Ubaguzi wa Jaguar,siasa chafu na hatari kwa umoja wa Afrika ya mashariki

Idd Ninga

Idd Ninga

Verified Member
Joined
Nov 18, 2012
Messages
2,669
Points
2,000
Idd Ninga

Idd Ninga

Verified Member
Joined Nov 18, 2012
2,669 2,000
OSHA DOMO LAKO.

Wazi wewe mbaguzi,hata uso na maana
Hakika we mlanguzi,leo wazi nakuchana
Haujapita makuzi,natamani kutukana
Jagwa osha domo lako,ushindwe na ulegee

Wafrika sote ni ndugu,tunapaswa tuungane
Siasa zako magugu,wataka tubaguane
Akili zako ni njugu,za usiku wa manene
Jagwa osha domo lako,ya hovyo umeropoka.

Maneno uloyatoa,ni wazi ya kishetani
Tena umedhamiria,na wala siyo matani
Wafrika tumesikia,tumejua wewe nani
Jagwa osha domo lako,ewe koloni jeusi.

Laiti isingekua,hu wetu mshikamano
Hasubuhi kufikia,tungekupiga sindano
Mbali ukaangukia,ukiwa hauna meno
Jagwa osha domo lako,kiri wewe mbaguzi

Rohoni una mapepo,hiyo siyo mila yenu
Bendera fata upepo,nakutumia rununu
Laani chako kiapo,laana isije kwenu
Ukinywa damu ya mtu,matumbo hutoa funza.

SHAIRI-OSHA DOMO LAKO.
MTUNZI-Idd Ninga,Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 
princemikazo

princemikazo

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2019
Messages
1,977
Points
2,000
princemikazo

princemikazo

JF-Expert Member
Joined Jan 10, 2019
1,977 2,000
Kwani chalii kazingua nini ariff??
 
stwita

stwita

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2011
Messages
1,327
Points
1,500
stwita

stwita

JF-Expert Member
Joined Feb 14, 2011
1,327 1,500
Sitasikiliza tena muziki wa Jaguar
 
Mzee_Mzima

Mzee_Mzima

Member
Joined
Jul 2, 2019
Messages
38
Points
95
Mzee_Mzima

Mzee_Mzima

Member
Joined Jul 2, 2019
38 95
OSHA DOMO LAKO.

Wazi wewe mbaguzi,hata uso na maana
Hakika we mlanguzi,leo wazi nakuchana
Haujapita makuzi,natamani kutukana
Jagwa osha domo lako,ushindwe na ulegee

Wafrika sote ni ndugu,tunapaswa tuungane
Siasa zako magugu,wataka tubaguane
Akili zako ni njugu,za usiku wa manene
Jagwa osha domo lako,ya hovyo umeropoka.

Maneno uloyatoa,ni wazi ya kishetani
Tena umedhamiria,na wala siyo matani
Wafrika tumesikia,tumejua wewe nani
Jagwa osha domo lako,ewe koloni jeusi.

Laiti isingekua,hu wetu mshikamano
Hasubuhi kufikia,tungekupiga sindano
Mbali ukaangukia,ukiwa hauna meno
Jagwa osha domo lako,kiri wewe mbaguzi

Rohoni una mapepo,hiyo siyo mila yenu
Bendera fata upepo,nakutumia rununu
Laani chako kiapo,laana isije kwenu
Ukinywa damu ya mtu,matumbo hutoa funza.

SHAIRI-OSHA DOMO LAKO.
MTUNZI-Idd Ninga,Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
Jaguar alizungua lakini kaka iweje ninyi mnaingia kenya kwa Urahisi na sisi tunasumbuliwa sana kuja Bongo kufanya biashara, mbona tujiite Afrika Mashariki hadi passport tunazotumia zimeandikwa “East African passport” na haturuhusiwi kuvuka boda vile Jaguar na Mtu Mzima AY waliimba?
 
Idd Ninga

Idd Ninga

Verified Member
Joined
Nov 18, 2012
Messages
2,669
Points
2,000
Idd Ninga

Idd Ninga

Verified Member
Joined Nov 18, 2012
2,669 2,000
Jaguar alizungua lakini kaka iweje ninyi mnaingia kenya kwa Urahisi na sisi tunasumbuliwa sana kuja Bongo kufanya biashara, mbona tujiite Afrika Mashariki hadi passport tunazotumia zimeandikwa “East African passport” na haturuhusiwi kuvuka boda vile Jaguar na Mtu Mzima AY waliimba?
Inwezekana nawe hujawahi kuja Tanzania,ninafahamu na nina marafikik wengi wa Kenya wanaofanya kazi Tanzania bila ya bughudha yeyote,na wengi na mameneja.
 

Forum statistics

Threads 1,315,675
Members 505,292
Posts 31,866,470
Top