Tutaikumbukaje Tanzania ya enzi hizi

Waridi

JF-Expert Member
Mar 30, 2008
1,025
172
Kura lipewa kikwete,maendeleo tupate,
wapinzani wasipate,wabaki kutokwa mate,
tulimwamini kikwete,tukampa zote kete,
maisha bora alete,kumbe ghilibu siasa!

Tutamkumbuka hasa,edo ngoyai lowasa,
alivyotulisha kasa,kwa mengi yake makosa,
richimond aligusa,wabunge wakamtosa,
ama kwa kweli siasa,siri zake mbona nyingi!

mkataba wa buzwagi,alisaini karamagi,
ukazua hoja nyingi,tena hoja za msingi,
kulikoni karamagi,akaiuza buzwagi,
mbona si mnywa konyagi,na wala havuti bange!

Kumbuko rada na ndege,mtaje enduru chenge,
naye ni memba wa genge,la kutufanya makenge,
sisi twala maharage,yeye vinono kingunge,
la mafisadi ni genge,la kutuletea dhiki!

Kwa dhiki twala mapanki,yani samaki mabaki,
minofu wanaipaki,na mifupa inabaki,
sio kwamba hatutaki,sisi kuwala samaki,
jinamizi la mapanki,halina cha mwanaume!

Kajitahidi karume,ili mwafaka ukwame,
kacheza karata dume,wana kafu kiwaume,
sisiemu chama dume,hata nchi iwe kame,
wanawake wanaume,zanzibari tete hali!

Kumbukumbu ya balali,kala kisicho halali,
watu tukawa wakali,arudishe yetu mali,
akakimbilia mbali,eti kenda sipitali,
haitaki serikali,kumrejesha kuzito!

Tutamkumbuka zitto,mjenzi wa hoja nzito,
bunge aliwasha moto,mawaziri viti moto,
kapewa adhabu nzito,eti aache utoto,
hawakutambua zitto,hojaze za wananchi.

mwendelezo jamani...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom