TheMeek
JF-Expert Member
- Mar 12, 2016
- 460
- 400
Ndugu wana jamvi,
Habari zenu!
Napenda kuchukua fursa hii kuelezea machache kuhusu suala la Ugaidi Tanzania; Lakini pia, kushirikiana nanyi kimawazo/kulidadisi suala hili ili kulifanya Taifa letu kuwa salama wakati wote.
Ninavyoelewa Mimi, Ugaidi ni Vita ya Kiimani, yaani Imani potofu au kwa maana nyingine Elimu potofu.
Ni watu wachache sana wenye uelewa ( imani endelevu) kuwa , nyakati tulizonazo sasa ni nyakati za hatari. Namaanisha , kukithiri kwa rushwa ( Upotoshaji) kumewaathiri watu wengi katika mataifa mbalimbali ikiwemo TANZANIA.
Rushwa imewafanya watu wengi kutofikiri sawa sawa, kukosa maono, kukosa namna ya kutatua CHANGAMOTO zinazowazunguka katika misingi ya Haki, Demokrasia na Maendeleo. Tatizo hili lipo kwa Wananchi wengi na hata kwa viongozi wengi wa Serikali /Taasisi binafsi.
Tatizo la Rushwa pia limesabisha kuwepo kwa Familia Ovu, Jamii Ovu na Taifa lililojaa mawingu meusi yenye giza Kali ( Mawingu Haya ndio yanatufanya tuendelee kukaa na kutembea kizani wakati wote, huku tukijiaminisha kuwa tupo salama)
Mbaya zaidi, kutokana na Rushwa kushamiri, Taifa letu limekuwa likiwaamini sana watu wenye Ujuzi (Knowledge) na kuwapuuza wale wenye Uelewa (Understanding).Hii imesababisha kuendelea kuwepo kwa migogoro mingi na kujirudiarudia kwa matatizo mbalimbali.
Nikiwa na maana ya kwamba, viongozi wenye Ujuzi mara nyingi husuhurisha migogoro kwa muda mchache tu (na kisha migogoro hiyo kujirudia) lakini sio permanently kama ilivyo kwa wale wenye uelewa.
Nataka kusema kwamba, kutokana na hali tuliyonayo hivi sasa ( ya maasi kuongezeka) ulimwenguni kote , ni vyema sasa , Serikali ikawatizama watu wenye maono na wenye Uelewa mpana kuhusu masuala mbali mbali ili kulinusuru Taifa letu katika kadhia hii ya kigaidi inayoweza kujidhihirisha wakati wowote kuanzia sasa katika Taifa letu.
Ni vigumu sana kuliondoa tatizo la Ugaidi kama likijidhihirisha katika Taifa letu. Viongozi na Wananchi wote kwa ujumla wanapaswa kutambua kwamba , kuilinda, kuitunza na kuiendeleza Amani, Umoja na Mshikamano ni gharama sio lelemama kama ilivyozoeleka.
Tunahitaji kushirikiana na vyombo vya usalama kuhakikisha Taifa letu linakuwa salama wakati wote.Ni wakati pia, vyombo vya Usalama kuvichukulia hatua vyombo vyote dini na vya habari vinavyohamasisha tabia za kigaidi.
Elimu pia ni muhimu ikatolewa kwani fikra za watu wengi ulimwenguni (wakiwemo baadhi ya watanzania) wanatambua kuwa Ugaidi ni Uislamu , ili hali ukweli sio hivyo.
Vyombo vya Usalama vinapaswa kutambua kwamba, kadhia hii kama ikijidhihirisha katika Taifa letu, itakuwa ya Hatari sana ukizingatia, masuala ya udini kuongelewa chini chini yameshamiri sana katika Taifa letu ( sasa ni dhahiri kwamba waislamu wanaona kama wanaonewa na kutopewa kipaumbele katika masuala mbalimbali) ; Minong'ono hii ni lazima ifanyiwe kazi na kukemewa mapema ili kuondoa chuki, hasira na ubaguzi.
Uelewa ni Silaha pekee itakayoweza kuilinda,kuisimamia na kuiendeleza Tanzania. Elimu ni Uelewa. Ni lazima sote kwa pamoja kwa kushirikiana kuipiga Vita Rushwa katika nyanja zote kwani Rushwa ni Adui wa Uelewa ( Elimu). Rushwa ni Ujinga, Rushwa ni Upumbavu, Rushwa ni Ulofa, Rushwa ni Ugaidi, Rushwa ni Ushoga, Rushwa ni Ufisadi, Rushwa ni Nkurunzinza, Rushwa ni Umalaya , Rushwa ni Adui wa Haki, Demokrasia na Maendeleo!
Asanteni Sana.
MUNGU IBARIKI AFRIKA , MUNGU IBARIKI TANZANIA