Bernadetta
Member
- Mar 24, 2013
- 7
- 3
Naomba maoni yenu kuhusu hii hoja. Hivi ni kwanini ubakaji nchini unaonekana kama jambo la aibu kwa mtendewaji? Na kwanini jamii baada ya kuwasaidia hawa waliobakwa wengi hukaa chini na kuwasengenya na kuwaongelea waliobakwa kama vile ni habari za kunywea chai vijiweni? Je jamii yenu imekuwa haina moyo wa utu na huruma kwa hawa waliobakwa au ni kutokuwa na ufahamu wa madhara ya ubakwaji kisakologia? Ni mara nyingi nasikia na kusoma kwenye blogs watu wanasema 'duh huyu demu alibakwa bwana' au 'mtoto wa yule mama kaharibiwa maskini'...nabaki najiuliza jamani hizi ni habari za kutangaza kwa jamii kama gossips au inatakiwa ujiulize nitamsaidiaje huyu binadamu mwenzangu. Nilifurahi sana ile issue ya ubakwaji wa yule mwanafunzi wa chuo wa India ilivyochukuliwa na jamii ile. Watu waliandamana, vyombo vya habari vilipiga kelele mpaka serikali ilichukuwa hatua. Je ni watu wangapi na watoto wa Tanzania wanabakwa kila siku? Je serikali na wewe kama mtanzania unafanya nini? Tusifungie macho jambo hili hata kidoogo :nono: kwani hao wanaobakwa ni mama zetu, dada zetu, marafiki zetu, watoto zetu...usingoje mpaka janga hii lifike kwenye familia yako ndipo uchukue hatua. Usiwe mmoja wa tatizo kwa kugossip tu na kucheka yaliowakumba (eee haeli kabakwa alikuwa anaringa sana huyo) kuwa mmoja wa suluhisho.