GE2025 Uchaguzi wa Ubunge Fuoni na Udiwani Chamwino, Mbagala Kuu utafanyika Desemba 30, 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
354
Reaction score
395
Uchaguzi wa Ubunge katika Jimbo la Fuoni, Zanzibar na Udiwani katika Kata ya Chamwino mkoani Morogoro na Kata ya Mbagala Kuu mkoani Dar es Salaam utafanyika siku ya Jumanne Desemba 30, 2025.

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imetangaza kufanyika kwa uchaguzi wa Ubunge katika Jimbo la Fuoni kwa tarehe hiyo kufuatia kifo cha Abass Ali Mwinyi, aliyekuwa mgombea wa Ubunge Jimbo la Fuoni Wilaya ya Magharibi B, Zanzibar, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichotokea Septemba 25, 2025.

Kwa udiwani ni kufuatia kifo cha Hassani Salum Hassani, aliyekuwa mgombea wa Udiwani katika Kata ya Chamwino, Jimbo la Morogoro Mjini kupitia Chama cha Wananchi (CUF) kilichotokea Septemba 27, 2025 na kifo cha Rajabu Sultan Mwanga, aliyekuwa mgombea Udiwani Kata ya Mbagala Kuu, Jimbo la Mbagala, Dar es Salaam kupitia Chama cha Wananchi (CUF) kilichotokea Septemba 27, 2025.

Soma Pia: INEC yaahirisha uchaguzi Fuoni, sababu ni kifo cha mgombea Abbas Mwinyi

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa INEC Ramadhani Kailima imeeleza kuwa fomu za uteuzi kwa mgombea Ubunge Jimbo la Fuoni kupitia CCM na wagombea Udiwani katika Kata ya Chamwino na Kata ya Mbagala Kuu kupitia CUF zitatolewa kuanzia Oktoba 15, 2025 hadi Oktoba 21, 2025, na uteuzi wa mgombea Ubunge Jimbo la Fuoni na wagombea Udiwani katika Kata ya Chamwino na Kata ya Mbagala Kuu utafanyika Oktoba 21,2025.

Kampeni za uchaguzi wa Ubunge Jimbo la Fuoni zitafanyika kuanzia Oktoba 22, 2025 hadi Oktoba 27, 2025, na Oktoba 28,2025 hadi Novemba 4, 2025 zitasitishwa ili kupisha upigaji kura ya mapema kwa upande wa Zanzibar na siku ya kupiga kura hadi kutangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 29,2025.

Novemba 5, 2025 hadi Desemba 29,2025 kampeni zitaendelea

1759500771682.png

1759500782177.png

1759500792417.png
 
..kumbe uchaguzi unaweza kuahirishwa?

..sasa waliokuwa wanasema Reforms haziwezekani kwasababu haiwezekani kuahirisha uchaguzi wana kauli gani baada ya haya yaliyotokea?
 
Back
Top Bottom