Nikupongeze sana kwa maono yako mdau binafsi sio mkazi wa Kilosa lakini nimevutiwa sana na mji wa Kilosa na mara nyingi nimekuwa nikienda huko maeneo mbalimbali kama Zombo,Ulaya,Kigunga,Miyombo et al fursa zipo nyingi ila watu wamelala usingizi wa pono katika lindi la umasikini.Hamasa isiwe kwenye siasa peke yake hata katika nyanja nyingine pia kama nilivyosema awali fursa zipo nyingi sana Kilosa na nimetembelea sana hayo maeneo ila hivi karibuni migogoro ya ardhi ni wazi itaibuka na sina hakika kama serikali za vijiji zimejipanga kutatua migogoro hiyo na kingine ni uhalibifu mkubwa unaofanywa na wafugaji hususani Wamasai wamekuwa na tabia ya kuchoma misitu ili kuweza kupata malisho mapya kipindi mvua zinaponyesha,sasa hii inapelekea uharibifu mkubwa wa mazingira na uoto wa asili haswa misitu ya asili.