Huyo bibi nae! Sometimes grandparents wanatia hasira. Kwetu ni wavulana wawili na mimi msichana mmoja. Nakumbuka babu alikuwa akija nafukuzwa niende jikoni kupika au kumsaidia housegirl kazi badala ya kukaa sebuleni nikifanya homework au kuongea na kaka zangu na baba. Tulikuwa na fryer, rice cooker, pasi ya umeme, jiko la umeme n.k lakini pia tulikuwa na jiko la mkaa, la mafuta, mishumaa kwa ajili ya back-up (no generator), na pia kupunguza gharama za umeme manake huwezi chemsha maharage weee kwenye jiko la umeme lol.
Anyways wakati utakuja watoto watajifunza kupika na kufanya kazi na vifaa walivyonavyo. Kama ni boarding nilijifunza kupiga pasi na pasi ya mkaa, na kuweka malinda kwenye sketi kwa kuilaza katikati ya magodoro mawili (kama sandwich lol), na mimi ni mpishi mzuri sana, lakini mdogo wangu wa kiume anapika nyama kama hana akili nzuri.
Mambo mengine watoto watajifunza mbele kwa mbele, si lazima training yooote ifanyike nyumbani. Ulishawahi kusikia mtu anakufa njaa kisa hajui kutumia mkaa? Kama watoto wana akili, watafanya maarifa.