tushirikiane kuishitaki CCM kwa kuliingizia taifa hasara!

Jaslaws

JF-Expert Member
May 31, 2011
6,016
5,296
Habari wadau,kama kichwa cha habari kinavyojieleza,
Natafuta vijana wanaojielewa wanasheria na wasio kuwa Mwanasheria,tupange mikakati tuone ni kwa jinsi gani tunaweza kuwashitaki hawa CCm kwa kuliigiza taifa katika hasara zisizokuwa na msingi!!
Najua wamepewa ridhaa na wanachi kuongoza nchi,ila sio kwa Namna wanayofanya,tangu miaka ya 70 ccm wameruhusu rasilimali za nchi hii kuibiwa kiolela na hakuna anaewajibika,hivi karibuni kwenye swala la madini na makanikia tumeona wapuuzi wachache wa ccm waliingia mikataba ya siri ambayo sisi kama taifa tumepoteza mapato mengi sana bila sababu, baada ya mambo kuharibika wanajivisha uzarendo na kuanza kutulaghai kwana kwamba kuna jini lilitoka morocca ndo likasign huu upuuzi,na kwa bahati mbaya wananehemeka wao na familia zao.wametuacha asiimia kubwa ya wananchi tukilowea kwenye dimbwi la umasiki pasipo kuwa na mtetezi wamefanya sasa zitutawle tushindwe hatankufikiria mambo ya msingi.
natoa wito kwa vijana wenzangu tujitokeza tukadai haki na rasilimali zetu zilizoibiwa mahakamani siasa zimetosha..tuache ushabiki wa siasa tuwe kitu kimoja tupambane kwa ajili ya wadogo zetu na vizazi vijavyo..historia itaandikwa.
Binafsi Niko tayari kutoa ada zote za kimahakama kwa ajiri ya kesi hii.karibuni kwa michango ya kujenga kama unahisi haiwezekani pita kushoto!!
 
Badala yake tudai katiba mpya, maana katiba ya sasa ya ccm inaruhusu kuwepo kwa mikataba ya siri inayohusu rasilimali zetu.
 
CCM ni taasisi ambayo inajumuisha watu wengi sana na ninaimani kuwa kama si Wazazi wako au babu au bibi walikuwa wanachama wa CCM je na wao tuwashitaki? hakuna asiye mjua ambae ametufikisha hapa hata mtoto mdogo anamjua aliyetufikisha hapa hila siku zote pamoja na yote na udalali mkubwa alioufanya Tanganyika lakini hakuna aliyejitokeza na kumsema au kusema japo wanasemea chooni au bafuni lakini si hadharani kwa vile ni mwanataasisi ambayo inamlinda taasisi ambayo ni ya pili kwa kukusanya mapato makubwa baada ya FIFA
 
Badala yake tudai katiba mpya, maana katiba ya sasa ya ccm inaruhusu kuwepo kwa mikataba ya siri inayohusu rasilimali zetu.
Huyo mikataba haiwapi mamlaka ya kutuvuruga na kuiba rasilimali zetu Namba hii bwana,ccm wanajificha nyuma ya siasa..maandamano hatuwezi twendeni mahakamani tu..
 
Badala yake tudai katiba mpya, maana katiba ya sasa ya ccm inaruhusu kuwepo kwa mikataba ya siri inayohusu rasilimali zetu.
Katika mpya,uko tunarudi tena kwenye siasa ambacho ndo kichako wanakojificha,tunatakiwa kutumia Silaa tofauti na zakwao!!
 
Back
Top Bottom