Ubalozi wa Norway watoa bilioni 10.6 kuwasaidia wakimbizi mkoani Kigoma

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,512
IMG_2017.jpg


Kwa kutambua hali ya kimaisha ambayo inawakabili wakimbizi waliopo mkoani Kigoma, ubalozi wa Norway nchini umesaini mkataba wenye thamani ya dola milioni 4.8 (Tsh. Bilioni 10.6) na Umoja wa Mataifa (UN) kupitia Mpango wa Misaada ya Maendeleo (UNDAP 2) kwa ajili ya kuwasaidia wakimbizi waliopo nchini.

Akizungumza katika hafla ya utiliaji saini mkataba huo, Balozi wa Norway ncini, Hanne-Marie Kaarstad alisema pesa ambazo wamezitoa zinalenga zaidi kuwasaidia wakimbizi waliopo Kigoma ili waweze kuwa na shughuli za kuwasaidia na hasa kwa wanawake na watoto.

“Kwetu ni jambo muhimu kushirikiana na UN kwa ajili ya kuwalinda watu ambao wanaingia nchini kutoka nchi jirani, tulichangia katika mpango wa kwanza wa misaada ya maendeleo na sasa tumejiunga katika mpango mwingine wa maendeleo wa 2016-2021,

“Tunafahamu Kigoma mwaka jana mwezi Mei ilipokea wakimbizi wengi kutoka Burundi na sasa tunaona ni vyema tukishirikiana na mashirika ya UN ili kuwasaidia na zaidi kwa wanawake na watoto na wote tunatambua kuwa wanawake ndiyo chanzo kikuu cha uchumi na hili sio Kigoma tu, maeneo yote ipo hivyo,” alisema Kaarstad.

Nae Mratibu Mkuu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN), Alvaro Rodriguez alisema ni jambo zuri kuona Norway inaendeleza ushirikiano na Tanzania na wao wamejipanga kuhakikisha wakimbizi wanaokusudiwa kunufaika na pesa hizo zinawafikia na kufanya kazi ambayo zimepangiwa kufanyika.

“Tunajivunia ushirikiano imara wa UN na Norway kwa kuwa tayari kusaidia watoto na wanawake , Norway imekuwa ikisaidia Tanzania na leo ni heshima kuona wakisaidia kwa mara nyingine,

“Sehemu ambazo zinakuwa na wakimbizi zina changamoto zake na hata kwa nchi kunapokuwa na wakimbizi kunashughuli za kijamii zinakuwa zinasimama, sisi kama UN tutashirikiana na serikali kufanya ambacho mnakilenga na kufikia malengo yaliyowekwa hadi 2021,” alisema Rodriguez.

Aidha alisema msaada ambao umetolewa na ubalozi wa Norway utatekelezwa sambamba na malengo ya dunia ambayo ni pamoja na kumaliza umaskini, usawa wa kijinsia na uhifadhi wa mazingira.

Chanzo:
Dewji Blog
 
Nilitaka niseme hii ni "misaada isiyo na tija tu" kama alivyosema Dambisa Moyo kwenye kitabu chake"Dead Aid" lakini nikafikiria UNHCR wanavyosaidia refugees.... hao wakimbizi wanavyopata shida hizo chapaa zinasaidia sana japo zinaibiwa vilevile. Billion kumi si haba hapo medical facilities zinaweza nunuliwa, chakula, tents kwaajili ya makazi, kupata chanjo kwa watoto wanaozaliwa kambini na mambo mengine mob. Kwa upande mwingine wasisahau kumulika chanzo cha tatizo........viongozi ving'ang'anizi ndiyo chanzo cha haya matatizo ya wakimbizi......Viongozi Africa acheni UBINAFSI hakuna atakaye toka salama wote tutakufa tu kwenye hii journey we call life. Shenziiiiiiiiii kabisa!
 
Back
Top Bottom