belionea
JF-Expert Member
- Mar 17, 2014
- 1,052
- 914
Usiyafunue sana mahusiano yako na huyo mpenzi wako kama hamjafika kwenye hatua nzuri ya kufunga ndoa, yaani;
1.Amejitambulisha kwenu.
2.Amekutolea mahari.
3.Harusi inajulikana ni lini
4.Amekutambulisha kwao
5.Kanisani wanajua
Nimezungumza hivi kwa makusudi kwa sababu wengi hulia hapa.
Unaanza kujitangaza kwa watu, mtandaoni, sijui una update status zako in relationship with. Jamaa hajawahi kufika hata kwenu, wala kwao hupajui na zaidi ya yote hata kwa rafiki zako kila kona na kila muda unamzungumzia mtu wako huyo, hata kanisani kwenu hawatambui.
Ikitokea mmeachana, moja ya kitu kitakachokutesa ni mazingira na marafiki na mtandao uliomuweka, utasema je, hasa wakikuuliza juu ya yule mpenzi wako au ndoa ni lini, kumbe mlishaachana.
Utajikuta unalia, unaona aibu, mazingira yanakuzomea, una tafuta pa kuficha sura yako. Kwani ungekaa kimya ingekuwa je, au haujui wanadamu wanabadlika kuliko kinyonga. Kuna maumivu mengine mnajitengenezea wenyewe kwa kukosa hekima na maarifa.
Na zaidi ya yote unaanza kuwekeza vitu kwa huyo mtu wako, au haujui hazina yako ilipo ndipo moyo wako utakapokuwepo.
Unaweza je kuwekeza vitu kwa mtu wakati hakuna hatua yeyote mliyofikia ya kuoana? Hauoni siku akikubadilika hivyo vitu vitakutesa, utaanza kukumbuka ulivyowekeza,jambo litakalo gharimu moyo wako.Mungu ametupa akili tuzitumie,hata kama anakuambia
I love you mara 7,70 kisiwe ni kigezo kuwa hawezi kukusaliti au kukuacha ( Yuda alimbusu Yesu, lakini alimbadilikia),hapo kwa Yuda nimechomekea tu hahhahaha. Ukimpata mtu, mwombe Mungu, kaa kimya, hakikisha huo uhusiano unakuwa na mwelekeo.
Usiingie haujui ndoa ni lini,unajiendea tu, hata kanisani haujawahi kukaribishwa, ila umekaribishwa kweenda nyumbani kwa huyo mwezio ( au ndiyo mapenzi nipige shoti hadi nitetemeke. Hiyo shoti angalia usinaswe juu ya nguzo maana utakufa kiroho na kimwili.
Mambo mengine muwe mnatumia akili, si kila kitu kinahitaji maombi.