Tutafakari sote: Kwanini Zanzibar haichangii chochote shamrashamra za muungano?

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,592
36,005
Mtaalam mmoja wa Philosophy aliwahi kusema kuwa if "a=b" and "b=c" then "a=c" tukapata kitu kinachotafsiriwa "a=b=c"

Rais Magufuli kufuta sherehe za muungano na kuagiza fedha yote iende jiji la Mwanza kwenye shughuli za kimaendeleo nini tafsiri yake?

Rais Magufuli anafuta sherehe za muungano zinazojumuisha nchi mbili zinazojitawala kwa kila kitu (Huyu ni kiongozi asiye na mamlaka yoyote ndani ya Zanzibar). Wakati huo huo fedha hizo zote zimeenda kuinufaisha sehemu moja ya muungano (jiji la Mwanza) kwa Tanganyika.

Kwa maana nyingine swala la muungano na mambo yake yote halilihusu kabisa taifa la Zanzibar! Zanzibar mchango wake kwenye shamrashamra hizi ni kuwaleta tu viongozi wake ambao wanaalikwa na viongozi wa Tanganyika na baada ya hapo kila kitu kinabaki Tanganyika! Hapa kuna muungano kweli?

Sasa tumegundua kuwa kumbe sherehe za muungano zinaihusu Tanganyika pekee na viongozi wakuu wa Zanzibar wanakuja tu kama waalikwa wa nchi jirani. Hivyo basi sherehe za muungano ni mzigo mkubwa kwa watanganyika na hazina maana yoyote zaidi ya unafiki tu uliotukuka! Hatuna muungano wa nchi mbili bali kiini macho tu kinachotudananya mchana kweupee!

Tunamshukuru sana Mungu kwa kuendelea kutufunulia unafiki huu wa CCM ambao umejaa hila za hali ya juu.

Mabilioni yaliyotumika kwenye sherehe za miaka 50 ya muungano tuliyabeba sisi watanganyika huku wazanzibar wakijongea kama mwali kunywa na kula!

Huu unafiki wa CCM kujitafutia maslahi yake kwa hali na mali mwisho wake hauko mbali.
 
Back
Top Bottom