Uchafuzi wa hewa Mwenge

Gibeath-Elohimu

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2014
Posts
489
Reaction score
700
Habari wanajamvi watu makini Kabisa.Natumai sote tuko poa.

Naomba kuwasilisha kero hii Kwa NEMC sijui ni mimi pekeyangu ndo napua kali ama vipi.

Kwa siku kadhaa na tuseme Kwa miezi hata mwaka hapa maeneo ya Mwenge kuanzia ITV,stendi mpya,njia yote mpaka huu upande wa petrol station ya ORYX kuna haka kaarufu Ka Kali sana hasa mida ya jioni.Nimekuwa nikijiuliza ni Ka harafu Kwa kutokwa wapi?,kiwandani au?,maana Kwa hakika haka kaarufu kametapakaa eneo kubwa Sana la Mwenge na napata mashaka na wasiwasi kama ni harufu salama.Maana ukali wake unaviashiria vyote vya kuwa na madhara kiafya.Ukizingatia eneo la Mwenge kuna raia wengi na huenda hata wanavuta hii harufu bila hata kutambua chanzo chake.

Naomba kuwasilisha hili kama kero na niiombe mamlaka husikanya NEMC kufanya utafiti wa chanzo na madhara ya harufu hii.Hakika inakera na nadhani si salama Kwa afya na mustakabali wa eneo zima la Mwenge.

Naomba kuwasilisha na kuruhusu nyongeza ya taarifa kutoka Kwa mwingine yoyote Yule ambaye Kwa namna moja ama nyingi amepata kukutana na kadhia hii ya haka kaharufu hapa mitaa ya Mwenge.

Ahsanteni.
 
Huu mtandao umefungiwa hawawezi kusoma na kutatua kero zako Chief, kapost Instagram
 
Huu mtandao umefungiwa hawawezi kusoma na kutatua kero zako Chief, kapost Instagram
Naelewa kuwa umefungiwa Ila naamini ujumbe utawafikia kama ulivyokufikia wewe.Pia sina account Instagram.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…