GE2025 Uamuzi wa kesi ya Polepole dhidi ya jamhuri kutolewa leo Oktoba 24, 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Shauri namba 24514 la mwaka 2025 lililofunguliwa na aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania kwenye nchi za Malawi na Cuba Humphrey Polepole dhidi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) na wenzake, linatarajiwa kutolewa uamuzi leo, Ijumaa Oktoba 24.2025, Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam

Kesi hiyo imefunguliwa kwa hati ya 'dharura sana' na Wakili Peter Kibatala kwa niaba ya mleta maombi (Humphrey Polepole), ambapo washtakiwa (Jamhuri) wanaombwa kumleta Mahakamani au kueleza alipo Humphrey Polepole ambaye ametoweka katika mazingira tatanishi na hadi leo haijulikani alipo

Kesi hiyo inayosikilizwa chini ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam Salma Maghimbi, ilikuwa ikiendeshwa kwa njia ya maandishi ambapo Mawakili wa pande zote mbili walikuwa wakibadilishana nyaraka.

Pia Soma: Maamuzi ya kutoweka kwa Polepole kutolewa Oktoba 24, 2025

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…