Uchaguzi wa TLS waachiwe mawakili

nyamakonge

JF-Expert Member
May 28, 2013
363
131
Wakuu heshima kwenu.
jumuiya ya wanasheria nchini inatarajiwa kufanya uchaguzi baadae mwezi huu kupata viongozi mbalimbali watakao ongoza jumuiya hiyo kwa muda husika kikatiba.

Tofauti na chaguzi zingine zilizopita za jumuiya hii( TLS) ,uchaguzi huu umeonekana kuingiliwa na watu ata ambao sio wanasheria/mawakili.

Kuingiliwa kwa uchaguzi kunatokana na aina ya wagombea wa nafasi ya urais wa jumuiya hii.
Mvutano mkubwa unatokana na sababu ya kiitikadi za kisiasa kwa wagombea wa nafasi hiyo.

Hali hii imepelekea watu tofauti na wanasiasa kuanza kufanya kampeni kila kundi likimnadi mtu wa itikadi yao.

Tls ni jumuiya ya mawakili/wanasheria hivyo wao wahusika ndio wanajua nani anafaa kuwaongoza kulingana na malengo yao na mipango yao.

Hivyo nawasihi watu wengine ambao sio wanasheria /wamawakili wasiingilie uchaguzi huu kwa sababu ya mapenzi yao binafsi.

Tukianza kuchagua watu kwenye hizi proffesional association kwa kubase kwenye itikadi ya kisiasa na influence nyingine tutaharibu vyama hivi na kuvifanya ni sub branch za vyama vya siasa.

Tutafanya hivi kwa TLS tutaenda kwa MAT tukishinikiza rais wa Mat awe ni daktari mwenye mlengo flani wa kisiasa,tutaenda kwa maengineer,walimu na vyama vingine vya kitaaluma.

Nawasihi wanasheria /mawakili wafanye uchaguzi sahihi bila kuongozwa na mambo mengine yatokayo nje ya utaalamu wao wa kisheria.

Mungu ibariki Tanzania.Ahsanteni
 
Back
Top Bottom