Tutaanza kukenua sasa

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,454
Reaction score
872,070
January ilikuwa ngumu mno December na watoto waendao shule walipukutisha visenti vyote mifukoni na vibindoni watu wakawa hawasalimiani kwa mdomo kwa msg wala kupigiana simu
ukisikia simu inaita unafikiri ni mzinga unakuja watu wakawa wakali na wengine kukimbiana
fridge zilizokuwa zimesheheni mapochopocho December zikabaki tupu na madumu ya maji tu na nyingine kuzimwa kabisa
lakini naona kuanzia leo watu wataanza kukenua na tabasamu zao kuonekana tena na nyuso zitakunjuka sasa maana January hiyooo inayoyoma na akounti zimeanza kucheka hata mabar na wahudumu wake vitapata uhai sasa bila kusahau mipaka ya bar na mbwakoko wa uswazi
 
Wengine tutacheka mayb on April!
Mitoto mi3 yote skullfizi bodin , plus vitendea kazi vyao!
Same January rent ya banga!
Mziki mnene Babaake !
 
Wengine tutacheka mayb on April!
Mitoto mi3 yote skullfizi bodin , plus vitendea kazi vyao!
Same January rent ya banga!
Mziki mnene Babaake !

mkuu kumbe nawewe uko macho? hatujasalimiana kabisa mwaka huu....yani usingizi umekata mazima !kweli siku hizi tunawekeza kwenye elimu
 
Mwezi December hata wapenzi wengi (wasio wanandoa) huwa wanaachana -inasaidia kupunguza gharama na maandalizi ya kuikabili Mwezi mgumu January
 
february oyeeee...thank God u r here
 
Mwezi December hata wapenzi wengi (wasio wanandoa) huwa wanaachana -inasaidia kupunguza gharama na maandalizi ya kuikabili Mwezi mgumu January

December noma mkuu, ni mwezi ambao nyumba ndogo zinazidisha mapenzi ile mbaya, hasa kabla ya sikukuu wakati mzee mzima mapenzi ndo yanakufa kabisa!! Hata akikupigia simu hupokei!! Huwa ni low season kwenye suala Zima la mapenzi!
 
hapana, mimi nitaanza kupumua kuanzia mwezi april tena kwa mbaali....!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…