Katika hali ya ushindani ktk mbio hizi ndani ya CCM kugombea nafasi ya urais,Mh.Steven Massatu Wassira ameendelea kupokewa kwa kishindo ktk mikoa aliyopita kwa lengo la kupata wadhamini kuelekea kuteuliwa kuwa mgombea ndani ya Chama Cha Mapinduzi.
Katika mikoa ya na maeneo aliyopitia mpaka sasa ya Dodoma,Singida,Manyara,Arusha na Kilimanjaro, Mh.Wassira amepokewa kwa wingi sana na wanachama wa chama cha Mapinduzi wanaoonyesha kuunga mkono nia yake ya kuwania "ofisi ya kwanza" ya Nchi hii.Amedhaminiwa na makada wa ngazi mbalimbali ndani ya chama na kuvuka malengo ktk kila eneo alilopita
Mpaka sasa zoezi hilo linaenda kwa kasi na kwa ufanisi mkubwa,huku Wanachama wengi toka ngazi yofauti ya chama wakimuunga mkono.Wassira ni moja kati ya Wabunge na watia nia wenye nguvu na ushawishi ndani ya chama cha Mapinduzi hivyo kuwa miongoni kati ya watia nia wenye nguvu na ushawishi ndani ya duru za siasa za Ushindani ndani ya CCM.Huu ni mchakamchaka kuelekea Dodoma mpaka jogoo litakapowika Chimwaga!!