Tusiwaite wahadhiri kwenye siasa na kuwaumbua.

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
13,585
14,045
Wasomi wengi hawaingii kwenye siasa kwa hiari yao, wengi wao wanafanya kuingizwa kwenye siasa kwa kuteuliwa na wanasiasa wakidhani kuwa elimu na uongozi ni kitu kimoja. Matokeo yake wanapofika kwenye siasa huwa wanaingizwa mjini na wezi wazoefu waliowazunguuka pande zote.

Kutokana na umbumbu wao kwenye mfumo wanaishia kutimuliwa kwa aibu kubwa kutokana na makosa ya watu wengine.

Kwanini wasomi msifanye Kazi zenu mlizozisomea na kuzizoea mazingira yake kuliko kuingia kwenye siasa ambazo hamziwezi?

Tafakarini kwa makini
 
natafakari kama ile kamati imethibitika ni uwongo je hasara tutakayopata kama nchi nani atakuwa liable? naomba mungu report yao iwe sawa
 
Back
Top Bottom