Tusifichane shemeji zetu!

Mchimbwi

Member
Joined
Jan 6, 2013
Posts
38
Reaction score
4
Hii ni kweli na ilitoke juma lililopita maeneo ya Dsm.marafiki wawili walioshibana,kujaliana na kuishi kama ndugu walipo kosana kisa huyu bint!mmoja kati yao alikuwa na mpenzi lakini hakupenda kumtambulisha rafiki yake,hawa jamaa walikuwa wakiishi umbali kadhaa,hivyo huwa wanatembeleana.sasa sikumoja inadaiwa yule msicha alikuwa matembezi ya kawaida ndipo alipokutana na mmoja kati ya wale marafiki,ofcouse ni cute girl.jamaa akaseduce shem wake bila kujua na yule demu akaitika wito.siku moja huyu msichana aliaga anakwenda matembezi kumbe alikwenda kwa yule rafiki wa bwana wake.kufika pale baada ya maongezi mambo yakawa mpwitoto,kisha jamaa akamtaka yule binti aandae chakula kwani kuna mgeni atafika muda si mrefu.mgeni huyu hakuwa mungine ni yule rafiki yake kipenzi.basi wakiwa wamepozi kwa mbwembwe zilizojaa mahaba ghafla mlango ukagongwa,ndipo jamaa alipomruhusu rafiki yake kuingia ndani,ile jamaa anaingia alipotupa jicho kulia na kushoto anaiona sura ya mpenzi wake kipenzi amekumbatiwa kimahaba.kwa kweli kilichotoke hapo ni balaaaaa.....!!TUSIFICHANE MARAFIKI KUTAMBULISHANA.
 
Vipi na wale marafiki tunaowatambulisha afu wana-overtake?
 
Lakin kwanini dada zetu wasiku hizi ni matapel wa mahaba, hona sasa huyo dada anajua ana mtu wake lakin tamaa ya mapenz imemzid, haya we kagombanisha maswahiba walioshibana
 
Kwahiyo bora kipi!!!!

Hatari ya kunyang'anya mpenzi na rafikio akiwa anamfahamu ni ndogo kuliko kama hamfahamu;
Maumivu ya kunyang'anywa mpenzi ambaye rafikio anamjua ni makubwa kuliko asiyemjua.

@Evelyn Salt;
Kupanga ni kuchagua;
Kuchagua ni uamuzi wa mhusika;
Mhusika ni wewe mwenyewe.
VodaCom (Kazi ni Kwako)
​


Bazazi!
 
Tatizo ni mdada wala sio kutambulishana..Hafai tu kuwa na yeyote kati ya hao marafiki..Mii ningewashauri hata wasiharibu urafiki wao kwa mtu asiyestahili
 
Lakin kwanini dada zetu wasiku hizi ni matapel wa mahaba, hona sasa huyo dada anajua ana mtu wake lakin tamaa ya mapenz imemzid, haya we kagombanisha maswahiba walioshibana

Si utapeli madada wana danganywa sana na hawa makaka, na huwa awamakaka si wakweli na hawana ahadi timilifu, madada wanabahatisha yule atakayeweza kumpa ahadi timilifu na yenye mwelekeondio maana wanakosa msimamo, na chanzo ni makaka!
 
Kwahiyo bora kipi!!!!
Ukitambulisha wanabwenga, usipotambulisha wanabwenga vilevile, sasa bora utambulishe ili huyo m'baya utakapomfanya kitu mbaya usilaumiwe na yeyote. hadi yeye mwenyewe hakulaumu
 
Ndugu yangu hapo sio suala la kutambulishana tena,kwa ufupi mdada mwenyewe hajatulia kwa nini awe na mtu mwingine tofauti na mpenzi wake?hata kama angetambulishwa si ajabu bado angetoka,wangapi tumewaona wanawasaliti waliowaosimamia kwenye ndoa?Asante kwa ujumbe lakini msg sent kwa wasipoenda kuwatambulisha ma sweety wao.
 

kuna mashost hawana adabu!!!
kazi kujilengesha kwa mashemeji zao huku ushawatambulisha!!!!
 
Duuuh, kimeeeo hicho, ni cha kukichana na kukiacha tu!
Mi na mshikaji wala hatugombani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…