Udhalilishaji huu utaendelea mpaka lini?

Huyo kijana wenu katoa sababu gani kwanini hakujiandikisha daftari la wageni.
Huyo kijana yupo hapo guest toka ijumaa na alijiandikisha wao walipofika wamewachukua hapo guest hawakutaka maelezo mpaka walipofika Polisi.
Mama mwenye guest alienda jana ikashindikana kutokana na maelezo kuwa mkuu wa operations hayupo kwa kifupi mkuu ni udhalilishaji
 
Kuna vyumba vina twin bed maalum kulala watu wawili jinsia moja chumba kimoja. Tatizo kuna watu wanafanyakazi kama robot
Walikataa kata kata! Tukawauliza hivyo vyumba vyenye twin bed ni kwaajili ya nini(maana ndivyo tulivyofanyia booking) wakasema ni kwaajili ya wanawake, ila wanaume hawaruhusiwi. Ikabidi wanaume walale separate rooms.
 
Haya ni maajabu ya Tz....kama ndo mgeni umefika hapo unajuta
 
Huo siyo udhalilishaji labda useme n usumbufu, watz tunapenda kuishi tutakavyo na kulaumu laumu. Hao polisi wangekuwa wanafanya hayo kinyume na sheria/kanuni za nchi nadhan wangeshapigwa stop maana hata kwenye hizo guest house wanakuwemo watu wa aina tofauti na wengine wana madaraka serikalin lakn wanatii huo utaratibu kwa hiyo km imehalalishwa na serikali yetu tusilaumu wasimamizi wa sheria. Kwan kujiandikisha kwenye daftari la wageni?
 
Nikienda Guest kucheza mechi za kirafiki sijiandikishi au naandika jina la uongo. Lakini ukiwa Safarini ni muhimu kujiandikisha
 
Walikataa kata kata! Tukawauliza hivyo vyumba vyenye twin bed ni kwaajili ya nini(maana ndivyo tulivyofanyia booking) wakasema ni kwaajili ya wanawake, ila wanaume hawaruhusiwi. Ikabidi wanaume walale separate rooms.
Ndio hao ninaosema wanafanyakazi kama robots..hawatumii common sense
 
Ok. Hapo juu umesema sababu ni kutojiandikisha. Inawezekana kweli polisi waje guest house au hotel wachukue watu wote na kuwalaza ndani bila sababu?
 
Nikienda Guest kucheza mechi za kirafiki sijiandikishi au naandika jina la uongo. Lakini ukiwa Safarini ni muhimu kujiandikisha
Kuna siku utaona umuhimu wa kujiandikisha jina la ukweli hata ukiwa short time mgeni wa dar-dar.
 
Kwa style hiyo tusishangae kusikia ya kibiti huko Njombe
 
Unapoongea jambo jaribu kutafakali na kujiuliza ni mambo mangapi yanayofanyika kinyume cha utaratibu na fikiria kama jambo hilo lingekukuta wewe
 
Ok. Hapo juu umesema sababu ni kutojiandikisha. Inawezekana kweli polisi waje guest house au hotel wachukue watu wote na kuwalaza ndani bila sababu?
Ndiyo nimeeleza hiyo sababu hata huyo mmiliki wa hiyo guest alikuwa na kijana wake ambeye huenda hapo kusaidia kazi naye pia amechukuliwa na amelala ndani
 
Kuna siku utaona umuhimu wa kujiandikisha jina la ukweli hata ukiwa short time mgeni wa dar-dar.
Inaonekana uelewa wako ni mdogo umesoma vizuri hiyo thread
 
Inaonekana uelewa wako ni mdogo umesoma vizuri hiyo thread
Wewe huna akili. Hio post nimemjibu aliesema yeye akiingia guest house short time haandiki jina la kweli. Mwezi mtukufu huu ninachoweza kukwambia ni hicho tu.
 
Lakn jamani kwann ss wafrika hasa watz hatutaki kubadilika?Kwani ukifata sheria na taratibu kaandika jma Lako utakufa? Mambo mengne tunatafta maneno
 
Nikienda Guest kucheza mechi za kirafiki sijiandikishi au naandika jina la uongo. Lakini ukiwa Safarini ni muhimu kujiandikisha
Kuna siku utaona umuhimu wa kujiandikisha jina la ukweli hata ukiwa short time mgeni wa dar-dar.
Inaonekana uelewa wako ni mdogo umesoma vizuri hiyo thread
Wewe Nkungulume sijui karumekenge usipende kukurupuka, hio post nimemjibu huyo Gide mk sasa wewe unakurupuka. Tatizo lako unataka kila mtu aandike unachotaka kusikia.
 

Kumbe mnajua kosa lenu ila hamtaki tu kukubali?

Ingekuwa waliwakamata wote na waliojiandikisha kwenye daftari hapo ningekufikiria, otherwise no way..Muwe mnafata utaratibu.

Usisingizie vielelezo..hata aliyejilipua huko Manchester alikuwa na vielelezo vingi kuliko vyako..na hata hao wanaofanya mauaji huko pwani wanavielelezo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…