TUUNGANE KWA PAMOJA

TUUNGANE KWA PAMOJA

Persistance

Member
Joined
Aug 14, 2017
Posts
10
Reaction score
2
Kwa takribani siku tatu taarifa ya kushikiliwa kwa Ndege yetu aina ya Bombardier Q 400 huko nchini Canada imekuwa na mjadala mpana kiasi cha kusababisha sisi tunaopenda kupitia maandiko (Literature review) kuingia maktaba na kuanza kuyapitia na kuyapembua.

Kwanza nilianza kujiuliza je, Ni kweli nchi yetu inadaiwa kwa kuvunja mkataba wa ujenzi Wa barabara ya Wazo Hill hadi Bagamoyo? Jibu Ni ndiyo Serikali iliingia mkataba Wa kandarasi ya ujenzi Wa kujenga barabara ya Wazo Hill hadi Bagamoyo yenye urefu Wa kilomita 45 na kampuni ya lmpresa Ing. Fortunato Federici(IFF) kupitia mkataba namba 10050/98/99. Baada ya mkataba huo kampuni ilianza ujenzi,kwa bahati mbaya Ujenzi wa barabara hiyo haukufikia viwango, hivyo kulazimu mwenye kutoa kandarasi ( serikali)kuhoji 'value for money' baada ya kampuni ya IFF Kushindwa kutoa majibu ya kuridhisha ilisimamishwa kuendelea na ujenzi huo usiokidhi vigezo vilivyoanishwa mwaka 2009.

Baada ya kusimamishwa Wakakimbilia Mahakamani, mahakama ikawapa ushindi na kutoa amri ya kulipwa Dec2009/June 2010, Hata walivyokwenda kwenye mahakama za usuluhishi jambo hilo liliendelea kubaki hivyo hivyo, Kwa upande wa Serikali yetu iliendelea kushikiria msimamo kwamba kampuni hiyo haikustahili kulipwa kutokana na kushindwa kufanya kazi kwa mujibu wa mkataba.

Tukumbuke haya yote yalifanyika Serikali ya awamu ya tano ikiwa bado haijaingia madarakani,na wala RAIS Wa sasa Dkt.Magufuli alikuwa Si Waziri mwenye dhamana ya ujenzi. Na kwa kipindi hicho chote tangu mwaka 2009 madai haya yalikuwepo na yalikuwa yakifahamika vyema . Nini kimetokea?

Kama tutakumbuka vizuri RAIS wetu Dkt.Magufuli ametangaza rasmi VITA YA KIUCHUMI baada ya kupokea ripoti ya pili ya uchunguzi Wa kisheria na kiuchumi kuhusiana na mchanga Wa Madini unaosafirishwa nje ya nchi iliyowasilishwa tarehe 12.06.2017 , Vita hii pamoja na kugusa maeneo mengine, sehemu kubwa imegusa kampuni ya uchimbaji Madini ya BARRICK na washirika wake ACCACIA zenye Makao makuu Canada.

Kama tunavyojua baada ya kuundwa tume ya kuchunguza hasara,aina za Madini na taratibu za kisheria kama zinazingatiwa, ilibainika kuwa kulikuwa na Madini yanayofikia zaidi ya saba yalikuwa yakitoroshwa ,kulikuwa na ukwepaji kodi mkubwa tu pamoja na malimbikizo yake ambayo tayari TRA ilishawapelekea demand notes. Na wanapaswa kulipa.

Baada ya kuwekwa bayana wadeni wetu wameamua kwa makusudi kabisa kutumia mbinu inaitwa kitaalam ice breaker ( kuvunja ukimya) kwa kupitia mawakala wao. Na kwa bahati mbaya wamelianzisha vibaya kwa maana ifuatayo, kwanza kampuni Ya (Stirling Engeneering) hawakuwahi kufanya kazi na Tanzania, badala yake hawa mabepari Wa cannada wanataka kufanya kama yale ya Escrow na IPTL au yale ya Richmond na Dowans.

Ukirejelea huko mwanzo nimefafanua vyema kuwa Aliyefanya kazi na Serikali ya Tanzania anaitwa Impresa Ing. Fortunato Federici kupitia mkataba namba 10050/98/99. Mdeni wa Tanzania ni IFF ya Italy, ila sasa anayedai ni kampuni kutoka UK! hapa utashangaa kidogo lakini kigezo anachotumia Anadai kwamba yeye ame acquire mali na madeni ya IFF, inaweza kuwa kweli, lakini ukipitia nyaraka na kumbukumbu mbalimbali hakuna taarifa rasmi kutoka IFF kwamba amekuwa acquired? Jambo jingine tumemsikia naibu msemaji wa Serikali amesema Kuna uhusika Wa wanasiasa , nadhani inatokana na kwamba mwakilishi wa hiyo kampuni iliyodandia (Stirling) ni Advocates company ambayo ipo Hapa nchini ambayo Managing Partner Wao ni wanachama wa Chadema.

Hata hivyo inaonesha Baada ya mashauriano ya muda mrefu kati ya IFF na Serikali ,na kama inavyojulikana kampuni huanzishwa na hatimaye hufa. Kampuni ya IFF ikafa huku Tanzania ikiwa haijapatiwa taarifa rasmi za huyo mdai wa sasa (Stirling Engineering) ambaye anaonekana ndiye amenunua mali na madeni ya IFF. Kimsingi hawapaswi kutudai hili linafahamika vyema na hata Canada inajua sema ndio hivyo tuko vitani na Ndege tunatengenezea kwao.
Kwa mujibu wa nyalaka Hao wadeni wa sasa wamesajili hiyo award ya Mahakama nchini Uganda, Ufaransa, Canada na Uingereza. Sasa ukipitia mlolongo huo utangundua kwamba vita ya kiuchumi baina ya Tanzania na Canada imefikia mahali ambapo Canada wanataka kuitishia Serikali ya Tanzania ili ikishtuka tu wao waweze Ku win(kushinda) kitu ambacho naamini kwa sasa Ni ngumu sana.

Pili inaonekana wamebanwa kwa kiwango cha juu kiasi cha kutumia mbinu ya Ku spoil water hasa kwa kuwatumia watu ambao wanaweza kusema na kuzua mjadala nchi nzima, tukumbuke Hawa mabepari hutumia siraha zifuatazo kuhakikisha wanashinda vita ya kiuchumi ,hutumia Rushwa,hutumia propaganda za vitisho,hutumia watu maarufu kwenye nchi au Eneo husika ili kujenga hofu kwa wengine na wakishindwa hutumia mbinu ya kuchonganisha ili kuzua ugomvi kwa kuwaahidi watakaowaunga mkono Mali na vyeo hata wengine huahidiwa kupewa madaraka ya nchi pale vita vikizuka ili kuiondoa Serikali madarakani.

Kwa Bahati nzuri hivi sasa watanzania walio wengi tupo imara tumeelewa lengo na nia ya dhati ya Serikali hii ya awamu ya tano ya kupambana na wahujumu uchumi na wapinga maendeleo Wa aina yoyote wawe waafrika wenzetu au wazungu au Wa rangi yeyote kama nchi iko tayari kupambana nao Mwisho lakini Si kwa umuhimu Ni kuwakumbusha tu watanzania wenzangu hasa vijana nchi yetu ipo vitani tena vita ya kiuchumi ,maadui zetu wanaweza tumia mbinu zote ikiwemo divide and rule,tusikubali hili litokee tusimame upande Wa nchi ,tusimame upande Wa rasilimali zetu ,tusimame na Rais wetu Magufuli.

Copied from I.C.
Big up bro.
Utafika mbali.
 
Back
Top Bottom