Uamuzi wa busara wa Nyerere ni kuacha ualimu na kufanya siasa

shaurimbaya

JF-Expert Member
Oct 3, 2013
1,915
2,329
habari wadau.

ualimu sio ndoa ya mateso..

hii kwa walimu wote wa kiume waliopo mazingira magumu, na wanaochukia kunyanyaswa na kila mtu.. mara zamu za usafi shuleni, mara wachapwe viboko.. maneno ya mwandishi wa hii article yamenigusa ku share na walimu wote wa kiume...

Ualimu si ndoa ya mateso | Gazeti la MwanaHalisi

NADHANI alikuwa Edda Sanga, mtangazaji wa Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD sasa TBC Taifa) ambaye aliendesha kipindi cha maswali na majibu mwaka 1981 kati ya Tabora Boys na Milambo sekondari.

Lengo la shindano lile la chemshabongo lililoandaliwa na RTD lilikuwa kupambanisha wanafunzi wa shule hizo mbili ambazo Mwalimu Julius Nyerere alisoma na kufundisha.

Nyerere alisoma Shule ya Sekondari Tabora Boys na alifundisha Milambo sekondari zote za mjini Tabora.

Katika shindano lililofanyika Tabora Boys, kila shule iliandaa vijana watano mabingwa wa kufikiri haraka na kujibu au waliosoma na kuhifadhi kichwani mafundisho.

Swali likatupwa kwa Milambo, “Uamuzi bora ni nini?” Swali jepesi sana, lakini liliwagalagaza mabingwa wote 10 wa kidato cha V na VI yaani watano wa Milambo na watano wa Tabora Boys. Edda akalitupa swali hilo kwa wasikilizaji.

Kijana wa kidato cha III kutoka Milambo sekondari alisimama na kujibu kuwa uamuzi wa busara ni hatua ya Mwalimu Nyerere kuacha kazi ya kuajiriwa (ualimu) na kufanya kazi ya siasa.

Mwanafunzi yule (nimesahau jina lake) alichagua kibao “Ndoa ya mateso” cha Marijan Rajabu kwa ajili ya burudani.

Ndiyo maana mpaka leo, walimu wanaojiamini hufanya ‘uamuzi wa busara’ kuacha kazi hiyo na kutafuta kazi nyingine, ikiwezekana hujiingiza katika masuala ya siasa - “kazi” yenye malipo ya ajabu.

Wengi wamefikishwa hapo kutokana na kupuuzwa na serikali, kukatishwa tamaa na mazingira ya kazi na tamaa ya maisha bora.

Walimu wengi ambao wangekuwa wanafundisha vijana leo wamechukua ‘uamuzi wa busara’ wakagombea na kuchaguliwa kuwa madiwani na wabunge.

Walimu wengi wametupa chaki wakachukua mafunzo mengine sasa ni wahariri wakuu wa vyombo vya habari au wafanyakazi katika mashirika na makampuni.

Ndiyo maana walimu kadhaa waliopangiwa vituo vya kazi Februari mwaka huu baada ya kukumbana na mazingira yasiyo rafiki kwao wakachukua posho za kujikimu na kuondoka.

Kulikoni? Katika siku chache walizokaa vituoni wakisubiri kulipwa fedha za kujikimu, walimu wapya wamekuwa wakisikia malalamiko yasiyoisha ya wenzao kutopandishwa madaraja kwa muda mrefu, wengine tangu 2004 hivyo wanaendelea kulipwa mishahara ileile ya wakati walipoanza kazi.

Aidha, wamesikia malalamiko ya waliopandishwa vyeo au madaraja lakini wakiendelea kulipwa mishahara ya zamani.

Mbali ya kusikia malalamiko ya walimu wenzao wanaodai malimbikizo ya mishahara, posho mbalimbali; wengine hawajalipwa fedha za uhamisho. Hizi ni kero sugu kwa walimu.

Katika hotuba yake ya kwanza alipoteuliwa kuchukua mikoba ya Edward Lowassa mwaka 2008, waziri mkuu, Mizengo Pinda aliangiza mwalimu asihamishwe kama hakuna fedha za uhamisho. Agizo hilo halifanyiwi kazi.

Kwa hiyo, japokuwa walimu waliochukua posho na kuacha kazi wamefanya kosa kisheria, lakini kuna mchango mkubwa wa serikali katika kosa hilo.

Tazama, waliporipoti hawakulipwa fedha za kujikimu, wengine walilipwa baada ya mwezi na zaidi. Serikali inadhani walimu walikuwa wanakula nini, mchwa au hewa?

Baadhi walikopa wakitarajia wakilipwa posho pamoja na mshahara wataweza kurudisha mikopo. Lakini baadhi waliambulia mshahara wa msaada wa Sh. 100,000 tu wakiambiwa wasubiri kuingizwa kwenye pay-roll.

Hata mwezi uliofuata majina ya walimu hayakuingizwa. Kwanini ualimu unafanywa ndoa ya mateso? Kwanini malalamiko ya mishahara ni kwa walimu tu na si idara nyingine?

Katika kipindi ambacho serikali imetoa vitisho kwa walimu ikitaka ama warejee kazini au warejeshe posho katika mwezi mmoja ujao, itakuwa busara ikatathmini upya wajibu wake kwa walimu. Kuufanya ualimu ndoa ya mateso, uamuzi wa busara ni kuacha kazi.
 
Tatizo walimu wengi mapoyoyo,hawajitambui

kwa changamoto za ualimu.. ndio maana kina Magufuli, Kassim Majaliwa, walikimbia baada ya mwaka mmoja tu wa kufundisha..

nina imani wangekomaa na chaki 5 to 10 years wasingefika walipofika leo... wangekuwa bado wanateswa tu na wakuu wa wilaya na maafisa elimu... maporini huko...

walimu wa kiume ni mateso sana hasa ukuwa huna plan b.. maana majukumu plus manyanyaso kibao
 
kwa changamoto za ualimu.. ndio maana kina magufuli, kassim majaliwa, walikimbia baada ya mwaka mmoja tu wa kufundisha..

nina imani wangekomaa na chaki 5 to 10 years wasingefika walipofika leo... wangekuwa bado wanateswa tu na wakuu wa wilaya na maafisa elimu... maporini huko...

walimu wa kiume ni mateso sana hasa ukuwa huna plan b.. maana majukumu plus manyanyaso kibao
Majaliwa alifundisha miaka 12 ni 1988-2000
 
Alifundisha shule za msingi,ni mwalimu wa Grade A

CV yake hiyo hapo Mr Majaliwa..

Vijalizo vya Jina Mhe.
Jina la Ukoo: Majaliwa
Jina la Kwanza: Kassim
Jina la Kati: Majaliwa
Tarehe ya Kuzaliwa: 1960-12-22
Mahali Alipozaliwa:
Hali ya Ndoa: Nimeoa
Kundi: Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
Jinsia: M
Simu ya Ofisi: -
Simu ya mkononi: 785205910
Barua pepe: majaliwa.kasimu@yahoo.com
Anuani: P.O.Box 51,
Ruangwa
Elimu
Toka
Hadi Jina la Shule/Chuo Cheti
1970 1976 Mnacho Primary School cheti cha Elimu ya Msingi
1977 1980 Kigonsera Secondary School CSEE
1991 1993 Mtwara Teachers College -
1994 1998 University of Dar es Salaam Bachelor Degree
1999 1999 Storckolm University PGDP

Mafunzo Mengineyo
-
Uzoefu
Toka
Hadi Jina la Mwajiri Ngazi/Wazifa
2010 2014 - MB
2006 2010 PM Mkuu wa Wilaya
2001 2006 PS-CWJ Katibu Mkoa
2001 2001 PS-CWJ Katibu Wilaya
1988 2000 PS-Moec Mkufunzi
1981 1986 TD-Lindi Council Mwalimu
 
Kiukweli huwa nawaonea huruma saana waalimu kwa manyanyaso yao.

Hivi karibuni nilikuwa nafanya mitihani ya OUT, nikiwa kwenye exams hall ghafla namuona mwl wangu wa somo la mwandiko pembeni yangu anahenya na mtihani wake wa kozi ya education, sio siri alikuwa kachoka kiatu cha mokasini kimeisha upande, shati limepauka, amechoka nyang'anyang'a nikakaa kimya mpaka mtihani ulipokwisha nikamfuata nje nikamnunulia soda na cake then tukapiga soga nikamuuliza anapokaa then nikamrush na gari la sikutaka kumwambia mimi ni mwanafunzi wake wa mwandiko darasa la kwanza B, nilihisi nitampa stress na kumkumbusha machungu mwalimu wangu mpendwa.

Mungu watizame Waalimu maana watapata ahueni kwa neema yako tu na sio kwa ujanja wao.
 
Ualimu ni kazi nzuri ukiingia huko ukiwa na positive attitude
Na pia ualimu huohuo ni kazi mbaya ukiingia ukiwa na negative attitude.
Tumia ualimu kama fursa ya kuazisha fursa nyingine za kimaisha nakuhakikishia hutoona kama unanyanyasika lkn ukitegemea ualimu huo tu utabaki hvyo ulivyo.

Cha msingi ni sisi waalimu kubadili mindset zetu tusilaumu tu kuwa ualimu ni mateso wakati sisi wenyewe ndo tumeamua kujitesa wenyewe kwa kushindwa kufikiria fursa za maisha kupitia huo ualimu.
 
CV yake hiyo hapo Mr Majaliwa..

Vijalizo vya Jina Mhe.
Jina la Ukoo: Majaliwa
Jina la Kwanza: Kassim
Jina la Kati: Majaliwa
Tarehe ya Kuzaliwa: 1960-12-22
Mahali Alipozaliwa:
Hali ya Ndoa: Nimeoa
Kundi: Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
Jinsia: M
Simu ya Ofisi: -
Simu ya mkononi: 785205910
Barua pepe: majaliwa.kasimu@yahoo.com
Anuani: P.O.Box 51,
Ruangwa
Elimu
Toka
Hadi Jina la Shule/Chuo Cheti
1970 1976 Mnacho Primary School cheti cha Elimu ya Msingi
1977 1980 Kigonsera Secondary School CSEE
1991 1993 Mtwara Teachers College -
1994 1998 University of Dar es Salaam Bachelor Degree
1999 1999 Storckolm University PGDP

Mafunzo Mengineyo
-
Uzoefu
Toka
Hadi Jina la Mwajiri Ngazi/Wazifa
2010 2014 - MB
2006 2010 PM Mkuu wa Wilaya
2001 2006 PS-CWJ Katibu Mkoa
2001 2001 PS-CWJ Katibu Wilaya
1988 2000 PS-Moec Mkufunzi
1981 1986 TD-Lindi Council Mwalimu
Mkuu acha kupendezesha CV ya mtu kisa kwa Sasa ni waziri mkuu

Majaliwa Kala sana vumbi kule singida akiwa ni mwl wa primary miaka km mitano ivi
habari wadau.

ualimu sio ndoa ya mateso..

hii kwa walimu wote wa kiume waliopo mazingira magumu, na wanaochukia kunyanyaswa na kila mtu.. mara zamu za usafi shuleni, mara wachapwe viboko.. maneno ya mwandishi wa hii article yamenigusa ku share na walimu wote wa kiume...

Ualimu si ndoa ya mateso | Gazeti la MwanaHalisi

NADHANI alikuwa Edda Sanga, mtangazaji wa Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD sasa TBC Taifa) ambaye aliendesha kipindi cha maswali na majibu mwaka 1981 kati ya Tabora Boys na Milambo sekondari.

Lengo la shindano lile la chemshabongo lililoandaliwa na RTD lilikuwa kupambanisha wanafunzi wa shule hizo mbili ambazo Mwalimu Julius Nyerere alisoma na kufundisha.

Nyerere alisoma Shule ya Sekondari Tabora Boys na alifundisha Milambo sekondari zote za mjini Tabora.

Katika shindano lililofanyika Tabora Boys, kila shule iliandaa vijana watano mabingwa wa kufikiri haraka na kujibu au waliosoma na kuhifadhi kichwani mafundisho.

Swali likatupwa kwa Milambo, “Uamuzi bora ni nini?” Swali jepesi sana, lakini liliwagalagaza mabingwa wote 10 wa kidato cha V na VI yaani watano wa Milambo na watano wa Tabora Boys. Edda akalitupa swali hilo kwa wasikilizaji.

Kijana wa kidato cha III kutoka Milambo sekondari alisimama na kujibu kuwa uamuzi wa busara ni hatua ya Mwalimu Nyerere kuacha kazi ya kuajiriwa (ualimu) na kufanya kazi ya siasa.

Mwanafunzi yule (nimesahau jina lake) alichagua kibao “Ndoa ya mateso” cha Marijan Rajabu kwa ajili ya burudani.

Ndiyo maana mpaka leo, walimu wanaojiamini hufanya ‘uamuzi wa busara’ kuacha kazi hiyo na kutafuta kazi nyingine, ikiwezekana hujiingiza katika masuala ya siasa - “kazi” yenye malipo ya ajabu.

Wengi wamefikishwa hapo kutokana na kupuuzwa na serikali, kukatishwa tamaa na mazingira ya kazi na tamaa ya maisha bora.

Walimu wengi ambao wangekuwa wanafundisha vijana leo wamechukua ‘uamuzi wa busara’ wakagombea na kuchaguliwa kuwa madiwani na wabunge.

Walimu wengi wametupa chaki wakachukua mafunzo mengine sasa ni wahariri wakuu wa vyombo vya habari au wafanyakazi katika mashirika na makampuni.

Ndiyo maana walimu kadhaa waliopangiwa vituo vya kazi Februari mwaka huu baada ya kukumbana na mazingira yasiyo rafiki kwao wakachukua posho za kujikimu na kuondoka.

Kulikoni? Katika siku chache walizokaa vituoni wakisubiri kulipwa fedha za kujikimu, walimu wapya wamekuwa wakisikia malalamiko yasiyoisha ya wenzao kutopandishwa madaraja kwa muda mrefu, wengine tangu 2004 hivyo wanaendelea kulipwa mishahara ileile ya wakati walipoanza kazi.

Aidha, wamesikia malalamiko ya waliopandishwa vyeo au madaraja lakini wakiendelea kulipwa mishahara ya zamani.

Mbali ya kusikia malalamiko ya walimu wenzao wanaodai malimbikizo ya mishahara, posho mbalimbali; wengine hawajalipwa fedha za uhamisho. Hizi ni kero sugu kwa walimu.

Katika hotuba yake ya kwanza alipoteuliwa kuchukua mikoba ya Edward Lowassa mwaka 2008, waziri mkuu, Mizengo Pinda aliangiza mwalimu asihamishwe kama hakuna fedha za uhamisho. Agizo hilo halifanyiwi kazi.

Kwa hiyo, japokuwa walimu waliochukua posho na kuacha kazi wamefanya kosa kisheria, lakini kuna mchango mkubwa wa serikali katika kosa hilo.

Tazama, waliporipoti hawakulipwa fedha za kujikimu, wengine walilipwa baada ya mwezi na zaidi. Serikali inadhani walimu walikuwa wanakula nini, mchwa au hewa?

Baadhi walikopa wakitarajia wakilipwa posho pamoja na mshahara wataweza kurudisha mikopo. Lakini baadhi waliambulia mshahara wa msaada wa Sh. 100,000 tu wakiambiwa wasubiri kuingizwa kwenye pay-roll.

Hata mwezi uliofuata majina ya walimu hayakuingizwa. Kwanini ualimu unafanywa ndoa ya mateso? Kwanini malalamiko ya mishahara ni kwa walimu tu na si idara nyingine?

Katika kipindi ambacho serikali imetoa vitisho kwa walimu ikitaka ama warejee kazini au warejeshe posho katika mwezi mmoja ujao, itakuwa busara ikatathmini upya wajibu wake kwa walimu. Kuufanya ualimu ndoa ya mateso, uamuzi wa busara ni kuacha kazi.
 
nimeitoa kwenye tovuti ya bunge... sasa wao ni waongo au wadanganyifu.... cv ya mtu utaipendeshaje wakati safari yake ya elimu na maisha anaijua mwenyewe??

Mkuu acha kupendezesha CV ya mtu kisa kwa Sasa ni waziri mkuu

Majaliwa Kala sana vumbi kule singida akiwa ni mwl wa primary miaka km mitano ivi
 
Alifundisha shule za msingi,ni mwalimu wa Grade A
Usiwe unaongea bila data.mwalimu wa msingi grade A alikua ni mkewe alifundisha ligula primary school mtwara akitumia jina la Mwl mbawala (she was very cute those days) na majaliwa ttc mtwara. baada ya hapo sijui walihamia wapi..
 
Tuwahurumie walimu! Nikikumbuka nilipotoka hata kuumba herufi "a" sijui lakini sasa naweza kusimama kwenye hadhara ya watu wasiojua lugha ya kiswahili na kufanya muhadhara na kunikubali napaswa kuwashuru sana Walimu wangu!
 
Sidhani kama nitakuja niache ualimu labda itokee fursa ambayo nitaona itanifanya niishi maisha ya furaha zaidi ya haya. Tatizo ni kwamba walimu wengi wameingia kwa hii fani pasipo kujua wanataka nini. Kiongozi au boss yoyote atakunyanyasa kutokana na jinsi unavyojiweka ama namna yako ya kufikiri. Ukiwa smart kichwani na unajiweka vyema ma-boss wenyewe huwa wanapwaya mno mbele yako.

Walimu tujiamini.
 
Kwa nchi yetu bado elimu haijawa issue ya kupewa priority tofauti na nchi zingine ndo maana matatizo ya walimu ni mengi sana.

Ualimu sio ni mother profession ambayo kada zote uzaliwa kwayo... Kutoithamini hii fani ni kubomoaa misingi ya elimu kabisaa nchini.

Walimu wasipokua na fikra endelevu na zenye kuleta mabadiliko hakika vilio vitaendeleaa hadi mwisho wa ulimwengu huu

Kuna wimbi kubwa sana la walimu wasiozijuaa haki zao na wenye mentality ya uoga... Thanks God vyuoni ss iv wanazalishwa wahitimu ambao wanakua conscious na wenye kuzijua changamoto

Kitu ambacho ambacho serikali na wadau wa elimu twapaswa kufanya ni kuwa motivate walimu ndani na nje kabla ya chochote kile kwani mwalimu ndio dereva na aribia n wanafunzi... Ata km utampa gari luxury aendeshe lina kila kitu wakati yy ana shida kila kona usitegemee safari salama
 
viongozi walimu lakini hawajali walimu wenzao

walimu ni watu muhim sana

Back
Top Bottom