Tuunge mkono ujenzi wa Dar es Salaam mpya

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,531
RAIS John Magufuli jana alizindua rasmi ujenzi wa barabara ya juu (flyover) katika makutano ya Tazara jijini Dar es Salaam. Rais alisema ujenzi wa barabara hiyo ya juu unaotarajiwa kuanza karibuni, utakamilika Oktoba 2018 na kugharimu Sh bilioni 100 za Tanzania.

Rais alitamani kuona ujenzi huo unakamilika hata kabla ya muda huo na sisi tunawasihi makandarasi kujitahidi ili hilo liwezekane. Rais pia alitaja miradi mingine inayotazamiwa kujengwa ikilenga kuondoa kero za msongamano katika jiji hilo kuwa ni pamoja na kukamilika kwa daraja la Kigamboni ambalo litazinduliwa rasmi keshokutwa, Jumanne, ujenzi wa barabara ya kutoka Kigamboni hadi Chalinze, pamoja na barabara nyingine ya juu itakayojengwa Ubungo.

Miradi mingine inayokuja ni wa daraja litakalopita kando ya bahari kuanzia Koko Beach hadi Aga Khan, ujenzi wa Reli ya Kati utakaosababisha magari makubwa kutoingia tena katikati ya jiji pamoja na ukamilishaji wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART).

Kama alivyosema Rais, miradi hiyo itaibadilisha Dar es Salaam ambapo mbali na kupunguza kero za msongamano itaipa sura mpya Dar es Salaama na kuifanya kuwa mahali salama zaidi kama lilivyo jina lake. Aidha, Rais Magufuli alisema miradi hiyo pia itatengeneza ajira kwa Watanzania.

Tunaipongeza Serikali ya Awamu ya Tano, kwa kuanza kutekeleza mradi huo wa ujenzi wa barabara ya juu Tazara na mingine inayokuja, hatua inayodhihirisha kwamba ahadi za Rais Magufuli alizozitoa wakati akiomba kura mwishoni mwa mwaka jana ni za kweli na zitatekelezeka.

Kupunguza, kama si kuondoa kabisa kero ya msongamano jijini Dar es Salaam ni hatua muhimu kutokana na faida zake nyingi zikiwemo za kiuchumi kwa kuwa muda mwingi sana wa uzalishaji umekuwa ukipotea kwenye foleni sambamba na mafuta mengi yanayotumiwa na magari katika eneo fupi.

Wakati Serikali kwa upande wake ikidhamiria kutekeleza miradi hiyo muhimu, sisi wananchi kwa upande wetu tunatakiwa tuwe tayari kuisaidia ili ikamilishe malengo yake ambayo yana faida kubwa kwetu tunaoishi sasa na hata vizazi vijavyo.

Mambo ya kuisaidia mengi lakini kubwa, kama alivyosema Rais Magufuli, ni kulipa kodi. Bila kulipa kodi, hakuna ubishi kwamba miradi mingi tunayoitarajia kuwa chachu ya mendeleo ya nchi yetu itabaki kuwa ndoto.

Na kwa kweli hatuna sababu ya kukwepa kulipa kodi kwani matumizi yake tunayaona. Lingine ni kuwa waangalifu kwa kutunza miundombinu hii tunayojengewa na serikali yetu. Ni vyema pia watakaobahatika kupata ajira kwenye ujenzi wa miundombinu hii, wakamsikia Rais alivyowaasa; kuacha vitendo vya wizi wa vifaa kwa manufaa ya Taifa.
 
Huo mradi wa DART ni kichaa.

Hizo barabara wangezifumua wakaweka barabra 4 kwenda na 4 kurudi. Kidogo ingepunguza msongamano ila hayo makarandinga ni biashara kichaa.

Huu mradi lazima ufe.
 
Vipi ule mradi wa barabara 4 toka Ubungo hadi Chalinze? Au ndio imekuwa replaced na Kurasini_Chalinze kupitia kando kando ya jiji?
 
Kama JPM akiwa na nia ya dhati kubana upigaji then yote haya yanawezekana. JPM ataweza tu pale atakapoikana au kuiumiza CCM na mambo yake yote.

Sie wengine tusio na vyama au wale wa upinzani hakuna effect tena. Uchaguzi ushaisha
 
sema tuwaunge mkono ukawa kwa plan zao nzuri za maendeleo.

swissme
 
Huo mradi wa DART ni kichaa.

Hizo barabara wangezifumua wakaweka barabra 4 kwenda na 4 kurudi. Kidogo ingepunguza msongamano ila hayo makarandinga ni biashara kichaa.

Huu mradi lazima ufe.
Asante kwa uchawi na ramli!
 
Back
Top Bottom