"Uchotara" ndani ya Tanzania - Ni sehemu ya historia

2kimo

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
2,029
2,072
Katika makala nyingi za historia ya Tanganyika zinaoensha kuwa watu wa jamii za Asia na ulaya ni miongoni mwa wakazi wa kudumu katika jamii zetu! Makala za historia ya Dar es Salaam zinaonesha kati ya miaka 1920s Dar es Salaam ilikuwa na wakazi kati ya 20,000 - 35,000 miongoni mwao 4000-5000 walikuwa wahindi/waasia na 500-1000 wazungu! Idadi hii ni karibu robo ya wakazi wote wa Dar es Salaam si wabantu! Na miaka ya 1930s idadi ilikuwa 130,000 na wazungu walikuwa karibu 5000, wa Asia 30,000 ambapo hawa walikuwa wanakaribia kufikia theluthi ya wakazi wote! Kumbuka among Bantus wapo ambao walikuwa mixture!
Nadhani historia ipo ili tujifunze na kisha tuyafanyie kazi haya tunayoyasoma!
Hatuna haja ya kuwaona wahindi, waarab na wazungu ambao ni wakazi wammuda mrefu wa nchi hii na kuwachukulia kuwa wao ni wageni na haki yao ni ya pili baada ya wabantu!
Tumekuwepo ktk uwiano maalum toka vizazi vilivyopita na sidhani kama kuna mtu haki yake ya msingi inaongezwa au kupunguzwa kutokana na rangi ya ngozi yake!
Kama yalivyo makabila mwngine na asili zake ambapo wengi asili ya makabila yetu ni nchi za mbali kama Somalia, Ethiopia,Africa ya kati au Magharibi, then hii diversity ya race ktk jamii zetu ni inevitable! Mungu ameumba hivyo, circumstances zinalazimisha hayo yatokee na hayaepukiki! Leo tusubiri vizazi vya kichina kuwa ni miongoni mwa jamii za watanzania, hili hakiepukiki pia! kwa wale waislam wamkumbuke Bilal ktk zama za Mtume Muhammad (S.A.W) alikuwa ni mwana jamii mtu mweusi ktk ardhi ya waarabu, hiyo ni zaidi ya miaka 1400!
Jamii hukua na kuimarika inapotokea diversity, jamii ya aina moja ikikaa pamoja hudumaa!
Yatupasa kukemea hali zozote zinazodhoofisha misingi ya umoja inayopindishwa kwa tofauti zetu za dini, kabila, rangi ya ngozi na namna nyingine za ubaguzi!
 
Thread yako imejaa kweli tupu na ukomavu. Amerika imeendelea kwa sababu ya mchanganyiko wa mataifa yote duniani!
 
Ikiwa ubaguzi unaanzia penye ngazi ya familia au ukoo tegemea hilo katika ngazi ya kijamii pia.Na katika hayo makundi uliyoyataja wahindi ,wazungu na waarabu waqt wapo hiyo dasalama unayoisema wenyewe walimuweka mbantu katika darja la mwisho na kiakili wamejengwa hivyo kuwa wao ni bora kuliko nywele ngumu.Ni jambo baya sana kubaguana kwa namna yoyote iwe kwa ngozi,hadhi au kipato lakini halijaanzia hapa lina trend ndefu.
 
Nakubaliana nawe asilimia kubwa, kiukweli ubaguzi upo kila mahali lakini nchi nyingi zinapinga ubaguzi (serikali) na sio wananchi wote lakini sheria zetu ni tofauti kabisa na wazungu. Kwa mfano UK utakuta serikali haina ubaguzi kabisa ni wewe na elimu yako kwani bunge lao wapo wenye asili ya Africa na Asia mpaka house of Lords wamo na wanapiga kazi vizuri, wameenda mbali zaidi na kuwaomba raia vwenye asili tofauti na wao wajiunge na jeshi la polisi kwa mfano wachina polisi utawakuta China Town na wahindi wengi tena unamkuta kavaa turban halafu polisi London.

Kweli foreigners walikuja zamani sana hapa na wamezaliana na kuoleana pia lakini wanapoingia kwenye shughuli za serikali wanabaguliwa kama yaliyotokea Mwanza,
Nafikiri serikali ingeajiri na kuwapa kazi sehemu zote kama jeshini,polisi, wizarani ili kupunguza racism katika jamii kwani nchi kama Brazil hawana ubaguzi kabisa na hata jirani zetu Kenya wasomali wapo serikalini tena wizara nyeti.

Ifike mahali tukemee ubaguzi kwani pindi mtu anapozaliwa mahali popote hapo ndio kwake
 
Ikiwa ubaguzi unaanzia penye ngazi ya familia au ukoo tegemea hilo katika ngazi ya kijamii pia.Na katika hayo makundi uliyoyataja wahindi ,wazungu na waarabu waqt wapo hiyo dasalama unayoisema wenyewe walimuweka mbantu katika darja la mwisho na kiakili wamejengwa hivyo kuwa wao ni bora kuliko nywele ngumu.Ni jambo baya sana kubaguana kwa namna yoyote iwe kwa ngozi,hadhi au kipato lakini halijaanzia hapa lina trend ndefu.
Yesu aliposema samehe saba Mara sabini alikuwa ana maana kubwa sana!
Ukisamehe ubaguzi nawe hautabaguliwa!
Dhambi uliyosamehe daima haitokupata!
Kwa kuona ubaguzi ni kitu cha kawaida au tunapaswa kuwalipizia waliotutendea dhambi Mara nyingi tunaendelea kuishi na machungu tu!
Ukizungumzia yaliyotokea kabla ya 20th century hakuna wa kulaumiwa, mifumo wa kibeberu ilitawala dunia, matabaka yalijengwa na mfumo huo wa dunia, sasa hv mambo yamebadilika!
Ila kwa bahati mbaya hayo matabaka mengine hata kama tutapenda kuyabagua tunajiumiza tu, tunawategemea zaidi kuliko wao kututegeea when it comes to issues za mtu na mtu!
Pia suala la madaraja ya kipato yapo hata ktk familia zetu, lkn sio kitu chema!
 
Hakuna anaepanda kubaguliwa au kubagua kama ana akili timamu wawe wazungu,waarabu au waafrika tatizo limeanza karne nyingi labda nini kifanyike ndo la msingi ila kiakili jamii nyingi zimejengeka hivyo ni mbegu inayotakiwa ichomwe moto.
 
hawa wenzetu nao wanakasumba zao wapo wanyamwez wenzangu wa chuma cha nkola choma igulubi, usoke sasa waambie nyny wanyamwez kabila lao la passport wanawakaa hao wajomba zangu wazaramo wa kariakoo nao miaka nenda rud yupo kariakoo huko Gujarati anakusikia ila atukwita veve sio ww tena SOTE NI NDUGU ILA
 
Lakini ubaguzi upo sana hapa - hata baadhi ya makabila kiafrika yanabaguliwa na kudharauliwa sana
 
hawa wenzetu nao wanakasumba zao wapo wanyamwez wenzangu wa chuma cha nkola choma igulubi, usoke sasa waambie nyny wanyamwez kabila lao la passport wanawakaa hao wajomba zangu wazaramo wa kariakoo nao miaka nenda rud yupo kariakoo huko Gujarati anakusikia ila atukwita veve sio ww tena SOTE NI NDUGU ILA
Duh!nenda puge sijui nkiniziwa au itogwanholo rangi tu ndo itakutambulisha lakini wanajua kutengeneza ntwili hao ila unyamwezi au umanyema hawajinasibishi nao.
Ndo maana tunasema akili za watu wengi sio suala la uarabu na uafrika ni la kijamii mswahili kwa mswahili wana baguana hali kadhalika mwarabu kwa mwarabu ukianza kutajiwa kabila ambazo ukiangalia sana ni ukoo atakwambia mimi aljabry yule sijui al likindi basi tabu tupu.
 
Back
Top Bottom