Uchaguzi 2020 Uchambuzi wangu kuelekea tamati ya kampeni kwa vyama vikuu vitatu CCM, CHADEMA na ACT Wazalendo

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
207
677
UCHAMBUZI WANGU KUELEKEA TAMATI YA KAMPENI KWA VYAMA VIKUU VITATU, CCM, CHADEMA NA ACT WAZALENDO​

Leo 20:20hrs 25/10/2020


Nimefuatilia kampeni za uchaguzi kwa wagombea wakuu Watatu,Ndugu John Pombe Magufuli,Tundu Lissu na Bernard Kamilius Membe, Japo Bernard Membe alitupa taulo ulingoni mapema kuashiria kuisha kwa pambano,Ushindani ulikuwa nani anajaza watu wengi Uwanjani,Tundu Lissu akijaza katika baadhi ya Kanda na maeneo,wakati Ndugu John Pombe Magufuli akijaza kila eneo,kila kanda,kila Mkoa,kila Wilaya hata barabarani,sababu ni kwamba Watanzania wana imani kubwa sana na Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Ndugu John Pombe Magufuli kutokana na yale yaliyofanyika,

Kwa hakika Ndugu John Pombe Magufuli atashinda uchaguzi huu kwa asilimia zaidi ya 90% kutokana na kujiunganisha na Watanzania wote wa hali ya chini,na hali ya kati na Watanzania wote wamejenga imani na Ndugu John Pombe Magufuli,Tumeona kila mgombea akijinadi kwa style yake na upekee kulingana na malengo na mikakati thabiti waliyojiwekea,
Chama tawala,Chama Cha Mapinduzi,Chama dume kigumu kutoka Madarakani,CCM kilianza kampeni kwa kishindo na kinamaliza kwa kishindo kikubwa pale dodoma baada ya kuzunguka Tanzania nzima kwa njia ya barabara,njiani kila kata,kila Wilaya,kila Mkoa,

CCM imeonesha ukubwa wa idadi ya wafuasi wake kila mahali kuanzia kwenye shina,kata,Wilaya hadi Mkoa,kwa hakika CCM ilijipanga kutetea kiti chake,kadiri siku zilivyozidi kwenda utamu wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi,chama tawala,Chama dola, ulinoga kupita kampeni zote zilizopita,hata kuliko kampeni za wapinzani wote,Msingi mkubwa ulikuwa nyomi la watu na uwezo wa kufika vijijini zaidi,tofauti na miaka yote mgombea wa CCM amefika maeneo mengi ya mijini na vijijini na kujiunganisha na kila Mtanzania kwa Utendaji wake uliotukuka na kuwekeza hasa kwa Watanzania wa hali ya chini,

Miaka yote ya uchaguzi Mkuu,Wapinzani walitambaa na kashfa za ufisadi kama ajenda yao kuu ya kuwaambia Watanzania,utakumbuka kashfa ya Loliondo Mwaka 1995 iliibua Upinzani mkubwa toka kwa Ndugu Augustino Lyatonga Mrema,Mwaka 2005 Ufisadi wa Kagoda,Meremeta, Epa uliibua Upinzani mkali toka kwa Profesa Ibrahim Haruna Lipumba,Mwaka 2010 kashfa ya Ufisadi wa Richmond, uliibua Upinzani mkali toka kwa Daktari Wilbroad Slaa,Mwaka 2015 kashfa ya Escrow iliibua Upinzani mkali toka kwa Ndugu Edward Lowassa,hizi ndio ajenda zilizokuwa zinaibua Upinzani mkali toka Upinzani kwa Miaka yote ya nyuma,

Hali ya mambo 2015 ilikuwa ngumu kwa CCM hasa baada ya Mh Edward Lowassa kukatwa CCM na kuhamia Chadema na kundi kubwa kutoka CCM jambo lilopelekea watu kupiga kura ya hasira dhidi ya CCM wakihisi Edward Lowassa alikuwa ameonewa kwa kukatwa kwake,mwaka huu ni tofauti kwani Upinzani umekosa mwanaCCM maarufu na mwenye mtandao ndani ya CCM ambaye angeweza kuyumbisha chama hata kusambaratika,Mkoa wa Kilimanjaro ulikuwa ngome kubwa ya Wapinzani,Ila wiki hii ya mwisho ya kampeni,Wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro wameamua kuonesha wazi kuachana na siasa za kiuwanaharakati baada ya kumpokea Ndugu John Pombe Magufuli kwa mafuriko makubwa ya mahaba,

Wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro walimpokea Ndugu John Pombe Magufuli kwa nderemo na vifijo wakisema wapinzani na siasa zao za kiuwanaharakati haziwasaidii na badala yake zimepunguza fursa za kimaendeleo katika Mkoa wa Kilimanjaro,ishara ya umati wa watu kuinua majani ya masale kuanzia njia panda ya Himo,Mwanga,Moshi,Hai,Usa,Arusha jiji ni ishara ya kuiunga mkono CCM na Mgombea wake John Pombe Magufuli ambae ameonesha Utendaji kazi uliotukuka,

Safari hii mambo yamekuwa magumu kwa Chadema,Act Wazalendo na wapinzani wote kwa kuwa ajenda yao kuu ya Ufisadi,imefanyiwa kazi balabala na Rais John Pombe Magufuli,na sasa hakuna Ufisadi tena,hivyo kuwawia vigumu wapinzani kuendesha kampeni zao kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu 2020,Rais John Pombe Magufuli alichukua ajenda zao zote na kuzifanyia kazi,tumpe Miaka mitano tena ndugu John Pombe Magufuli ili aweze kwenda kukamilisha kuifanya Tanzania kuwa Taifa kubwa,

Uchaguzi wa Mwaka huu 2020 Ndugu Tundu Lissu Mgombea wa Upinzani kupitia Chadema,hakuwa na hoja tena ya Ufisadi,Ndugu Tundu Lissu amekuwa akihutubia Mambo yake binafsi kwenye kampeni akipigia debe ushoga,anasema "Nina damu ya Kenya na Ubeligiji,Mimi ndie mgombea wa uraisi ninaeongoza kua na kesi nyingi mahakamani na hivyo nimeweka rekodi,Tutaandamana Nchi nzima,Mwaka huu sitamuachia Mungu,corona ipo kwa sababu Wakenya wanakaa ndani ya nyumba zao,Kiukweli ni wazi Chadema haikujipanga vizuri kuanzia namna ya kuelezea sera na ilani ya chama mpaka mapokezi waliyokuwa wakiyapata katika kampeni zao,muda mwingi Mgombea wa Chadema amekuwa,akilalamika,anatumia muda mwingi kuelezea vitu ambavyo havina maana,mfano wahuni anaowahutubia wakipiga kelele anakatisha hotuba anaanza kuwaeleza jinsi dunia inavyojua yeye kuitukana Tanzania,

Tundu Lissu amekuwa akielezea Tanzania itafungiwa misaada na na wazungu,Ndugu Tundu Lissu bado anawaza kutegemea wazungu tu,mpaka mwisho wa kufunga kampeni haikujulikana sera na ilani zao zilikuwa ni zipi baada ya Ndugu Tundu Lissu kutumia muda mwingi katika kampeni kumwaga lawama kwa Serikali, kulialia jukwaani kwa fouls walizofanyiwa wabunge, kufukuza media, kutafuta sympathy kwa kuonesha makovu yake akivua suruali na kuonyesha mguu,Ndugu Tundu Lissu ameshindwa kabisa kutuliza hisia zake binafsi,amekuwa kama mgeni katika taifa lake akielezea kufanya vitu ambavyo tayari Rais John Pombe Magufuli ameshavifanya,mfano kuondoa kodi za mizigo ya Wakulima barabarani,

Ukiangalia upande wa CCM na Mgombea wake Ndugu John Pombe Magufuli ni wazi alikuwa amejipanga vyema sana,Ndugu John Pombe Magufuli amekuwa akipanda jukwaani na kwenda moja kwa moja kwenye kueleza mengi yaliyofanywa na Serikali yake,ujenzi wa vituo takribani 450 vya Afya, miundo mbinu ya barabara akiboresha na kujenga nyingine za njia nane,akielezea alivyojenga reli ya Umeme itayopunguza masaa ya safari Dar-Morogoro saa moja,Dar -Dodoma masaa mawili,Dar-Tabora masaa matatu,Dar -Mwanza masaa sita,

Katika anga akielezea ununuzi wa rada kubwa tano,kumbuka Miaka ya nyuma tulinunua rada moja tu ikatuletea mzozo wa Ufisadi mkubwa hadi waingereza kuamua kurudisha pesa,Ununuzi wa ndege kubwa kumi,Boeing,Airbus na Bomberdier,nidhamu makazini, namna nzuri ya kudhibiti public panic katika janga la corona tofauti na Chadema waliokuwa wanataka tujifungie ndani tufe na njaa,

Ndugu John Pombe Magufuli amekuwa akieleza alivyoweka mifumo mizuri ya ukusanyaji kodi na kuwa msimamizi mzuri wa kodi za wananchi, kupungua kwa gharama za nishati ya umeme, kudhibiti ufisadi na matumizi mabovu ya kodi zetu na mengine mengi,na pia akimaliza hayo amekuwa akielezea nini atakifanya kwa miaka mingine mitano,kwa ufupi CCM walikuwa na mtiririko mzuri ulioleta ladha katika presentations zao za majukwaani kuanzia mwanzo wa kampeni hadi mwisho,

Nimalizie kwa kusifu mpangilio wa CCM katika kampeni zake zilizokonga nyoyo za watanzania toka mwanzo hadi mwisho,nitumie pia fursa hii kupongeza chaguo la CCM la kutuletea kiongozi Mzalendo na Jasiri wa kueleza wazi kile ambacho anakusudia kufanya kama Rais lilopelekea taifa katika Uchumi wa juu,NduguJohn Pombe Magufuli ndiye mwenye kuongelea hatma ya kizazi cha Watanzania leo,kesho na kesho kutwa,kwa hakika Ndugu John Pombe Magufuli is the right presidential candidate who doesn't talk about personalities, but talks about the future generations of our beloved country Tanzania and for sure I can tell, has all the qualities of a good leader that we,Tanzanians supposed to have,

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master of Leadership and Management.

Recent Publications;
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Watanzania tunaenda na Rais Magufuli
Mzalendo
Mpenda watu
Jasiri
Mtekelezaji
Mchapakazi
Mvumilivu
Mnyenyekevu

Rais Magufuli ni zawadi kwa Watanzania
 
Naona mnaandika ma bandiko marefu marefu zikiwa zimebakia siku 2 hazitawasaidia. Mlikuwa na miaka 5 kuwa convince watanzania lakini mmeshindwa. Safari hii hata vijijini wana hali ngumu na wanajua CCM imeshindwa kuwasaidia. Kutoka Mbeya hadi Kilimanjaro , Pemba hadi Kigoma kote hawaitaki CCM ya Magufuli!
 
Back
Top Bottom