Tuzungumze, Tusaidiane

Tuzungumze, Tusaidiane

Dr leader

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2016
Posts
1,041
Reaction score
1,294
Kuna vijana wanatembea huku nafsi zao zimejaa majeraha . Wanabeba matarajio ya familia, presha ya mitandao ya kijamii, changamoto za mahusiano, na khofu ya kesho.

Tunatakiwa tuwe "role model", tuwe na mafanikio mapema, tuwe wazazi wa kesho, tuwe na furaha muda wote , lakini nani ametufundisha namna ya kuhimili yote haya?

Wengi wanalia faragha, wengine wamekata tamaa, na wachache wamepotea kabisa. Na kila wakijaribu kusema, huambiwa: “We bado mdogo, utaweza.” Lakini hawajui kwamba hata roho ya mtoto mdogo inaweza kuchoka.

Afya ya akili kwa kijana ni ya msingi. Sio kila anayefurahia mtandaoni yuko sawa. Sio kila anayesoma au kuzungumza kwa kujiamini hana vita ndani yake.

Ni muda wa kusikilizana. Kujifunza kuuliza, “Unaendeleaje?” kwa nia ya kweli. Kwa sababu kuna maisha nyuma ya tabasamu, na sauti nyuma ya ukimya.

Abuuabdillah ✍️
 
Back
Top Bottom