Uko kwenye dawati la Mkuu wa Mkoa na FBI wa kuchonga.
Watawala Wanacheza na damu za watu. It won't let them free. Always hunted by guilty concsiounsness kwa muda mfupi waliobakiza kuwa madarakani kisheria (si kihalali), kabla kila mtu hajabebeshwa mzigo wake, kwa matendo yake na kauli zake.
Watoto wadogo wale, wakitoka madarasa, wameuwawa kikatili, wengine wanaugulia majeraha na vilema vya maisha, huku wengine wakiathirika kisaikolojia na kuhitaji msaada mkubwa...kilio chao hakiwezi kwenda bure.
Damu ya kamanda Judith William itaendelea kudai haki na utu wa mwanadamu. Watawala wana kihoro. Zaidi ya mwezi mzima sasa hakuna taarifa yoyote, no even a preliminary report, why?!
Machozi, jasho na damu...hazitawaachia, hata kama wataficha ukweli kwa muda wa kibinadamu.
Serikali inayoshindwa kuwajibika kwa uhai na maisha ya raia wake...ina uhalali gani machoni pa waliopatia dhamana hiyo?