singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
WATANZANIA wanaweza kukomesha rushwa nchini ikiwa watakubali na kujitoa kwa dhati kuhakikisha haiendelei. Rushwa nia adui wa haki na ni chanzo cha baadhi ya watu kuwa na maisha yaliyo juu sana, huku wengine wakisuasua kuyafikia hata yale ya kati.
Ni tatizo linalohitaji kumalizwa kwa nguvu ya pamoja kwa Watanzania wote kuwa tayari kutoa ushirikiano kuiambia sasa basi kwa vitendo. Palipo na rushwa maendeleo hudorora au kutokuwepo kabisa, kwa maana hiyo, rushwa ni adui anayepaswa kufanyiwa mkakati wa kudumu wenye nguvu ya pamoja na wenye uhakika wa kufanikiwa ili isipate nguvu.
Tunafahamu jitihada zinazofanywa na viongozi wetu kuikomesha lakini mafanikio kwa asilimia 100 yamekuwa yanachelewa kufikiwa kwa sababu kati yetu wananchi na viongozi wapo wanaoomba iendelee kuwepo siku zote, ili wazidi kuneemeka. Wapo wanaoogopa kuikemea hadharani na wapo wanaoikemea kinafiki.
Kwa mtindo huo, haiwezi kwisha hata kama tutapiga kelele namna gani. Alhamisi ya wiki iliyopita Rais John Magufuli alikutana kwa nyakati tofauti na Rais mstaafu, Benjamin Mkapa na Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba kwa mazungumzo Ikulu, Dar es Salaam.
Viongozi hao, pamoja na kumtakia Rais Heri ya Mwaka Mpya, waliahidi kumpa ushirikiano atakaouhitaji ili kufanikisha majukumu yake, huku Jaji Warioba akienda mbele zaidi kuwaomba Watanzania wasimwachie Rais kazi ya kukomesha rushwa, bali wampe ushirikiano.
Katika mazungumzo hayo, Jaji Warioba alisifu kuanza vizuri kwa Rais Magufuli kutekeleza majukumu yake ambapo alieleza wazi kuwa ameonesha mwendo mzuri katika suala la kuhakikisha mapato ya serikali yanakusanywa na kubana ufisadi.
Alichokisema Warioba ni sahihi, nasi tunakiunga mkono kwa asilimia 100, huku tukiwaomba Watanzania wenzetu popote walipo wasiifumbie macho rushwa au kuficha wala rushwa na watoa rushwa.
Maneno ya Jaji Warioba yana mantiki na yanaweza kuwa mkakati mzuri zaidi ikiwa Watanzania watayafanyia kazi kwa vitendo kwa kutoa ushirikiano pindi wanapotakiwa, hasa wanapokuwa na taarifa mbalimbali kuhusu suala la rushwa linalochunguzwa au kutakiwa litolewe ushahidi iwe mahakamani au kwenye taasisi husika.
Umoja wa kweli wenye malengo yanayofanana yenye nia ya kuleta maendeleo kwa wote siku zote huwa na nguvu inayoweza kumshinda adui hata kama atakuwa amejiwekea mizizi kiasi gani. Kwa hiyo, ni rai yetu kwa Watanzania kuuonesha umoja huo sasa kwa kushiriki kukomesha rushwa bila hofu, woga wala uonevu.
Tunaamini pia kuwa, penye malengo safi ya kuletea nchi maendeleo, hata kama kutakuwa na maumivu kwa wachache wanaojipendelea kwa sababu ya ubinafsi na uroho wa kujineemesha kwa kutumia njia za rushwa zisizotakiwa, Mungu naye huweka mkono wake kuzuia wasiendelee kuumiza wengine.
Rushwa inaweza kubadili faraja ya nchi kuwa majonzi, hivyo kila mmoja ajitolee kuikomesha, kama alivyoshauri Jaji Warioba. Nguvu ya Rais ikiunganishwa na ya wananchi rushwa itakuwa historia Tanzania