Yericko Nyerere
JF-Expert Member
- Dec 22, 2010
- 17,005
- 20,423
Wakati naamua kuandika kitabu cha Ujasusi wa Kidola na Kiuchumi nilikuwa na lengo kuu moja tu, nalo ni kuhimiza Tanzania kuhama hapa ilipo na kwenda kwenye nchi ya uchumi wa viwanda amboko msingi wake ni Ujasusi wa Kiuchumi.
Dunia ya leo ni ya Ujasusi wa Kiuchumi, mshindani wetu kiuchumi awali alikuwa ni Kenya, nchi hii iliamka na kuwekeza kwenye misheni za kiupelelezi wa kiuchumi sio kisiasa, Leo mshindani ameongezeka Rwanda, taifa dogo lenye watu wasiozidi milioni 20 ndio mshindani na kiongozi wa ujasusi wa kiuchumi leo, Kila wakifanyacho leo Rwanda wanazingatia maslahi ya kiuchumi kwa nchi yao kwanza tofauti na Tanzania ambayo maslahi ya Chamwino ni muhumu kuliko ya Taifa.
Kisayansi na kinadharia uwakilishi wa EALA unahitaji vitu vitatu muhimu, Kwanza ni Sheria, yani taifa likipata uwakilishi wa mtu anayejua sheria ataweza kulipigania taifa lake kuzishinda za kisheria,
Pili ni Uchumi, yani Taifa likipata mwakilishi anayefahamu vema na aliyebobea katika uchumi, mtu huyo ataweza kutetea maslahi ya taifa lake dhidi ya hila za kiuchumi,
Na tatu ni diplomasia, hapa inahitajika mbobevu anayeweza kuhudumu katika diplomasia ya kisiasa, kiuchumi nk, huyu kwa namna yoyote atakuwa kiungo wa hao hapo juu niliowaeleza.
Leo Rwanda imechagua wawakilishi wao makini akiwemo Mwanadheria wao Mkuu kuwa mbunge wa Bunge la Mashariki, Sisi kwetu chama kwanza cha Mapinduzi ndicho kimeatamia mchakato wote na kuchagua makada wasio na vigezo vya kileo kuwa wawakilishi,Kibaya zaidi kwa uwingi wao Bungeni, wamezuia wabunge wa Chadema ambao kimsingi ndio wenye vigeo mujarabu vya kisasa kuwa wawakilishi.
Kikanuni nafasi mbili (2) katika wawakili 9, ni za chadema, hili halihitaji mjadala, Chadema baada ya mchakato halali na halisi wakuchuja wagombea wake wote walioomba kupitia Chama, Waliamua kupitisha majina mawili tu ambayo yangethibitishwa tu na bunge, Kinyume chake Wabunge wa CCM wameyakataa kwa kura, kimandiki hakukuwa na sababu za kupiga kura bali kupita bila kupingwa ikiwa nafasi zinazotakiwa ni mbili na wagombea walioletwa ni wawili.
Kiuhalisia hoja yakuwa Idadi ya Wagombea, walioiwakilisha CHADEMA Katika Uchaguzi wa EALA, Jana ndio msingi wa matokeo ya jana ni yakupuuzwa na wanaoisimamia wapuuzwe.
Kimsingi kila nafasi inapaswa kuwa na Wagombea wasiozidi watatu, ila wakiwa pungufu hakuna tatizo lolote la kikanuni au kisheria. Pia hoja ya Jinsia ya 1/3 inasimama katika wajumbe 9 waliochaguliwa tayari na Wabunge ambao kimantiki watatoka kwenye wajumbe 6 wanatoka ccm.
Picha ya hapa chini ni mbunge aliyepitishwa na ccm binti Fancy Nkuhi, huyu ndie atakwenda kupambana na majasusi ya uchumi toka Rwanda, Kenya, Uganda, Burundi, na S.Sudani
Yani ccm inataka kuwachagulia vyama vya upinzani wabunge wawatakao wao. Hili ni jambo la ajabu sana... Ajabu kuna wanaoamini kuwa Taifa litapata mageuzi ya kiuchumi kwa aina hii ya siasa za ccm. Hili ni ndoto, Taifa linahitaji MAPINDUZI ya kiuchumi sio mageuzi.
Na Yericko Nyerere