Ubalozi London 2013/14 ulitumia Tshs bilioni 4.2 badala ya bilioni 2 zilizotengwa

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
15,500
22,349
Kamati ya mahesabu ya bunge imeitaka Wizara ya Mambo ya nje Kikanda na Kimataifa kuwasilisha taarifa ndani ya siku nne zijazo ya matumizi ya kiasi cha shilingi bilioni 4.2 katika Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza.

Mwenyekiti wa kamati hio Mbunge Hillary Aeshi amesema taarifa hiyo ya uchambuzi wa mahesabu hayo ya mwaka wa fedha wa 2013/14 wameipitia na kuona matumizi hayo ambayo si ya kawaida na kuitaka wizara kuwasilisha taarifa yake wiki hii kwa ofisi ya msajili wa bunge.

Katika mkutano wake na wizara hio, kamati hio ya bunge pia iliitaka wizara hio kuwarudisha nyumbani maofisa wote ambao wamestaafu.

Hatua hio inatokana na kugundulika kuwa kuna baadhi ya maofisa wa Ubalozi ambao wamekwishastaafu lakini wanaendelea kupokea mishahara kutoka serikalini ambayo imekuwa ikilipwa kwa fedha kigeni.

Baadhi ya maofisa wa ubalozi wamekuwa wakitoa sababu mbalimbali za kifamilia zinazowafanya kuendelea kuishi huko ughaibuni zikiwemo za kuwasubiri watoto wao wamalize shule.

Nae katibu mkuu wa kudumu wa wizara hio Dr Aziz Mlima amekiri kupokea maagizo ya kamati hio ya bunge na kueleza kuwa taarifa itakuwa tayari ndani ya wiki hii kuhusiana na machanganuo wa matumizi ya Ubalozi wa Tanzania Uingereza.

Chanzo: Gazeti la The Citizen.

My Take:

Hii ishaanza kuleta matatizo mahali fulani.

Friday, April 1, 2016
Ministry in hot water over Sh4.6bn spent on London mission

In Summary

The committee was reviewing the ministry’s audited report for the year 2013/2014 and asked the ministry to submit a detailed report within four days.

By Henry Mwangonde @henrymwangonde4 hmwangonde@tz.nationmedia.com

Dar es Salaam.

The parliamentary Public Accounts Committee on Thursday has asked the ministry of Foreign Affairs, East Africa, Regional and International Cooperation to explain how the Tanzania High Commission in London spent Sh4.6 billion when it was only allocated Sh2.0 billion.

The committee was reviewing the ministry’s audited report for the year 2013/2014 and asked the ministry to submit a detailed report within four days.

“We want the ministry to submit the report to the parliamentary clerk next week so that we understand what is really going on,” said the committee’s chairman Mr Hilary Aeshi.

At the same meeting the committee directed the ministry to ensure that all retired officers still attached to missions abroad return home.

It emerged that there are various embassy personnel who, although they have reached the age of retirement are still being paid by the government.

The officials claim they are waiting for their offspring to complete the studies they have already embarked on outside the country.

The ministry’s Permanent Secretary, Dr Aziz Mlima said the retired embassy officials cite family related matters as reasons for extending their stay abroad.

He told the committee, “We will submit the report in time to the clerk in line with your instructions.”
 
Hivi maafisa wa balozi karibia asilimia 80 si huwa wanakuwaga majasusi wa nchi wanazoziwakilisha.? Hapa TISS na wizara ya mambo ya nje wana ya kujibu.
 
Hivi maafisa wa balozi karibia asilimia 80 si huwa wanakuwaga majasusi wa nchi wanazoziwakilisha.? Hapa TISS na wizara ya mambo ya nje wana ya kujibu.

Sasa mkuu, ujasusi wa kumtafuta nani tena?

Tusubiri watakuja na majibu.

Ila sidhani kama siku nne zinatosha kupata taarifa nzima.

Ndio maana wakati mwingine utaona kwamba haya mambo ni magumu sana.
 
My Take:

Hii ishaanza kuleta matatizo mahali fulani.

Really? Is this all you can muster as far as your opinion regarding the veracity of these accusations? Why bother bringing this up if all you got to say can be surmised in 6 (six) words?
 
Sasa mkuu, ujasusi wa kumtafuta nani tena?

Tusubiri watakuja na majibu.

Ila sidhani kama siku nne zinatosha kupata taarifa nzima.

Ndio maana wakati mwingine utaona kwamba haya mambo ni magumu sana.
Mkuu,

Taarifa wazotaka 2013/14 katika utawala bora lazima zimeshaifadhiwa kimaandishi. Ni ku-copy and paste.

Kama ndio wanazitafuta sasa hivi wapishe watu wengine waje kuzitafuta.
 
image-jpeg.327101

Msafiri Marwa Kaimu Balozi-Uingereza ni jipu lililotukuka
 
Wakuu, mnaweza kundelea kuchangia hii mada lakini msiihusishe kabisa na mambo mengine kama yanavyoletwa.

Richard ni mmoja wa watu waliochoshwa na tabia za Ubalozi wetu London za uswahili-uswahili.

Pia Richard hajawahi kufanya kazi ubalozini.

Richard ni mhangaikaji na mtafutaji maisha tu ya ujasirimali ughaibuni lakini ameishi pia UK na nchi zingine za Ulaya.

Lakini lengo kuu la mada hii ni matumizi ya mwaka 2013/14 ambapo fedha za walipa kodi kutoka Tanzania zimetumiwa vibaya.

Napenda kurudia kwamba mada hii haikusiki kwa namna yoyote ile habari zingine za majungu.
 
Habari gani za majungu mkuu?? au hizi za Ujasusi??
hizi ni za kawaida hakuna nchi isiyojua kuwa mabalozi wa nchi nyingine ndani ya nchi zao ni majasusi
 
Habari gani za majungu mkuu?? au hizi za Ujasusi??
hizi ni za kawaida hakuna nchi isiyojua kuwa mabalozi wa nchi nyingine ndani ya nchi zao ni majasusi

Hapana, imebidi niweke angalizo baada ya kuona mmoja wetu ameunganisha na uzi mwingine wa mpumbavu mmoja anaitwa Bi Sent 50.

Naona huyo Bi Senti 50 kapigwa sindano tayari (online injection) kabla hajatumbuliwa majibu sasa hivi anaweweseka.
 
Another movie comin. Inakuaje wizara husika inaruhusu ofisi zake za ubalozi kufanya matumizi zaidi ya kiasi ilicho idhinishiwa? Kweli hii ndio Tanzania Zaidi ya Uijuavyo
 
Another movie comin. Inakuaje wizara husika inaruhusu ofisi zake za ubalozi kufanya matumizi zaidi ya kiasi ilicho idhinishiwa? Kweli hii ndio Tanzania Zaidi ya Uijuavyo
Hivi Mkwerre alifanya ziara ngapi kipindi hicho ndani ya Uingereza.??

Isije kuwa pesa nyingi alitafuna yeye
 
Hivi maafisa wa balozi karibia asilimia 80 si huwa wanakuwaga majasusi wa nchi wanazoziwakilisha.? Hapa TISS na wizara ya mambo ya nje wana ya kujibu.
Balozi ndiyo anaidhinisha matumizi. JPM alipoanza kwa kuwapangua mabalozi wengine waliguna hapa.
 
Hakuna ujasusi wowote unahitajika.

Ni Mtu kuangalia invoice in vs reality basi.

Mfano: mtumishi ame claim how much kwenye shopping cost ya kurudi nyumbani vs Market price ya wakati huo.

Mbona Easy tu.

Rent zao za Nyumba za Hendon Zipitiwe upya.
 
Wakuu, mnaweza kundelea kuchangia hii mada lakini msiihusishe kabisa na mambo mengine kama yanavyoletwa.

Richard ni mmoja wa watu waliochoshwa na tabia za Ubalozi wetu London za uswahili-uswahili.

Pia Richard hajawahi kufanya kazi ubalozini.

Richard ni mhangaikaji na mtafutaji maisha tu ya ujasirimali ughaibuni lakini ameishi pia UK na nchi zingine za Ulaya.

Lakini lengo kuu la mada hii ni matumizi ya mwaka 2013/14 ambapo fedha za walipa kodi kutoka Tanzania zimetumiwa vibaya.

Napenda kurudia kwamba mada hii haikusiki kwa namna yoyote ile habari zingine za majungu.
Mkuu kuna sehemu wamesema pesa zimetumiwa vibaya au ni kutumia zaidi ya budget?
 
Another movie comin. Inakuaje wizara husika inaruhusu ofisi zake za ubalozi kufanya matumizi zaidi ya kiasi ilicho idhinishiwa? Kweli hii ndio Tanzania Zaidi ya Uijuavyo

Watu wanafanya kitu kinaitwa "bypass all procedures" katika kuidhinisha matumizi, lakini nadhani ni chanzo cha tatizo (Dar)ndio kitabanwa na baadae London.
 
Mkuu kuna sehemu wamesema pesa zimetumiwa vibaya au ni kutumia zaidi ya budget?

Mkuu, bajeti ya matumizi kwa Ubalozi London ilitengwa 2.0 bilioni lakini zikatumika 4.2bilioni.
 
Hakuna ujasusi wowote unahitajika.

Ni Mtu kuangalia invoice in vs reality basi.

Mfano: mtumishi ame claim how much kwenye shopping cost ya kurudi nyumbani vs Market price ya wakati huo.

Mbona Easy tu.

Rent zao za Nyumba za Hendon Zipitiwe upya.

Hivi ni Hendon au Highgate?

Kama bado ni hio latter basi rent itakuwa kubwa si unafahamu eneo lenyewe ni la matajiri?
 
Kama Rent ni too much kuna Ulazima wowote wa wao kukaa eneo lile ambao Rent ziko juu??

Some of them wake/waume zao wanafanya kazi nyingine kwenye makampuni mengine, je kwa sababu wako kwenye full time employment hawatakiwi ku changia kwenye kodi za pango Na living expenses??

Yapo mengi Ila ndio hivyo WANAOSIKIA HAWAELEWI NA WANAOELEWA HAWASIKII

Ova to you Richard
 
Back
Top Bottom