MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,244
- 7,970
Ni mjinga pekee ndiye anayekurupuka na kupiga kelele kubeza uwepo na ustawi wa vyama vya upinzani, ni wendawazimu kusema wapinzani ni wapiga kelele hawana msaada wowote kwenye jamii. Haya ndio mawazo ya baadhi ya watu wasiolionea huruma taifa hili lililojaa umaskini Mkubwa pamoja na kua na rasirimali za kila aina.
Hivi kwa mtu mwenye akili timamu hawezi kutofautisha uendeshaji wa serikali chini ya mfumo wa chama kimoja na mfumo wa vyama vingi? Mtu badala ya kutoa njia mbadala ni kitu gani kifanyike ili kuimarisha upinzani uendelee kuikosoa serikali itoke usingizini eti unabeza. Huu ni upunguani uliovuka mipaka ha ni wa kukemea kabisa.
Ukiona kuna mtu anabeza upinzani ujue kua amechukia kwa sababu anahisi wapinzani watamnyang'anya kula yake, mtu wa namna hii hawezi kumsaidia mwananchi na huwezi kuleta mabadiliko yeyote katika jamii.Hana nia njema kwa vile hataki kukosolewa anataka kuendelea kukalia makandokando yake.Watu wa aina hii wameliua taifa na wametufikisha hapa tulipo.
Mtu wa aina hii hata sikua moja hawezi kuridhishwa na chama chochote cha upinzani kinachoenda kinyume na chama anachokipenda yeye, hii ndio maana leo CHADEMA,CUF,NCCR, ACT na vyama vingine vinavyoikosoa serikali vinachukiwa kwa sababu hiyo.
Wao wanaeeza kila mpinzani anayeikosoa serikali au anayekosoa chama chao kwa sababu ya tamaa binafsi,hata wapewe nyeupe wanasema nyeusi tu kwa sababu ya tamaa zao.
Tutambue mchango wa upinzani tuache umbumbumbu wa makusudi kubeza umuhimu wa upinzani, leo hii kuna ushindani wa kuleta maendeleo kwenye majimbo ya wanasiasa flani ili kuogopa kung'olewa na wengine baada ya kushindwa kwao.Leo hii CCM wanatumia gharama nyingi na nguvu kubwa kujaribu kuwadhibiti CHADEMA ambao wamejaribu kuthubutu kutaka kuwaondoa kwenye nafasi zao. Kusingekua na CHADEMA nchini pengine hata CCM wasingetumia rasirimali hizo zote, wangebaki kutibuana wao kwa kwao.
Ieleweke kwamba UPINZANI nchini umewaweka chama tawala pamoja, umewafanya waogope kulumbana wao kwa wao kuogopa kugawanyika hali itakayosababisha wengine kukimbilia upinzani na kukifanya chama tawala kife au kiodoke madarakani,Leo hii CCM ni wamoja bungeni kwa sababu ya upinzani. Hivyo basi kwa wanaCCM wenye akili hawathubutu kuuponda upinzani kwa sababu wanaelewa umuhimu wao.
Mwenye roho ya "kutu", aliyejawa tamaa na uroho w madaraka,aliyejawa tamaa na chuki hata siku moja hawezi kukubaliana na uwepo wa upinzani, anatonekana ni mtu tu siku atakapoonekana kukiunga mkono chama tawala.