Hassan Mambosasa
JF-Expert Member
- Aug 2, 2014
- 3,371
- 4,564
Si kwamba najikashifu na kuwaambia mabaya, ila hili swali napaswa kujiuliza na pia mjiulize. Afrika yetu inafahamika ni sehemu ya giza, imekuwa ikipuuziwa na kuonekana moja ya bara la hovyo. Kila kukicha ingawa wapo ambao hujitahidi kuonesha ni mahali stahiki pema kama kwingine.
Silaumu watu wa nje kuongea hivyo, maana hawawezi kutambua thamani na ubora wetu kuliko sisi wenyewe tunavyojitambua. Bali nalaumu kwa wenzetu, ambao wamekuwa mstari wa mbele, kuonesha Afrika yetu ni sehemu iliyojaa wajinga na wasiyojielewa. Wakati wao wenyewe wanajihusisha na hilo, wanaunganisha wazazi na hata jamaa zao wengine kwenye suala hili. Hata kama uhuru wa kutoa maoni upo, tuangalieni na kitu cha kukiongea na kuunga mkono. Tumieni kumbukumbu na dondoo, za kushusha maoni yenu juu ya jambo fulani. Si kukurupuka, kisa mikinzano ya mitazamo ya siasa. Huu ni ulimbukeni na hata hao wanaotushambulia hututumia vizuri, wakijua kuna baraza la wajinga wataungana nao.
Mfano suala la chanjo ya corona, kulikataa si dhambi na hakuna mahali ambapo iliandikwa ni lazima kuipokea. Watu huamua waikubali au waikatae, tusitake kuambiana kuna mwema duniani kiasi cha kufikia kuhimiza kuichukua hiyo chanjo. Kwa wenye uhitaji kidogo, huku kwao palipo na watakaji waliyopitiliza kuwe bado hakujamalizwa.
Jamani sote tunajua mahali penye shida kubwa ndiyo huongezwa msukumo wa msaada fulani, kuliko kule ambapo ipo kidogo. Mfano miundombinu kwa Tanzania, huelekezwa Dar es Salaam zaidi kwakuwa ndiyo kwenye tatizo kuliko sehemu zingine zozote.
Kwani watu walikuwa wakikaa hadi masaa manne barabarani kisa msongamano, ndiyo wakaongezewa ili kutatua tatizo hilo. Huwezi weka sehemu ambayo haina msongamano, ni upotezaji wa rasilimali. Ndivyo ilivyo hili suala la chanjo, lazima ianzie huko kwenye shida kubwa kuliko kuja kuibwaga mahali hapa. Kwa huruma gani mliyokuwa nayo, hadi mje kutumbuka sisi na kusahau maelfu ya watu wanafariki kila kukicha huko walipo. Tusitake tudanganyane wameona faida yetu kuishi kuliko wao.
Hadi huyu mwanamama kutoka Afrika ya kusini, anayejiita mwanaharakati afikie kutoa maoni yake. Ambayo kwangu ni matusi na kebehi za waziwazi kuonesha waafrika sisi ni vinyesi, maana naambiwa ni mtu kutoka Afrika ya kusini, ila alivyoongea kama anajitoa vile si kutoka bara lile. Yote kisa tu mitazamo ya watu, waliyoelemea kiitikadi na imani zao zingine juu ya jambo hili… Hivi huko nje ya Afrika hakuna watu wa wanaoelemea kiitikadi? Wakitoa mawazo ambayo ukiyachuja na chujio ubongoni. Huwezi ona mantiki yeyote, hata ukadhani yumkini aliyetoa wazo hilo ni mwendawazimu.
Je, hao huwa wanaongeleea kikebehi na kutukanwa bara zima kisa mawazo, matendo yao mengine na hata imani itakapoelekea? Hamuishii kusema ni uhuru wa watu kujieleza na kufanya maamuzi yao binafsi kama wanadamu.... Wapo ambao wanajioa wenyewe, wanatumia pesa nyingi ilo wafanane na nyoka kiasi cha kufikia kukata masikio yao.. Mwingine alitaka afanane na fuvu, yaani awe kama baki la mfupa wake akiwa bado akiwa hai. Ila hakuna kutoka huko kwao aliyewahi kuwakashifu, zaidi ya kuonekana ni uhuru wa mtu….. Iweje waafrika wenzetu kuhusisha chanjo ya corona na chapa ya shetani, mpinga kristo au kupunguza vizazi ndiyo iwe mawazo ya kipunguani kiasi cha kufikia kushushiwa kashfa pishi nzima? Nao si wana uhuru wa mawazo? Au haki yao wanayo wazungu pekee, ngozi nyeusi hii hatuna hiyo?.... Mwanamama Tricia atujibu hili kwanza.
Haya kufikia kutaja waafrika sisi hatuwezi kutengeneza dawa ya meno, mswaki, chupi, hata panadol. Kisa kukataa chanjo hiyo tu, eti kama vinatushinda tutawezaje kuunda hiyo chanjo. Hivi toka lini Mwafrika akabuni kitu kizuri kwa afya ya wanadamu duniani, mkaweza kukiunga mkono kama kipo kinyume na mitazamo yenu. Si mtaishia kusema mpaka mthibitishe nyinyi, ila kikitoka kwenu huko tukipokee moja kwa moja kama chakula kilichotoka kinywani kwa ndege kuja kwa kinda lake. Kwa msingi huo hata tukiunda na kutumia, si mtaanza kuzipiga propaganda mbaya, zionekane hazifai.
Sawa condom hatuwezi kutengeneza, sijui hawa PSI TANZANIA huwa wanatengeneza soksi za kuvaliwa ulaya. Ambazo huku Tanzania tunaziita SALAMA CONDOM. Maana tumeambiwa hatuwezi kumudu hizo, kama si kashfa hii ni kitu gani. Halafu kuna wenzetu wanaendelea kuunga mkono hili, ndiyo maana nauliza. TUTAENDELEA KUWA WAJINGA HADI LINI?
Yaani dawa za meno ambazo zimejaa, wakiunda wazawa napo tumeambiwa na huyu Bibi Tricia kuwa hatuwezi kutengeneza hiyo. Kisa tu colgate aliyoitaja imetoka nje ya Afrika. Akataja na zingine kadhaa, zinazotumiwa Afrika…. Jamani hili jambo si matokeo ya soko huria, ndiyo bidhaa za kutoka sehemu fulani zinakuja kwingine.. Haikumaanisha hatuwwzi kuunda hizo waafrika, watu wanatengeneza sana, ila kuruhusu bidhaa za nje kuwepo ndiyo imefanya hizo zikawa sokoni. Si kwamba zikikosekana basi, ndiyo mwisho wa watu kupata dawa za meno.
Hili jingine ni tusi eti hatuwezi kutengeneza chupi tunanunua za mitumba kutoka nje. Hivi anayaropoka haya, amekuja kufanya utafiti huku? Yaani nguo ziundwe ishindikane chupi. Hizo bidhaa zote zipo kwenye nchi zetu, kupokea za kutoka nje haimaanishi hatuna na tuna shida nazo. Bali ni matokeo ya sera za biashara huria hapa, na hata zikikosekana hakuna ambaye atatembea bila nguo ya ndani…… Yaani tuweze kuunda mabodi ya mabasi yetu kwa kutumia injini za kuagiza, kama wafanyavyo Yutong ns Zhongtong kutoka nchini China wanaonunua mashine Cannings, ndiyo lije kushindikana chupi kutengenezwa ilihali hadi viwanda vya nguo vipo.
Viwanda vya dawa navyo vipo hapa, hata panadol na zingine za kupunguza maumivu zinatengenezwa hapa Afrika kwa muda mrefu tu. Kuwepo kwa bidhaa za nje isiwe kigezo cha kutukanwa na kudhalilishwa kiasi hiko. Tiba zipo na zitaendelea kuwepo, tena kuna hata za asili zina nguvu kuliko zao.
Turudi palepale suala la chanjo kama mitazamo ya watu inaheshimiwa, basi akae kimya. Asichukulie sehemu ambazo wazungu walijitolea kusaidia, ndiyo fimbo ya kutuchapia. Kama hivyo vyuo vya elimu ya juu alivyotaja vimejengwa na wageni, akumbuke tunavyo vingi vilivyojengwa na wazawa na vinafanya vizuri. Kusaidia kimoja isiwe sababu ya kukashifu elimu nzima, wakati vimejaa lukuki hata vimezidi ubora walivyojenga wao…. Chanjo ni suala la hiyari, hii itabaki vilevile. Bibi Tricia aheshimu maoni na mitazamo ya watu, kama anavyoheshimu wanawake wenzake wanaoamua kujioa huko Ulaya bila kuzungumzia lolote kama mwanaharakati.
Bado haya mambo unakuta mwafrika mwenzetu anashawishi wengine, kisa maneno ya kashfa na kuweka vigezo vya uongo ndani yake. Hata hajatafakari na kuchunguza kuhusu tuhuma alizotushushia. TUTAENDELEA KUWA WAJINGA HADI LINI?
Sipo kwa ajili ya kubomoa, bali kujenga. Hata ukichukulia haya niliyoyaandika kwa mtazamo hasi. Ni sawa umeamua na hayo ni maamuzi yako, siwezi kukulaumu hata ukiangusha neno bovu. Ila tuangalie uhalisia wa mambo, si kukubali kutukanwa na mmoja kisa ni mwenye ngozi nyeupe mwenye uraia wa hapa. Akihimiza tupokee tusichokipenda, eti kama wazungu wangetaka kutuua wangeshafanya siku nyingi. Tukashifiwe kuhusu viwanda na vyuo vikuu, wakati mzungu alipofika Afrika alivikuta vipo akafanya kuviua kwa maslahi yake binafsi. Fikiria kwa mtazamo chanya.
Wasalaam,
Hassan Omar Mambosasa
Juniormambosasa@gmail.com
Tanga Tanzania
2021