Mchokoo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2015
- 1,179
- 1,579
Watazame vizuri watu hawa, utagungua kwamba kwa sasa wengi ni wasomi na hata wale ambao hawakwenda shule bado wana uelewa si haba!
Sasa kumbe tatizo liko wapi?
Shida yetu kubwa sisi watanzania na huenda waafrika kwa ujumla sisi ni waoga mno!
Si laia wa kawaida, wala Chama tawala, Upinzani, Taasisi za kidini, asasi za kilaia nk, wote ni uoga tu kwa kwenda mbele!
Ni hapa kwetu ambapo utashangaa kuona chama tawala kikiogopa uwepo wa tume huru ya uchaguzi ilihali haohao wanadai kupendwa!
Ukiachana na hao, utastaajabu zaidi kuwaona wapinzani wakiogopa mno kudai tume hiyo huru; ingawa wanadai kuibiwa kura kila uchaguzi.
Kama hiyo haitoshi katika hilo tatizo letu, rudi kwetu sisi wananchi wa kawaida.
Mbona tumeogopa kuidai katiba mpya?
Hivi tulitumia pesa kiasi gani kama taifa?
Ni nini kilichotukwamisha? kama si watu fulani kuogopa kuguswa maslahi yao?
Hivi huu uwoga wetu utaendelea kuligharimu taifa hili mpaka lini?
Ndugu zangu hawa wazungu tunaowasifia mno wangekuwa waoga kama sisi wasingekuwa hapo walipo!
Mwaonaje iwapo mwanamke angeogopa maswaibu yanayoambatana na ujauzito; basi leo hii tusingekuwepo!
Kinachowapa ujasiri wanawake ni kuangalia faida ya uzazi kuliko kuhofia maumivu yake.
Nimeshangaa kuwa hata Mwenyezi Mungu hatakubari waoga waingie mbinguni.
Soma ufu. 21:8