KERO Ucheleweshaji wa Malipo ya Refund ya SGR

KERO Ucheleweshaji wa Malipo ya Refund ya SGR

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Hello mimi ni mdau wa kutumia usafiri wa train ya kisasa sgr, Tar 2 January 2026 safari ziliahirishwa na mpaka sasa sijarudishiwa fedha ya ticket yangu ya daraja la biashara

Niliwasiliana na huduma kwa wateja wakaniambia nifike ofisi zao za Dodoma kupata utaratibu.

Niifikana na kupewa utaratibu wa kuandika barua na niache nakala ya kitambulisho nilichotumia wakati wa kukata tiketi. Nilifanya ufuatiliaji kujua imefikia wapi kupitia huduma kwa wateja na nikaambiwa niende Dodoma malipo yangu yapo tayari.

Nilifika Dodoma na kuambiwa pesa bado subiri mpaka utakapopewa taarifa kupitia simu, nikiwa Dodoma nikawapigia huduma kwa wateja kuuliza kwanini mmeniambia niende Dodoma malipo ya refund yapo tayari na huku naambiwa nisubiri hamuoni mnasababisha usumbufu kwa wateja na pesa zinachukua muda mrefu kurejeshwa kwa wateja zaidi ya miezi miwili sasa mtu nimepeleka taarifa kwa kufuata utaratibu na sijalipwa

Naomba muangazo uozo huu wa SGR
 
Back
Top Bottom