Twachezesha kiuno, akili, mchakato, kila kitu

immasoft

Senior Member
Joined
Mar 2, 2011
Posts
188
Reaction score
128
Haya basi, tukafika kwenye uwanja wetu, tayari kwa uburuzaji. Na sikatai, kidogo tulitingishika mlipotoka, tukafikiri kwamba labda mna mikakati murua ya kuwaamsha watu, kumbe yaleyale tu, yaleyale. Kutishia maandamano kisha kukaa kimya. Mmmh, kweli mmenifurahisha sana.

Halafu kung'ang'ania tu, kung'ang'ania tu rasimu ya sumu jinsi ilivyo mmetupatia nafasi nyingi bora kabisa. Kwani wale walikuwa miungu? Lazima walisahau mambo mengine, na kubwa kabisa hawakuandika katiba ya nchi isiyo na jina hivyo tumeweza kuahidi kila kitu kwa kila mtu ili kuficha jinsi tulivyoondoa yale ambayo yalitubana, pamoja na suala zito lenyewe la mahusiano ya ndoa.

Ndiyo, wasanii wamelalamika, wape, na wanawake, kabisa wape maana wapiga kura wengi ni wanawake, hata vijana wakorofi, wape, wakulima, wape. Mimi nilikuwa tayari kuwapa hata watoto wa shule za msingi iandikwe kwenye katiba kwamba ni marufuku kuwachapa viboko lakini wenzangu wakanikumbusha kwamba hawana kura. Senene wangekuwa na kura tungeweka kwamba wana haki ya kutoliwa ha ha ha lakini wenye kura si wao, na wa kuliwa wengine wala hawatambui. Na katika ahadi zote hizi, hakuna inayoweza kufuatiliwa kisheria. Na wote ambao wameahidiwa hivyo wanatingisha kiuno na wao. Angalia akina mama wanavyoshangilia.

Sasa tulitegemea na nyinyi mngekuja na mapendekezo mengine ya kuboresha lakini wapi. Rasimu ya sumu ikageuka msahafu kwa hiyo tuliachiwa uwanja kucheza tunavyopenda. Haya mkategemea kwamba tutashindwa kupitisha, mkalainishwa na mkutano mwingine tena na kurudi na furaha kwamba mchakato umeahirishwa. Ama kweli nyinyi hamjui siasa. Baada ya mapatano, uwanja ulikuwa wazi tukamilishe kila kitu bila kipingamizi, na kura zilipotaka kutuvuruga, sisi ndiyo tunaoshika mpini kwa hiyo ikawa rahisi sana na waliotaka kutingisha tumewaondoa.

Ndiyo. Hii ndiyo demokrasia yetu. Na tuna uhakika kwamba tutapitisha rasimu yetu tu. Tunajua mtalalamika tena kidogokidogo, lakini hakuna mpango wa kuzunguka na kutoa elimu ya kweli, hakuna ambaye atakaa chini na kulinganisha rasumu yenu na rasimu yetu, hakuna ambaye atatoa vipeperushi na kuvisambaza nchi nzima, hakuna mwenye ujanja wa kukwepa marungu yetu yote ya dola pamoja na dola zetu za kuhonga. Mtaingia barabarani tena na kupigwa kidogo kisha tutapitisha rasimu tena bila wasiwasi.

Na usije kwangu na machozi ya mamba, ooh demokrasia imebakwa, ooh sisi wateule tumeondoa mambo yote ya kutishia maslahi yetu, oooh sasa unatumika udikteta kulazimisha katiba yetu, oooh mbele ya safari itazaa machafuko. Nani anajali machafuko ya kesho wakati anabugia leo. Nani anataka kujua kuna nini nyuma ya mlima wa pilao mbele yake. Kula na kusaza ndiyo mtindo wa kisasa, ndiyo mtindo wa kisiasa pia.

Najua utachukia sana barua hii Makengeza maana tumewaweza ndiyo maana tuna haki ya kutingisha ------ mbele yenu. Nawaambieni ukweli hata ukiuma namna gani. Na usinisumbue kunilaani na kusema nimesema uongo. Nionyeshe. Nionyeshe kwa mipango yenu madhubuti siyo kelele zenu za juujuu. Vinginevyo, karibuni kwenye katiba mpya ha ha ha ha.

We Makengeza, Wewe na wehu na wahuni na wahaini wenzako.

Sasa mtasema nini ha ha ha ha ha ha ha! Eti mnaona gele kwa nini tunachezesha viuno. Tunachezesha viuno kama tulivyowachezesha akili mchakato wote huu. Eti kuna mtu kaandika kama tungejua kutingisha akili kama tunavyotingisha akili nchi ingekuwa mbali sana. Amka Bwana, tuko mbali sana na tunazidi kusonga mbele na mbali zaidi.

Ndiyo. Ni nyinyi mnaotakiwa kujua kutingisha akili zenu kama tunavyotingisha kiuno sasa maana tumewazidi ujanja tangu mwanzo huku mnajidai mna akili kumbe mna ukili wa kusukwa.

Kwani sisi tulitaka katiba ya kujizika na dhiki zetu? Thubutu. Lakini tulipoona mmeshikia bango hadi wananchi wanalisoma kwa furaha, ikabidi tuwanyang’anye bango. Kwa nini mpate umaarufu bure. Na baada ya hapo tumeweza kuendesha mchakato vizuri sana. Kila mkibisha kidogo, tunaitisha kamkutano mlainike kisha tunaendelea kama kazai. Kwa kweli aliyetutibua katiba yetu tu ni wale ambao waliamua kuwa makini kuwasikiliza wananchi na kuzingatia maoni yao kiasi kwamba waliamua kusaliti msimamo wetu. Ndiyo maana imebidi kuwatukana. Tangu lini maslahi ya wananchi yapewe kipaumbele badala ya maslahi yetu.

Lakini hata hivyo hatukuwa na wasiwasi, zaidi ya kwamba wananchi wataamka lakini nyie mliotakiwa kuwaamsha mkasinzia wenyewe hivyo hatujawa na shida. Usiniambie kwamba mliazimia maandamano.

Hii ni sawasawa na kulala tu kama si kulazwa kutokana na dawa yetu ya usingizi inayotolewa na rungu letu. Kila mlipotangaza maandamano tulicheka maana tulijua mtaandamana kidogo, wengine watapigwa kisha kimya tena. Tunashukuru sana kwamba hamkusoma kwamba kuna mbinu nyingi za kupinga siyo kujipeleka tu barabarani ha ha ha.

Kwa hiyo mambo yote yamekuwa poa. Tuliendesha mabaraza ya kukatika kichama, bila wasiwasi na ilipokuja suala la kuchagua wajumbe wengine wa Bunge Maalumu tulicheka sana mlivyohangaika kupeleka majina maelfu kwa maelfu. Na tulipoweka wa kwetu wenye kuaminika tulicheka mlivyopiga kelele tena. Kila siku kelele , kila siku kelele juu ya vitu vidogovidogo huku sisi tunapeleka tunavyotaka. Mmekuwa kama abiria ndani ya basi.

‘We Bwana acha kukata kona vibaya ….

Mbona unaovateki namna hiyo

Konda umewaacha watu bado wanajisaidia

Huyu dereva ana leseni kweli

Na maneno mengimengi bila kutambua kwamba dereva anafuata maagizo. Badala ya kuhoji mchakato mzima mmekuwa kama yule mwenye nyumba katika hadithi ya Achebe ambaye wakati nyumba yake inateketea yeye anapoteza muda wake kufukuza panya waliokuwa wanakimbia nyumba ile, badala ya kuokoa nyumba yenyewe.

Haya basi, tukafika kwenye uwanja wetu, tayari kwa uburuzaji. Na sikatai, kidogo tulitingishika mlipotoka, tukafikiri kwamba labda mna mikakati murua ya kuwaamsha watu, kumbe yaleyale tu, yaleyale. Kutishia maandamano kisha kukaa kimya. Mmmh, kweli mmenifurahisha sana.

Halafu kung’ang’ania tu, kung’ang’ania tu rasimu ya sumu jinsi ilivyo mmetupatia nafasi nyingi bora kabisa. Kwani wale walikuwa miungu? Lazima walisahau mambo mengine, na kubwa kabisa hawakuandika katiba ya nchi isiyo na jina hivyo tumeweza kuahidi kila kitu kwa kila mtu ili kuficha jinsi tulivyoondoa yale ambayo yalitubana, pamoja na suala zito lenyewe la mahusiano ya ndoa.

Ndiyo, wasanii wamelalamika, wape, na wanawake, kabisa wape maana wapiga kura wengi ni wanawake, hata vijana wakorofi, wape, wakulima, wape. Mimi nilikuwa tayari kuwapa hata watoto wa shule za msingi iandikwe kwenye katiba kwamba ni marufuku kuwachapa viboko lakini wenzangu wakanikumbusha kwamba hawana kura. Senene wangekuwa na kura tungeweka kwamba wana haki ya kutoliwa ha ha ha lakini wenye kura si wao, na wa kuliwa wengine wala hawatambui. Na katika ahadi zote hizi, hakuna inayoweza kufuatiliwa kisheria. Na wote ambao wameahidiwa hivyo wanatingisha kiuno na wao. Angalia akina mama wanavyoshangilia.

Sasa tulitegemea na nyinyi mngekuja na mapendekezo mengine ya kuboresha lakini wapi. Rasimu ya sumu ikageuka msahafu kwa hiyo tuliachiwa uwanja kucheza tunavyopenda. Haya mkategemea kwamba tutashindwa kupitisha, mkalainishwa na mkutano mwingine tena na kurudi na furaha kwamba mchakato umeahirishwa. Ama kweli nyinyi hamjui siasa. Baada ya mapatano, uwanja ulikuwa wazi tukamilishe kila kitu bila kipingamizi, na kura zilipotaka kutuvuruga, sisi ndiyo tunaoshika mpini kwa hiyo ikawa rahisi sana na waliotaka kutingisha tumewaondoa.

Ndiyo. Hii ndiyo demokrasia yetu. Na tuna uhakika kwamba tutapitisha rasimu yetu tu. Tunajua mtalalamika tena kidogokidogo, lakini hakuna mpango wa kuzunguka na kutoa elimu ya kweli, hakuna ambaye atakaa chini na kulinganisha rasumu yenu na rasimu yetu, hakuna ambaye atatoa vipeperushi na kuvisambaza nchi nzima, hakuna mwenye ujanja wa kukwepa marungu yetu yote ya dola pamoja na dola zetu za kuhonga. Mtaingia barabarani tena na kupigwa kidogo kisha tutapitisha rasimu tena bila wasiwasi.

Na usije kwangu na machozi ya mamba, ooh demokrasia imebakwa, ooh sisi wateule tumeondoa mambo yote ya kutishia maslahi yetu, oooh sasa unatumika udikteta kulazimisha katiba yetu, oooh mbele ya safari itazaa machafuko. Nani anajali machafuko ya kesho wakati anabugia leo. Nani anataka kujua kuna nini nyuma ya mlima wa pilao mbele yake. Kula na kusaza ndiyo mtindo wa kisasa, ndiyo mtindo wa kisiasa pia.

Najua utachukia sana barua hii Makengeza maana tumewaweza ndiyo maana tuna haki ya kutingisha ------ mbele yenu. Nawaambieni ukweli hata ukiuma namna gani. Na usinisumbue kunilaani na kusema nimesema uongo. Nionyeshe. Nionyeshe kwa mipango yenu madhubuti siyo kelele zenu za juujuu. Vinginevyo, karibuni kwenye katiba mpya ha ha ha ha.

Shairi gumu sana hili..sijaelewa.

Atakayelisoma aje kunisimulia. Asante!

Hata maneno haya hamjaelewa?

Ndiyo, wasanii wamelalamika, wape, na wanawake, kabisa wape maana wapiga kura wengi ni wanawake, hata vijana wakorofi, wape, wakulima, wape. Mimi nilikuwa tayari kuwapa hata watoto wa shule za msingi iandikwe kwenye katiba kwamba ni marufuku kuwachapa viboko lakini wenzangu wakanikumbusha kwamba hawana kura. Senene wangekuwa na kura tungeweka kwamba wana haki ya kutoliwa ha ha ha lakini wenye kura si wao, na wa kuliwa wengine wala hawatambui. Na katika ahadi zote hizi, hakuna inayoweza kufuatiliwa kisheria. Na wote ambao wameahidiwa hivyo wanatingisha kiuno na wao. Angalia akina mama wanavyoshangilia.

Hata maneno haya hamjaelewa?

Ndiyo, wasanii wamelalamika, wape, na wanawake, kabisa wape maana wapiga kura wengi ni wanawake, hata vijana wakorofi, wape, wakulima, wape. Mimi nilikuwa tayari kuwapa hata watoto wa shule za msingi iandikwe kwenye katiba kwamba ni marufuku kuwachapa viboko lakini wenzangu wakanikumbusha kwamba hawana kura. Senene wangekuwa na kura tungeweka kwamba wana haki ya kutoliwa ha ha ha lakini wenye kura si wao, na wa kuliwa wengine wala hawatambui. Na katika ahadi zote hizi, hakuna inayoweza kufuatiliwa kisheria. Na wote ambao wameahidiwa hivyo wanatingisha kiuno na wao. Angalia akina mama wanavyoshangilia.

Hapo nimeeelewa ujumbe wooooooooooooooote asante sana
 
Back
Top Bottom