Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,389
- 38,667
Kuna dhana isiyo sahihi miongoni mwa wanasiasa wetu na baadhi ya wananchi kwamba ujenzi wa Miundombinu pekee ndiyo suluhu la tatizo la uchumi wetu kuwa nyuma. Inaonekana kama vile ujenzi wa Majengo,Barabara,Reli, Madaraja,na hata viwanja vya ndege ndiyo uwekaji vitega uchumi. Kuwa na miundombinu si lazima miundombinu hiyo iwe ni kitega uchumi.
Nchi kama Marekani ilipoingia kwenye janga la kuporomoka kwa Uchumi wake si kwamba ilikuwa haina hiyo miundombinu ambayo hapa kwetu ndiyo tunaona kama tunawekeza kwenye vitega uchumi. Barabara, Reli,Majengo,na viwanja vya ndege vya ubora wa hali ya juu sana vilikuwepo wakati wa dhahama ya uchumi ilipotokea huko Marekani kuanzia mwaka 2007 na kuendelea.
Na mafanikio ya Uchumi wa nchi yanapimwa kwa kufaidisha watu wengi na si kikundi kidogo tu cha watu. Kwa mfano Ujenzi wa majengo makubwa na marefu yanayojengwa na mifuko ya Hifadhi ya Jamii katika miji mikubwa ya nchi yetu, yamebadili nini kwenye maisha ya wafanyakazi wanaochangia kwenye mifuko hiyo?
Tumetumia Bilioni kumi kujenga Mabweni ya wanafunzi pale Chuo Kikuu cha Dar es salaam, je tija yake kiuchumi inamfikiaje Mvuvi aliyeko Karema Wilayani Mpanda Mkoani Rukwa? Mpaka sasa tumeshapima hasara na faida inayotokana na kutumia fedha za mifuko ya Jamii kujengea Chuo Kikuu cha Dodoma pamoja na Daraja la Kigamboni?
Nchi nyingi tunazozisikia kwamba zimeingia kwenye migogoro ya kiuchumi si kwamba hazina miundombinu. Miundombinu inayoleta tija kwa jamii ni ile tu inayojengwa kwa kufuata uhitaji wa kiuchumi wa jamii husika kwa lengo la kurahisisha ugavi kwa bidhaa zinazohitajika kwenye soko.
Tuna Tanzanite ambayo inachimbwa nchi mwetu tu. Tumewahi kujiuliza India kuwa ndiyo nchi inayoongoza duniani kwa kuuza kwa wingi Tanzanite iliyosafishwa kunatokana na ubovu wa miundombinu yetu ama kunatokana na nini hasa. Hata ule mchanga unaosafirishwa kwenda nje ya nchi ili ukasafishiwe huko tatizo ni ubovu wa miundombinu yetu ama tatizo ni kitu kingine kabisa?
Jee tunajua tunatakiwa kufanya nini ili uchumi wetu ukue!? Wasomi na wataalamu wetu wa kiuchumi ndiyo wanashauri kwamba uwekezaji sahihi kwa watakati huu ili uchumi wetu ukue ni ujenzi wa miundo mbinu? Tanzania ndiyo soko Kuu la bidhaa toka Kenya kwenye soko la Afrika Mashariki. Jee tunanunua bidhaa toka Kenya kwa kuwa Kenya wana miundombinu mizuri zaidi kuliko sisi?