawakubali udhaifu wao hivyo hujiona wanajitambua kumbe ni upeo mdogo
 
Back
Top Bottom