Ndugu mtoa mada jambo la muhimu ni kuwahamasisha wananchi wawe tayari kupambana katika kuilinda kura ,kwa maana sio Slaa wala Lipumba ataweza kulifanya hilo ,hilo ni jukumu la kila mpiga kura kuwa matokeo ya kura yanakuwa ni ya halali na kama kura zilivyopigwa ndivyo zinavyotangazwa.
Pemba walifanikiwa kuing'oa CCM kwa kuwa walikubali kuwa jukumu la kulinda kura sio la Chama wala mugombea ni jukumu la kila mwananchi au kila mwananchama ,na mchakato huu unaanza wakati wa uandikishaji na pia wakati wa kuhakiki daftari au majina ya wapiga kura wa sehemu husika idadi iwe inajulikana kabla ya siku ya upigaji kura,pia mawakala wa vyama ambao wapo ndani ya kituo cha upigaji kura hawa hawatakiwi kutokatoka au kuondoka kwa pamoja na ikiwa chama kina wakala shupavu basi akianzisha vurumai humo ndani ya chumba mlioko nje mtasikia kuwa ndani mambo si shwari ,wakala asienunulika ,hawa kule Pemba walifanikiwa na hawakwenda hata kukojoa ,walishinda humo na kukagua kila kitu kadiri ya sheria inavyomruhusu na walihakikisha wanapata majina yote au takwimu zote za wapiga kura katika kituo na mwisho walihakikisha kura zinahesabiwa kiuhakika kabisa ,kila aliechaguliwa basi kura yake anawekewa na mwisho zinahesabiwa na kisha kulinganishwa idadi ya kura zote zilizohesabiwa na idadi ya waliopiga kura katika kituo hicho. Ila huko Tanganyika mawakala wengi wananunulika na siku ya siku wengine hawaonekani ,utasikia wamepotea katika mazingira ya kutatanisha au hawakufika.Hapo ujue keshakatiwa chake na anatakiwa asihudhurie ajifiche kabisa asionekane kwa masiku.