Udhaifu na uimara wa CHADEMA

Udhaifu na uimara wa CHADEMA

UTANIPENDA

Member
Joined
Feb 25, 2012
Posts
31
Reaction score
12
kushindwa kwa CCM Arumeru hakikuwa kipimo cha kuwa CCM wamekuwa dhaifu... na wala kushindwa kwa CHADEMA Kalenga sio kipimo cha udhaifu wa CHADEMA.

CHADEMA ipo na shida kubwa sana ya msingi ya uwezo wa viongozi wa ngazi za chini hasa kwenye kata na wilaya. Kwa siasa za hivi sasa ambapo CCM wanafanya siasa za kila namna huku wakisaidiwa na mfumo huu mbovu ili ashinde kwa kweli kwa aina hii ya viongozi wa ngazi za chini, wananunulika kirahisi, waoga hata wakigombezwa na balozi wa CCM unakuta mwenyekiti wa chadema anafyata mkia, yaani hamna kitu kabisa wanafurahia kuitwa viongozi wa chadema lakini hawafanyi kazi yoyote ya siasa.

Udhaifu huu uliopo kwenye uongozi wa chini unapelekea uongozi wa juu kuelemewa na kuonekana dhaifu.

Kuongoza chama cha siasa ni kazi kubwa sio kama wanaJF tunavyobeza beza kienyeji enyeji. MBowe na sekretariat ya chadema wanajitahidi sana na huu ndio uimara wa chadema, tatizo huko chini hakuna viongozi wenye uwezo, yaani wana shida nyingi sana.
 
Chadema ni dhaifu tuuu haina uimara wowote
 
Nakuunga sana mkono kamanda.Shida watu wengi wanashindwa kuelewa wapi Mbowe na Slaa waliitoa CHADEMA.Kwa kweli ni juhudi zao binafsi na upendo wao kwa Watz.
 
Uimara wa chadema uko sero na udhaifu wake kila mtu anaujua..UKABILA, UTAPELI NA LUGHA CHAFU
 
CHADEMA waanzishe biashara ya HELIKOPTA nahisi watafanya vizuri kusafirisha abiria kwa CHOPA kuliko SIASA
 
Kuongoza chama cha siasa ni kazi kubwa......., tatizo huko chini hakuna viongozi wenye uwezo, yaani wana shida nyingi sana.
images
 
kwa taarifa yako sio kweli kuwa ccm walishindwa arumeru bali walihujumiana kati ya kambi lowassa-sioi sumari (mgombea)---- na kambi sitta-nape-magufuli-mwakyembe----
upinzani tanzania ni kama umelaaniwa, mfano chadema wahafidhina badala wajipange vizuri wanaanza kuwatua tena watu muhimu kama Zitto. Dr. Kitila, na mwigamba. sasa kwa nini ccm wasitawale milele? ubaguzi haunaga rangi.
 
Mgonjwa
 
Back
Top Bottom