Fortilo
JF-Expert Member
- Apr 10, 2012
- 5,456
- 16,663
Nimeshutshwa na maneno ya Kiongozi mkuu wa Chama cha ACT wazalendo kuhusu suala la kuteuliwa kwa mshauri mkuu wa chama kuwa Katibu mkuu wa wizara ya maji na umwagiliaji.
Japo kuteuliwa kwa Prof. Kitila mkumbo ni jambo la kawaida ukizingatia wasifu wake, lakini suala hapa ni cheo alichokuwa nacho ndani ya Chama cha ACT ambacho kinaonekana kama kinakuja kwa kasi ya ajabu katika ulingo wa kisiasa Tanzania, hadi kufikia level za kupambanishwa na Chadema..
Bado nikaunganisha dots na zile mbwembwe za mgombea Urais wa ACT kwenda kumkabidhi Rais Magufuli Katiba na ilani yenu pale Lumumba mara tu baada ya uchaguzi, hii inatoa taswira tofauti sana kwa watu waliozoea siasa zetu za upinzani hapa nchini.
Zitto amesema"Rais ameamua kufanya kazi na watu wote bila kubagua itikadi za vyama'
Juu kidogo ya aya hiyo anasema"Kitila ni mtumishi wa umma hivyo, Nafasi aliyopata ni kama kupanda cheo tu kama mtumishi wa umma"
Kwa haraka kabiasa ni kama hakuna shaka, ila kiukweli .... tatizo lipo hapa>>>
Pengine Zitto alipitiwa, Kwanza kabisa ni marufuku kwa mtumishi wa umma kuweka hadharani itikadi yake ya kisiasa, kosa ambalo mara nyingi hufanywa na watu wa CCM katika teuzi zao....
Kama mnaweza kurejea suala la Prof. Baregu, Lwaitama na wengine wengi wa UDSM.... ila Kitila aliendelea kuvumiliwa sana tu, suala ambalo halijawahi kutolewa ufafanuzi hadi leo.
Hiyo pekee inaweza kuondoa uhalali wa kauli mbiu yenu ya 'taifa kwanza leo na kesho" taifa gani msilojali taratibu na sheria zake tena kwa maslahi ya muda mfupi wa kisiasa?
Hilo wala sio kosa kubwa kwenye dunia ya tatu, tumeshazoea ...
Makosa mliofanya ni kama mawili hivi , NO , ni matatu.
1. Kumruhusu mshauri wenu kuwa sehemu ya serikali ambayo nyie mnaikosoa!
Hapo mmezibwa mdomo likija suala la uhaba wa maji mjini na vijijini.. hamna la kusema... kwakuwa mmekuwa sehemu ya mfumo huo huo mbovu.
2. Magufuli controversy ....
Rais Magufuli hatabiriki likija suala la kazi na mtazaomo wake binafsi.
Kwa sasa ni kama Maisha ya kisiasa ya Prof. Kitila na ACT mmeyakabidhi mikononi mwa Mwenyekiti wa CCM na Rais wa JMT.. kwamba akiamua tu kumtumbua kwa sababu ya uzembe au kitu ambacho hakija mpendeza kama ilivyo kwa Nappe, mkatengenezewa zengwe mtaficha waipi sura zenu?.
3. Sera na ilani inayotawala ni ya CCM .
Hivi mtu wa ACT unakubalije kusimamia utekelezaji wa sera za CCM?
Naelewa Kuwa Mkumbo haendi kuwa Waziri, lakini ubavu wa kumkoromea waziri wa maji, naweza kuapa, uwezo huo hana..... kwahiyo hata kama ni sera na ilani zilizofeli, hana cha kupunguza wala kuongeza.... zaidi ya hasara kwa mustakabali wenu wa kisiasa.
Ubinafsi wa Prof. Kitila Mkumbo?
Sio ubinafsi , kumbuka anaelekea 50, na hakuna cha maana anachovuna upinzani zaidi ya show za TV na Radio, kama binadamu lazima ujifikirie na wewe kidogo.
Hata kama ni mambo ya kutunza heshima ya kuwa na msimamo... hiyo aliipoteza zamani hata kabla ya April 2016 alipokuwa anamnanga Magufuli kuhusu kuteua Wahadhiri... hana cha kuoteza.
Kumbuka ni majuzi tu Kitila Mkumbo alitaka kutoana shati na Tundu lissu juu ya kanuni za uchaguzi wa EALA ambapo yeye alikuwa mgombea, nadhani Kuna kitu Rais ameona akaamua kuwakomesha maadui zake kama alivyofanya kwa Mkuu wa mkoa wetu pendwa "ili uwe bosi wa maadui zako'.
Prof. Kitila ni mpambanaji wa uhakika(Nakumbuka akitupa somo 2010 Landmark hotel kipindi cha uchaguzi akiwa chadema) .
Ni mtu aliejitolea jasho na damu kufika alipofika katika maisha yake.
Vile vile, nadhani kwa cheo cha Ukatibu mkuu, akicheza karata yake vizuri na kutupa kadi ya upinzani hadharani , ni taa ya kijani katika historia yake binafisi.
Dunia ya tatu hii, ni lini Mtu apewe cheo hicho akatae? unless kama chama kinaweza kuja kushika madaraka mapema..... ACT ni kichanga mno hata kufikiriwa kwa miaka mingi ijayo.
Kwa mustakabali wa Kitila mwenyewe naona kama amechupa kwa maisha yake binafisi, ila kwa chama ni kama amekiharibia kabisa.
Kuna la Kujifunza...?
Duniani kote, wapinzani wakianza kula na watawala nchi inakuwa haina upinzani wa kweli na mtaendelea kuwa wapinzani wa kuganga njaa milele...
Nakumbuka ya Morgan Tsvangirai wa Zimbabwe, Raila Odinga wa Kenya, na wengine wengi.
Mtazamo wangu
ACT mmefanya makosa, ila bado mna nafasi ya kujisahihisha.... pengine press ya Zitto imekuja mapema mno kabla ya kutafakari athari zake kwa chama na wafuasi wenu, hasa ukizingatia ndio kama mmeset trendi kwa wanachama wachanga na wao pia kujiweka karibu na watawala ili na wao wapate chochote, kama mnavyofanya nyie.....
Pengine Zitto nae akiteuliwa ataenda kwa kisingizio cha weledi na uzalendo kwenye vyama vya upinzani.. which will be quite irrelevant......... pls Sir, don't.
He who pay the piper chose the tune,
Magufuli has played it smart, i applaud you Sir.