UCL Final: Tutegemee kuona nini katika fainali ya Madrid Vs Liverpool

Mimi naamini mabeki wataamua mchezo wa leo ikiwemo kufunga magoli, nategemea game itaenda 120 lakini haitofika penati. Nampa Real Madrid ushindi wa 3-1

Tupia utabiri wako hapa halafu tukutane baada ya mechi kuisha.
 
Liverpool kipigo cha mbwa koko kinamhusu. Atakula 4 bila na kati ya hizo ronaldo atapiga hatrick yake
 
1.china-win
2.Madrid-win
3.new York red bulls-win
4.kups- win and
5.palmeiras- win
kwa Leo natoa hizo
 
Michuano ya kutafuta klabu bingwa barani Ulaya itafikia tamati leo katika mchezo wa fainali utakaochezwa majira ya 21:45 Usiku.
Fainali hii inavikutanisha vilabu vya Real Madrid kutoka Uhispania(bingwa mtetezi) dhidi ya Liverpool kutoka Uingereza.

Nani kuibuka bingwa wa ulaya usiku wa leo??
Cc;@mussolin5 Kunguru Mjanja Somji Juma Ghazwat
 
Kwa taarifa tuuuu!
IMG_20180526_145743_206.JPG
 
Liverpool wana dakika 40 za kushinda yaani zile za dakika 40 za mwanzo kabisa na hii inatokana na aina ya uchezaji wao na pumzi pia,hawa jamaa hawana kabisa pumzi kuanzia dakika ya 60 salah,mane huwa wanakata pumzi kabisa huku Liverpool ikiwa haina mbadala wao huko nje

Madrid wana ushindi wao kuanzi dakika ya 70 huwa wako njema sana hapo

Yote kwa yote muda utaamua
 
"Kidogo kwa kina kuelekea mchezo huu" Anzia kwenye goli la Dzeko rudi nyuma. Liverpool weakness yao kubwa inaanzia kwenye mipira yakutupwa(set pieces). Hapa Lovren na VVD wanakwenda kukutana na wapigaji wa mipira hiyo na waumini wa mipigo hiyo(Marcelo na Carvajal). Sio tu waratibu wa mipira ya krosi ila pia ni miongoni mwa watumiaji wazuri wa mipira hiyo, eidha watengeneze wenyewe au watengenezewe. Hapa kazi kubwa inaanzia kwenye miguu ya Robertson na Trent Arnol, japo Robertson ni fundi mwingine kwenye kumwaga maji golini.

Achana na mitupo inayozalishwa kwenye mashavu ya Real Madrid..... Tuachane na udhaifu wa ku clear mipira inayoelekezwa kwenye lango la Liverpool. Kumbuka Christian Ronaldo "Mnyama" ni master katika kutumia "single touch", kwa maana ya kutumia mipira inayoelekezwa kwenye box la mpinza bila kutuliza(hapa CR7 huwa anaonganisha vivyo hivyo).
Ni rahisi kumfanyia man making kuliko kumtight wakati ana spring kucheza high balls...... Na Hapa ndipo Liverpool wanapotakiwa kuanzia. Hakuitaji height ya VVD Pekee "LA Hasha", Gloves za Karius zinahitaji mzimu wa Dudek.

Binafsi naungana na Babu Jupp Heynckes. katika mapungufu ya Real Madrid msimu huu basi ni kuruhusu mpinzani atengeneze nafasi nyingi zaidi katika lango lake.

Hapa makali ya utatu wa Liverpool(Mane, Salah na Firmino) Yanakuwa ya moto zaidi wanapokutana na eneo la ulinzi lililotetereka... Kasi yao, zile zigzag movements za utatu ule wakati wanapokuwa wanashambulia na hata kushambulia Kwa kushtukiza kumekuwa na hatari Sana sababu ya pressing yao.

Anzia kwenye goli la Kimmich tu pale Alianz Arena, Kabla ya mchezo wa nusu Fainali ya pili Kule Bernabeu. Kupungua kasi, ubora na kutumika Kwa muda mrefu katika ubora isiopishana Sana kwa Ramos na Varane.

Kumewafanya kuwa wahanga wa mashambulizi yanayofanywa kwa kasi. Kutokana na impact kubwa ya walinzi wa pembeni(Marcelo na Carvajal) ni katika kusapoti mashambulizi. Hii imekuwa ikiongeza idadi kubwa ya wachezaji kuanzia katikati kwenda mbele, na kuwafanya Ramos na Varane kujikuta wakiwa wachache wakati shambulio la Haraka zaidi.

Kwa ile kasi ya Salah, Mane na Firmino, ni hatari sana Kwa eneo la ulinzi la Madrid chini ya captain Ramos.

Moja ya sehemu imara zaidi Kwa Madrid ni eneo linalomilikiwa na Mondric, Casemiro na Kroos. Hawa ndio wamekuwa wakiamua timu ichezeje sasa na mipira ielekee wapi Kwa wakati. Kama Isco atapata nafasi ya kuanza basi eneo hilo huwa na Ugumu wa uratibu Kwa mpinzani Kutokana na kuwa na idadi kubwa ya watu katikati Haswa wakati aakushambulia.

Pressing high up(kukabia juu) ambayo wamekuwa wakiifanya washambuliaji watatu wa Liverpool(Salah, Mane na Firmino). Imekuwa ikitoa Mchango mkubwa zaidi kwa viungo wa kati(Milner, Hendo na Can). Hapa namna Liverpool wanavyoshambulia, wanavyokabia juu ndio imekuwa silaha yao kuu ya kujilinda Pamoja na madhaifu waliyonayo kwenye backline.

Trent ni mzuri Sana kwenye kuzuia na kusapoti timu kucheza zaidi kwenye kiungo. Hii ni sawia kabisa na aina ya uchezaji wa Carvajal.... Bahati mbaya zaidi Trent Alexander Arnold anakutana Kwanza na Marcelo na Francisco Allarcon "isco" kwenye upande anaouhudumia. Lakini pia bahati nzuri zaidi ni Andrew Robertson atakabiliana na Dani Carvajal kwenye upande ambao ndio kiini cha Ustadhi Sadio Mane.

Uimara Kwa Navas na Karius unaweza kuubeba mchezo mpaka 120. Ila nje ya hapo Vijana wa Klopp wanahitaji kuwa makini zaidi na mipira iliyokufa(dead balls) sababu Madrid ni master Sana kwenye kutumia Kona na Faulu kukuadhibu.

ila pia vijana wa Zidane wapaswa kuwa makini Sana na mashambulizi yakushtukiza. Hapa Liverpool wanakuwa superb Sana kwenye counter attack na unapokuwa na uchache kwenye ulinzi ni ngumu kupona.

Real Madrid Vs Liverpool
 
Ronaldo atapata red card mapema sana, sadio mane ataamua mchezo baada ya beki kindakindaki wa wakubebwa fc kufanya kosa la kizembe sana.
NB: game haiendi dk 120
FT: LFC 2 - RM 1
Mimi namba zangu zinaniambia hivyo pia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom