Siku moja nilikuwa naangalia kipindi cha usalama barabarani nikapata maelezo mazuri kutoka kwa mkuu wa kitengo cha usalama barabarani nchini kamanda Mpinga kuwa kwa sasa leseni zote ziko kwenye mtandao na faini inaweza lipwa cash au kulipa bank au kurusha mpesa kwenye namba maalum ya polisi na taarifa kutunzwa kielectroniki.
Wiki iliyopita nilikamatwa na polisi wa usalama barabarani nikaambiwa nilipe faini papo kwa papo, sikuwa na pesa mfukoni ila kwenye mpesa nilikuwa na salio kidogo, nikatizama wapi naweza toa mpesa nikakosa, nilimwambia polisi aniandikie notice ya kosa (notification) ili nikifika niendako nitalipa na kumjulisha kuwa nimelipa yule polisi alikataa kwa madai hamna namna ya kuhakiki kama hiyo pesa imelipwa kweli.
Mwafaka tulikubaliana twende kituoni wote na kuacha gari na funguo nikaenda kuchukua pesa kwenye kibanda cha mpesa nakuja kulipa faini ndipo nikaruhusiwa kuondoka. Ukweli ilibidi nirudi km zaidi ya 40 hadi kituoni hivyo nikawa nimeendesha 80km kwa ajili tu ya kulipa faini na haya makilimo kwanza yanavyokula wese timing yangu ikawa imevurugika kabisa.
Napendekeza polisi watangaze namba ya mpesa aliyotuonyesha kamanda mpinga kwenye TV ili ninapokuwa sina pesa basi nirushe kwenye mpesa ya polisi nakuruhusiwa kundoka badala ya kuzungushana siku nzima kisa tu sijabeba pesa mfukoni.
Kama polisi imeweza kununua camera za kupimia mwendo nchi nzima basi inunue na EFD mashine za kufanyia miamala ili kama hauna pesa basi uweze kutumia atm card au mpesa kulipa faini.