Tuzo ya Jamie Vardy imewafuta machozi Waingereza

blogmaster

Senior Member
Aug 15, 2015
167
74

.

Na Adam Mbwana,

Wakiamua wao hakuna anayeweza kupinga maana wao ndio wenye ardhi yao, wao ndio wenye ligi yao na wao ndio wenye vyombo vyao vya habari ambavyo vinaongoza kwa kuwapa watu umaarufu na kuufunika muda wowote wautakao wao. Lakini maamuzi hayo yanakuwa na nguvu endapo tu kama kuna mtu anayewatia kibuli maana huwezi kujisifia mshumaa gizani ilihali wenzio wana tochi ambayo haiyumbishwi na upepo wala mvua.

Kwa muda mrefu sasa, vyombo vya habari vya Uingereza vimekuwa vikiyatukuza majina yasiyo na asili ya kiingereza. Japokuwa hawawezi kuonyesha hadharani lakini ukweli ni kwamba inauma kumsifia jirani tena hadharani maana wapo watakaohoji kuwa kwani wewe umeshindwaje?. Na kuuma kwa roho kunanogeshwa zaidi na kuona jinsi timu yao ya taifa inaposhindwa kufurukuta kutokana na wachezaji wengi wa kiingereza kutofanya vizuri kwenye ligi yao hiyo ukilinganisha na wageni wanaokuja na kuondoka. Sasa kilio cha waingereza kimesikika

THE-SUN.png

Tovuti ya gazeti maarufu la The Sun iliripoti tuzo ya Jamie Vardy

Tuzo ya mchezaji bora wa kulipwa wa msimu huko nchini Uingereza ilikwenda Algeria, naweza kusema hivyo, kitu ambacho kwa namna moja au nyingine tunaweza kusema kuwa Waingereza walishindwa kufurukuta kwani Mahrez alitwaa tuzo hiyo mbele ya Jamie Vardy na Harry Kane, waingereza ambao kwa mwaka huu nahisi wamekuwa maarufu kuliko hata Malkia Elizabeth tena umaarufu wao ukitokea msimu mahususi ambapo timu ya taifa ya Uingereza itakuwa ikiwania kombe la Euro baadaye kule nchini Ufaransa.

KANE.jpg

Harry Kane na Jamie Vardy wakiwa katika majukumu ya timu ta taifa ya Uingereza

Ikionekana kama ni kupigwa kumbo baada ya fundi Mahrez kupewa haki yake, hatimaye Waingereza wamepata cha kujifariji msimu huu baada ya masaa kadhaa yaliyopita, mshambuliaji wa Leicester City ambaye ametia kambani mabao 22 msimu huu, Jamie Vardy kutwaa tuzo ya mwanasoka bora inayoandaliwa na Chama cha Waandishi wa habari za soka nchini humi (FWA) kwa msimu wa 2015-16 akimpiku mpinzani wake Riyad Mahrez ambaye wiki iliyopita tu alitoka kumliza kwenye zile tuzo kubwa pamoja na N’golo Kante, wote hawa wakitokea klabu ya Leicester City.

Katika kinyang’anyiro hicho, Leicester iliweza kutoa wachezaji saba ambao walikuwa wakiwania tuzo hiyo ambapo ukiachana na Vardy, Mahrez na Kante, wengine ni Danny Drinkwater, Danny Simpson, Wes Morgan and Kasper Schmeichel huku Vardy akiwa mchezaji wa kwanza kutoka Leicester City kutwaa tuzo hiyo

players.jpg

wachezaji wa Leicester City

Akizungumza baada ya kutwaa tuzo hiyo, Vardy alielezea kufurahishwa kwake na uteuzi huo na kwamba amefarijika sana huku akikishukuru chama hicho na kila mtu aliyempigia kura.

“Ni fahari kubwa kushinda tuzo hii kubwa na kuona jina langu limeongeza kwenye orodha ya wachezaji bora waliowahi kutwaa tuzo hii. Pia niwashukuru wachezaji wenzangu ambao ndio sababu kubwa nimeshinda tuzo hii”. alisema Vardy

Kwa ushindi huo, Vardy anakuwa muingereza wa 36 kutwaa tuzo hiyo tangu kuanzishwa kwake mwaka 1947 na pia ameweza kurejesha heshima nyumbani baada ya kuwa muingereza wa kwanza kutwaa tuzo hiyo baada ya misimu minne iliyopita kushuhudia tuzo hiyo ikitwaliwa na wageni. Scott Parker akiwa West Ham msimu wa 2010-11 ndio alikuwa mwingereza wa mwisho kutwaa tuzo hiyo kabla ya kuja kuvamiwa na Robin Van Persie, Gareth Bale, Eden Hazard na Luis Suarez

scott.jpg

Scott Parker

Baada ya waingereza kama vile Wayne Rooney, Frank Lampard, Steven Gerald na Scott Parker kutamba, sasa ni zamu ya utawala kurudi nyumbani na waingereza kufurahia na kuvitukuza vya kwao maana kwa kipindi kirefu sasa ligi hiyo imekuwa ikitawaliwa na wageni ambao wanakuja na kung’aa huku wenyeji wakiishia kusindikiza wageni.

Waingereza wameamua sasa maana wanajua fika kuwa mcheza kwao hutunzwa endapo tu anastahili kufanya hivyo. Hongera Jamie Vardy, Hongera Leicester City, Hongera Uingereza. Tuyasubirie magazeti maarufu nchini humo kama vile The Sun yataandika nini.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom