Tuthamini taaluma

chongoe

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2019
Posts
1,221
Reaction score
2,971
Ilikuwa siku moja upepo mkali sana baharini hakuingiliki; hatuwezi kusafiri sababu upepo ulikuwa mkali. Sasa ikawa sina ujanja, nasubiria bahari itulie tuanze safari.

Bahati mbaya ilichukua siku nne bahari kutulia na mfukoni sina kitu. Mida ya asubuhi naelekea zangu beach nikafanye mipango ya pesa angalau nipate kitu sababu baharini sijui lini itatulia, kabla sijafika beach, nikakutana na msafara wa magari umebeba maiti.

Ikabidi nisimame pembeni ya barabara; ndio sharia kwa Waislam. Lakini muda huo nawaza nitakula nini maana siku ya nne hali yangu ngumu, nakula ila kwa kudoeadoea.

Mara ghafla ile gari ilienda kusimama kwa mbele, kuna jamaa aliteremka akaja. Kumbe namfahamu na yeye anifahamu; tulisoma wote Tanga. Baada ya kunifikia akaniambia twende kwenye gari tupeleke maiti ikaoshwe. Wakati anasema hayo, mimi nawaza beach kwanza nikaangalie jahazi usalama wake. Jingine, hali yangu kifedha ngumu ikabidi nimwambie yule jamaa. Akasema we twende wala usijali, basi nikapanda ndani ya gari mpka unapofanyika msiba tukateremsha maiti.

Yaani muda huo mimi nina njaa kinoma, alafu ni asubuhi hiyo. Baada ya kuteremsha ikaingizwa ndani. Baada ya muda yule jamaa akaniita na kuniambia akasema itabidi Mimi nioshe maiti. Sikuwakatalia kuosha; ila kutokana na kazi yangu ya bahari, kuosha maiti ni kama uchuro. Baadae ntawaeleza kwanini inakuwa uchuro sisi kuosha maiti.

Wenye maiti walinambia watanipa 25000 Baada ya kuwaoshea maiti yao. Sasa wakati naingia chumbani nikasikia jina langu linaitwa ikabidi nirudi kuangalia nani ananiita. Alikuwa mtu mzima wastani tu; akanisalimia pale mbele za watu kama vile twajuana kumbe wala simjui. Akaniambia samahani kwa muda wako, nisaidie jambo nitakupa pesa. Nikamuuliza jambo gani, akaniambia yeye amepata khabari kuwa mimi ndio ntaenda kuosha maiti kwahiyo akanambia: "Naomba utapoenda kuosha maiti mimi nachohitaji ni maji ya maiti na kipande kidogo cha kitambaa ambacho hufunikiwa maiti kwa ajili ya kuoshea"

Pia kasema nakupa laki moja; ntakukabidhi hapo hapo baada ya kumaliza.

Nitaendelea wadau. Hiki kisa kisa kirefu sana.

Samahani kwa muandiko mbovu. Mimi nahodha tu
 
Baada ya miangaiko ya week nzima tunatulia sebuleni kuiangalia hii movie
 
Basi baada yule mzee kuniambia Yale
Ikabadi nimuambie kwamba maiti Mimi hainihusu siwezi kufanya yale hata kama Nina njaa yule mzee akaniambia kwa shida aliokuwa nayo nisipomsaidia nitamjua vyema sababu yeye kaelekezwa aje pale kwenye msimba na waliomuelekeza aje kwangu kuwa Mimi muoashaji ni baadhi ya wenziwe ambao wapo msibani kusema ukweli ile pesa niliitaka kweli sababu ile wiki bahari ilichafuka sikufanya kazi nikaingia ndani ikabidi nioshe ile maiti kabla sijamaliza alikuja mtu mwingine aliingia ndani na kiniuliza hujapewa salam zozote nika mwambia hapana akasema naomba utusaidie tupe tunachohitaji tunakuongeza hamsini kwahiyo sasa iwe laki na hamsini aisee uzalendo ukanishinda nikawaanbia nipeni kabisa yule jamaa akatoka nje alafu akarejea akaleta pesa kwakuwa nilikuwa naosha maiti nika mwambia nitilie mfukoni akaweka akaniambia baada ya mazishi tuonane ndio nimkabidhi basi nilivyo maliza kuosha nikashona sanda akavishwa maiti ikaswaliwa pale pale wakati huo ninayo maji ya maiti kitambaa tayari nshaandaa ili niwape wale wazee nikaenda kuweka kwangu tukaenda kuzika baada kumaliza kuzika nikapewa pesa ya uoshaji mi nikaondoka zangu beach sasa wale wazew huku wakawa wananitafuta yule anae nifaham akwaambia kaenda zake beach wakaja mpaka beach wakaniambia niwape mzigo wao nikawaambia nimeuweka ndani kwangu wanitafute jioni kwa bahati jioni niliwakwepa ikabidi usiku nisafiri kibiashi jahazi yangu nikapakia koki za pweza na samaki nikaanza safari maana nilienda kulala jahazini alfajiri jahazi ikaanza safari kumbe wale wazee mchongo wote wanaujua wa Mimi kuondoka nimetoka mafia nawahi kisiju nilishindwa kuwapa vile sababu niliona ushirikina ila yaliokuja kunitokea nilijuta bora hata ningewapa tu baada ya kufika kisiju ile nafika tu bandalini nakutana na mzee mmoja akaniambia kuna watu wanataka mzigo wao usipowapa Leo siku tano humalizi dunia unaiachaa aisee nilidhani utani si unajua ujana tena dharau kumbe wachawi wana chama chao dunia nzima Mimi sijui sasa ikabidi nitafute mawasiliano ya nilipotoka ili kuwapoza wale wazee wanisubirie kweli nilipata kuongea nae yule mzee alienipa pesa nime mwambia anisubiri nikirudi namkabidhi sasa yule mzee akakataa akasema Mimi siwezi tena sina mamlaka yakikoseana Leo basi ila nijiandae aisee kusikia hivyo nilipagawa ikabidi nimpigie simu babu nikamueleza mwanzo mwisho babu akaniambia achana nao hawawezi kukuua mi ntawaonyesha ila baadae ntaenda onana nao baada ya hapo mi nasubiria majibu ya babu sasa pale bandalini baada ya Mimi kuteremsha mzigo ukaingizwa garini tukapewa hela yetu kwa bahati siku ya pili tukapakia mzigo ili turudi mafia kabla ya kuondoka usiku ile jioni babu kanipigia kuwa alienda ila jamaa hawakukubali pia wakamwambia mjukuu wako tutamuonyesha hii wiki lazima aondoke babu kipindi hiko anaongea na Mimi anasema hata akijisaidia hakitoki kinyesi cha kawaida yani anajisaidia yai anakunya yai
Mimi kusikia hivyo nikazidi pagawa nawaza niondoke nimu wahi babu au niende kwa mtaalam kwanza maana wasije nizamisha baharini


itaendelea waungwana nipo baharini kisiwa cha kwale nasubiria maji yajae niingie kisiju mnivumile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ