Tusikitike kwa wanamichezo wetu wanaposhindwa,kuwabeza sio Uzalendo

Sheikh23

JF-Expert Member
Jul 11, 2016
1,128
1,842
Wadau habari,kumejengeka utamaduni usiofaa wa kubeza,kukejeli na hata kutusi pale wawakilishi au muwakilishi wetu kwenye shindano au mashindano fulani anapo_fail. Binafsi sijui roho hii mbaya wa_tz tunaitoa wapi,mahala tunapopaswa kusikitika tunafurahi,tunapopaswa kumtia mtu moyo na kumfariji tunamcheka,kwa utamaduni huu tutaona medali na tuzo mbalimbali zikienda nchi za wenzetu tu,maana tunatumia nguvu kubwa kuwarudisha nyuma mashujaa yetu kwa kufurahishana mitandaoni pasi na posho yoyote
Jana bondia mtanzania mwenzetu Abdallah Pazi "Dulla Mbabe" amepoteza pambano,leo mitandaoni anabezwa kwa spidi ya 5G as if kwenye michezo wa-tz tumeumbiwa kushinda tu.
Dulla sio bondia wa kwanza kupoteza pambano,wamepoteza kina Tyson,Evander,Bruno na wengineo enzi hizo,na hata jana Bondia Mkubwa Deontay Wilder amechapika mbele ya Tyson Fury.
Wa-tz na media zetu zinapaswa zijifunze uwasilishaji wa taarifa haswa kwa mambo ya National Interest pale yanapo_fail na sio kuyashangilia kwa style ya Juma Lokole
Tujifunze kujenga kuliko kubomoa.
Nawasilisha...
Screenshot_20211010-132200_Facebook.jpg
Screenshot_20211010-131752_Facebook.jpg
 
Back
Top Bottom