Akiwa rais wa watanzania wote huyu ni kiongozi wetu ambaye hata kama hutaki yeye ni rais tu, Ukuu huo na dhamana hio iende sambamba na vile anavyopaswa kuwa. Kwa kuwa ni rais haina maana yuko juu ya katiba hapana. Anatakiwa awe mfano kwa kila afanyalo.
Kuna mambo anafanya na akifanya yaliyo mazuri tutampongeza sana, vile vile akikosea tutamsema tena bila kujificha lakini kwa kutumia staha na heshima. "Hii ni alfa na omega" au "haki na wajibu"
kila mmoja atende haki na atimize wajibu.
Naam, rais wetu tutamkosoa. Mwenendo wa kauli zake, maamuzi na baadhi ya tabia zake haziridhishi. Analimega taifa na kuleta chuki na visasi. Rais wetu awe mvumilivu na kutumia mbinu mbadala za kiuongozi kutimiza dhamira njema aliyo nayo kwa watanzania kama anayo. Najisikia vibaya kuwa rais wetu kila akizungumza hadharani basi atakera watu tu. Hakukuwa na sababu kule kagera kutamka yale maneno ya kuhusu mafuriko na kukatisha watu tamaaa tena waliopatwa na majanga yale.
Hakupaswa kutamka lugha zile za fyoko fyoko kule Pemba na Unguja katika taharuki ya uchaguzi wa Zanzibar. Hakupaswa kuwajibu wananchi waliotaja njaa kuwa serikali haipiki ugali katika moja ya ziara zake mikoani hivi karibuni. Mifano iko mingi mengine haifai kusemwa inaaibisha.
Katikati ya haya yanayofanywa na Rais wetu, kuna baadhi ya wana CCM hasa mitandaoni hujibainisha kwa ubishi na kupinga wakisema eti hakuna tatizo maana watanzania walizoeya kubembelezwa. Hapana na wala huku sio kukakamaa, ni maudhi kwa wastaarabu wengine. Unaweza kuwa mkakamavu bila kumuuudhi mtu. Lugha za Rais wetu sio nzuri kamwe na wachache wanaojitokeza kuzipinga wanajitolea muhanga kwa faida ya wengi walio kimya wanaoogopa. CCM msaidieni Rais JPM kwa maslahi yenu kichama na nchi. Vyenginevyo mkae kimya muache sisi wengine tumkosoe na tumseme. Hakukuwa na sababu ya kutamka maneno yale ya kukatwa umeme ikihusisha Zaqnzibar ambako kuna mamlaka fulani ya kiutendaji, Majibibizano yale na dr Shein hata kama hayakuwa ya moja kwa moja, hayaleti afya kwenye Muungano wetu. Hivi kama kiongozi tena mzoefu kwenye serikali alishindwa nini kufanya vikao vya ndani na kuagiza wanaohusika kutatua tatizo mpaka aje hadharani atoe maneno yale?
Lawama za kauli za rais zisizochunga mipaka zinaendelea kulalamikiwa na makundi mengi, Baadhi ya maamuzi ya rais yanaumiza kichwa na yanaonesha ama sio shirikishi au wasaidizi wake wanamuogopa. Sijui huko CCM lakini huku kwenye umma yale baadhi tunayoona yanaashiria hivyo. Inajengwa hoja kuwa Rais anafanya kazi kwa kufuata katiba ndio, lakini njia inayotumika baadhi ya wakati inakera. Unamwita mfanyakazi mtendaji au mbunge unaanza kumsuta kwa maneno , unamsimamisha kazi hadharani kwa kustukizia bila ya kupata muda wa kujiridhisha, unatishia kufukuza watu , unahamasisha watu wajichukulie hatua mikononi(sakata la kutoa tairi gari zitakazopita barabara za BRT), unahamasisha lugha za ubabe katika kazi.
Katika hali hiyo hatutamsifu Rais, tutamkosoa na tutamwambia hivi sivyo. Uzoefu wake serikalini tunauhitaji utusaidie kupata maendeleo katika misingi ile ile ya "utu" na "kuheshimiana" kimoja kisiwe juu ya chengine. Kwa kipindi hiki cha kushika wadhifa wa juu wa nchi tumemuona hasa alivyo Dr Magufuli. Tumembaini kasoro zake walau kwa kiasi hicho. Hatupaswi kuzipuuza kasoro hizo eti kwa kuwa ana nia njema. Nia njema sio tiketi ya kuvunja utu na heshima za wengine. CCM mtuvumilie tu.
Kishada